Tuliowahi kuachwa: Ni changamoto gani uliyokumbana nayo baada ya kuona umeachwa?

2018
ghafla mtu hajibu sms..cm hapokei..hali ile iliniumiza sana sana coz haikuwa kawaida yake kabisa..akijibu sms anajibu kwa mkato nikiomba tuonane hataki hapo kipindi hicho nipo high school na nina siku kama nne tangu nimerudi maskani sijaonana nae.

Nilipoona maumivu yanazidi na sijui sababu ni nini
Mimi mwenyewe kwa mdomo wangu nikamwambia tuachane..haaa aisee sitasahau

Binti alikazia hapo hapo..nikaanza kuomba msamaha..omba msamaha..omba msamaha wapi..nakumbuka siku hiyo wakati natuma hiyo sms ya kuachana nilikuwa nimejilaza kwenye kochi..aisee

Nilikuwa nashindwa hata kunyanyua cm naona cm nzito kunyanyua ..mwili umeishiwa nguvu kabisa ..

Nilimbembeleza usiku kucha.binti alikataa kata kata

Wiki nashindwa kula..nalia kama mtoto..
With time kidogo kidogo nikaanza kurecover..baadae nikaja kusikia binti ameolewa..jamaa aliemuoa amenizidi kila kitu pesa,umri,mwili..yaani kila kitu
Daaaah maumivu yalianza tena..hadi leo moyo unashituka sana nikimuona..

Now binti ana watoto wawili wakiume na wamejenga na jamaa nyumba nzuri wanaishi maisha safi-binti amenawili sana anapendeza mno

Mimi sina mtoto sina mpenzi sina nyumba sina kiwanja ..naumia lakini kuna wakati naona ni sawa binti alikuwa sahihi na ni MUNGU tu alimuepusha na mimi kwa kweli ningemuharibia mtoto wa watu maisha yake..simchukii namuombea kila kheri..
poleeh jaman
 
Tena yupo na jamaa mmoja mnyonge sana kushinda Mimi,,

jamaa mwenyewe kachomekea suruali fulani hivi na shati limepauka mgongoni hatari,,,
kakaza sana mkanda wa suruali.,
Hata kiuno kikawa kidogo kama cha ngedere.


Hahahaa hapa tu
 
Nilikuwa napiga simu mfululizo,,
-- Hazipokelewi...
--SMS hazijibiwi,

Karibu siku tatu nzima.
Baada ya simu zangu kuzidi kusumbua mfululizo..
ikaja sms 1 tu toka kwake.

""Kwani mapenzi lazima""?

Aisee nilitetemeka sana,,halafu nikaitafakari sana ile kauli yake,

" ,,, Kwani mapenzi lazima?"
Mwishowe nikakubaliana na hali ya kuachwa,
Ikabaki kumbukumbu za love songs na matukio tuliyokuwa pamoja...

Nikisikia love songs tulizokuwa tunatumiana,,
kama kunogesha penzi,,
wakati ule wa mapenzi yetu matamu,,naumia sana.

Nikizisikia zile songs popote pale,,
nahisi roho yangu inataka kutengana na mwili..

Nakumbuka nyimbo moja ya bushoke jina siikumbuki ,
Ila amepiga na Dada Mmoja hivi,,

""Deka unavyodeka kama mtoto"

""Nitakubembeleza mm niwako ohoo.""

"Nitazidi kupa vitu moto moto"

"Mapenzi ni kupendana sio mchezo ohoo."

"Maumivu ya mapenzi yanauma sn,"

"Hata wivu sinao bali sina roho ya chuma.."

"Usiende mbali namiii,,""

""Usiende mbali namiiii ""

Mkuu hii nyimbo ilikuwa nikiisikia popote utanionea huruma,,
Kwa mawazo na hisia kali juu ya mapenzi wangu yule.

Moyo na roho yangu vinauma hatari,
Nilikuwa nateseka sana bila kujali mahali nilipo,,,mradi tu nisikie wimbo huo.

Saa ,siku,,week, ,miezi ilipita mwishowe nikasahau kabisa.,

Ilipita miezi kadhaa,, kuna siku nikakutana na yule ex wangu ,,
Yule aliyenifanya nikonde kwa mawazo.
Hata nikajiona sina faida ya kuishi hapa duniani bila yeye.
Tena yupo na jamaa mmoja mnyonge sana kushinda Mimi,,

jamaa mwenyewe kachomekea suruali fulani hivi na shati limepauka mgongoni hatari,,,
kakaza sana mkanda wa suruali.,
Hata kiuno kikawa kidogo kama cha ngedere..

Nilishangaa sana..
Nikajiuliza hivi mimi nilikuwa naumizwa na nini toka kwake huyu demu?
_Mbona huyu msichana wa kawaida sana?
-- Hata bure simtaki.,,
Duu!! hebu angalia wanaume anaotoka nao kwa sasa..!!
Nilishangazwa sn..

Aisee!! Kumbe kinachokuumiza ktk mapenzi ni hisia zako mwenyewe

Tupunguze kuwa na hisia Kali za mapenzi kwa tunaowapenda ,,
kuepusha maumivu makali wakati wa kuachwa...

Kumbuka

"Hata mapenzi pia yana date of issue...na date of expire...."

mark my words
Hayanaga formula.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza kwa Tuliowahi kupigwa vibuti, hebu tukumbushane changamoto tulizowahi kupitia baada ya kuona hapa sasa nimeachwa.

Mimi upande wangu nilipata tatizo la presha kushuka week mbili nimelazwa hospitali lakini pia mapigo ya moyo yalikuwa yanaenda kasi hatari.

Haya tuendelee

Once you master the art of ‘Loving with your heart and thinking with your brain’ you will always survive any breakup without destroying yourself.
 
Afu kuachwa ni kubaya sana,unakuja kuwa good mtosaji mbaya,unaishia kuumiza wasio na hatia....ila ndo hakuna namna
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom