Tuliowahi kuachwa: Ni changamoto gani uliyokumbana nayo baada ya kuona umeachwa?

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwa Tuliowahi kupigwa vibuti, hebu tukumbushane changamoto tulizowahi kupitia baada ya kuona hapa sasa nimeachwa.

Mimi upande wangu nilipata tatizo la presha kushuka week mbili nimelazwa hospitali lakini pia mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kasi hatari.

Haya tuendelee
 
Mimi niliwahi kupata vidonda vya tumbo kutokana na mrundikano wa mawazo.

Kawimbo.
Kuachwa kuachwa, kuachwa nishughuli pevu,
Unaweza kukonda wakati huna ugonjwa,

..Kuna binti mmoja aliniacha kwa jeuri na matusi hadi leo nikikumbukaga basi tu lakini cha kushangaza siku moja ananipigia wakati huo alishaolewa halafu anapiga kwa namba ya mmewe anasema hatuko vizuri na mme wangu,

Akawa ananipigia mmewe asipokuwepo tuliwasiliana kama siku mbili tukatemana mazima, sijui alifikiri mi ntashoboka na nikikumbuka lile tusi Acheni bhana.
 
Nilikuwa napiga simu mfululizo,,
-- Hazipokelewi...
--SMS hazijibiwi,

Karibu siku tatu nzima.
Baada ya simu zangu kuzidi kusumbua mfululizo..
ikaja sms 1 tu toka kwake.

""Kwani mapenzi lazima""?

Aisee nilitetemeka sana,,halafu nikaitafakari sana ile kauli yake,

" ,,, Kwani mapenzi lazima?"
Mwishowe nikakubaliana na hali ya kuachwa,
Ikabaki kumbukumbu za love songs na matukio tuliyokuwa pamoja...

Nikisikia love songs tulizokuwa tunatumiana,,
kama kunogesha penzi,,
wakati ule wa mapenzi yetu matamu,,naumia sana.

Nikizisikia zile songs popote pale,,
nahisi roho yangu inataka kutengana na mwili..

Nakumbuka nyimbo moja ya bushoke jina siikumbuki ,
Ila amepiga na Dada Mmoja hivi,,

""Deka unavyodeka kama mtoto"

""Nitakubembeleza mm niwako ohoo.""

"Nitazidi kupa vitu moto moto"

"Mapenzi ni kupendana sio mchezo ohoo."

"Maumivu ya mapenzi yanauma sn,"

"Hata wivu sinao bali sina roho ya chuma.."

"Usiende mbali namiii,,""

""Usiende mbali namiiii ""

Mkuu hii nyimbo ilikuwa nikiisikia popote utanionea huruma,,
Kwa mawazo na hisia kali juu ya mapenzi wangu yule.

Moyo na roho yangu vinauma hatari,
Nilikuwa nateseka sana bila kujali mahali nilipo,,,mradi tu nisikie wimbo huo.

Saa ,siku,,week, ,miezi ilipita mwishowe nikasahau kabisa.,

Ilipita miezi kadhaa,, kuna siku nikakutana na yule ex wangu ,,
Yule aliyenifanya nikonde kwa mawazo.
Hata nikajiona sina faida ya kuishi hapa duniani bila yeye.
Tena yupo na jamaa mmoja mnyonge sana kushinda Mimi,,

jamaa mwenyewe kachomekea suruali fulani hivi na shati limepauka mgongoni hatari,,,
kakaza sana mkanda wa suruali.,
Hata kiuno kikawa kidogo kama cha ngedere..

Nilishangaa sana..
Nikajiuliza hivi mimi nilikuwa naumizwa na nini toka kwake huyu demu?
_Mbona huyu msichana wa kawaida sana?
-- Hata bure simtaki.,,
Duu!! hebu angalia wanaume anaotoka nao kwa sasa..!!
Nilishangazwa sn..

Aisee!! Kumbe kinachokuumiza ktk mapenzi ni hisia zako mwenyewe

Tupunguze kuwa na hisia Kali za mapenzi kwa tunaowapenda ,,
kuepusha maumivu makali wakati wa kuachwa...

Kumbuka

"Hata mapenzi pia yana date of issue...na date of expire...."

mark my words
 
Dah kweli aisee yaani hata mimi hali ilkua ngumu sana nakumbuka nlikua Dar naishi geto nilikua nalala tuh sikua ham na chochote, Ilinibid nianze kuzurula napanda gari asubuhi naenda Morogoro alafu narud jioni ili akili yangu ikae busy somehow ila baadae nilizoea na nkaapa sitarudia huo ujinga aisee make nlimwamini sana na nilikua na malengo makubwa na huyo demu kumbe alikua ananichora nlikua nimesimamishwa kazi nikaendelea na kazi maisha yangu ni kuignore mademu naisha maisha ya Hit and Run alafu huyo demu alipokimbilia na penyewe aliachwa😃😃😃😃😃😃
 
Nilikaa mwaka mzima bila kutongoza wala kupiga mzigo maana nilikiwa nawachukia watoto kike mpaka akili zinarudi napiga mzigo aisee hadi nilikohoa damu siku tatu mfululizo aisee hadi kuna nyimbo huwa sizipendi kwa sababu zilitoka kipindi nimemwagwa mfano hakunaga ~ Sumalee lakini toka hapo sijawahi kuruhusu hiyo hali na haitatokea tena maana ilinikomaza
 
Wanasemaga what doesnt kill you makes you strong.

Ikishakutokea mara ya kwanza ikija jirudia tena hali inakuwa tofauti na mwanzo unajionea kawaida hata ukiumia sio saana.

Ila mapenzi bwana yanaweza kusababisha ukaonekana kituko hata ukirudi katika hali ya kawaida halafu ukavuta picha wewe ndio ulikuwa unafanya hivo vibweka kisa maumivu unajishangaa.
 
Hahahaaaa, hakuna maumivu nimewahi yapata kama siku nilikua na 10k nikaenda nunua valeur 8k na coca ya kuchanganyia, nikiwa narudi geto kibarazani nikateleza kwenye tiles ikapasuka, machozi yalinilenga nikawa nahema kwa kasi sana, joto likapanda na nkahisi kama nataka kutapika na kuzimia kwa wakati mmoja... nilikaa siku 3 kwa huzuni sana... mpaka leo niko makini nikimbeba mpenzi wangu valeur
 
Kuna Jamaa yangu aliachwa na demu wake Pindi tupo form 3, Nakumbuka Jamaa alilia sana siku hiyo.. Usiku wa siku hiyo jamaa alibeba panga kwenda kumuua huyo demu. Tulikuwa na Washkaji wengine tunapiga msuli maana tulikuwa tunakaa geto, Mwenye nyumba ndio alimuona Akaja kutuuliza mbona mwenzenu kabeba panga anaenda wapi usiku huu?

Ndio na sisi tukasanuka na kwenda kumkamata tumrudisha ndani tukamtuliza akatulia maana alichanganyikiwa Balaa.. Basi na Mimi tokea siku hiyo nikajifunza kubalance upendo kwa mwanamke
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom