Tuliovunjiwa nyumba Kimara tunaomba kulipwa fidia

Torero

Senior Member
Dec 22, 2017
122
138
Rais, kwa upole wako na huruma kwa Watanzania na upendo ulionao kwao naomba kwa heshima kubwa uwafikirie kuwalipa fidia wale wote walioathirika na bomoa bomoa ya majumba yao kwa ajili ya utanuzi WA barabara yaliyotokea enzi zile maeneo ya Kimara, Ubungo na kadhalika.

Wengi waliathirika na kuumia na wengi kufariki kutokana na kuwa nguvu zao ziilipotea bure. Sasa Rais kwa utendaji wako uliotuka tunaomba kwa upole kabisa uwakumbuke watu hao na waliofariki hata warithi wao wapo.

Kwa hakika Rais unapenda haki sana. Mwisho kabisa natoa shukran zangu kwako kwa kuleta maendeleo ya haraka kwa Watanzania wote bila ubaguzi
 
Shida ya watanzania kuto jua sheria, vamia kote ila sio hifadhi ya barabara, sijui wataka ukashtaki wapi wakuelewe, hiyo ni hasara kama hasara nyingine hukujua au mlijua kwa makusudi mkavamia hifadhi ya barabara ambayo ina sheria yake tokea miaka ya 1960's ndugu unapoteza muda
 
Mleta uzi usitutoe kwenye swala la bandari ebu tupambane na swala hili kwanza pakitulia tutakuja kwenye hilo lenu .wanzazibar washatuvuruga,angekuwa anapenda haki asingewapa waarabu bandari zote za tanganyika kwa waarabu na kuacha za kwao zanzibar. Au umetumwa kututoa kwenye reli!?
 
Rais, kwa upole wako na huruma kwa Watanzania na upendo ulionao kwao naomba kwa heshima kubwa uwafikirie kuwalipa fidia wale wote walioathirika na bomoa bomoa ya majumba yao kwa ajili ya utanuzi WA barabara yaliyotokea enzi zile maeneo ya Kimara, Ubungo na kadhalika.

Wengi waliathirika na kuumia na wengi kufariki kutokana na kuwa nguvu zao ziilipotea bure. Sasa Rais kwa utendaji wako uliotuka tunaomba kwa upole kabisa uwakumbuke watu hao na waliofariki hata warithi wao wapo.

Kwa hakika Rais unapenda haki sana. Mwisho kabisa natoa shukran zangu kwako kwa kuleta maendeleo ya haraka kwa Watanzania wote bila ubaguzi
Mheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania
Dr. Samia Suluhu Hasan.
Nakuamka kwa jina la Jamuhuri
Amani iwe kwako
Mimi na familia yangu ni muathirika .
Nimevunjiwa nyumba mbili pale Kibamba Makondeko. Moja ya nyumba hizo ikiwa ya kwangu na nyingine ni ya marehemu Baba yangu mzazi.
Mama yangu mzazi akiwa bado yu hai aliachiwa familia na Mzee wetu na Nyumba hii zikiwa kama urithi wetu na Nyumbani kwetuwan Familia. Mam yetu Mzazi akiwa ndiye kiungo kwa wana na wajukuu wa Familia hii.
Hivi sasa Mimi naishi nyumbani kwa mke wangu, na Mama yangu mzazi anatangatanga. Mara kwa Kaka mara kwangu ,mara kwa Mtoto wake wa kike.nk.

Kubwa zaidi Dada yangu ambaye ni Mjane alikuwa anishi na Mama, yeye kapata Stroke kwa tukio lile,
Na dada yangu mwingine ambaye naye alikuwa mjane vile vile akiwa anishi na Mama ,yeye Amekufa kwa mshtuko wa tukio lile.

Kwa muktadha huu, Kama Raisi atatufikiria angalau kutupa kiwanja na Fidia japo mkia wa mbuzi ,ili tuweze kuiombea Baraka serikali yako. Yule mwenda Zake Tulimuapiza kwa matendo yale, lakini Mungu alishapitisha Maamuzi kwake, sasa Umebaki wewe , Je Utajikomboa na Maapizo yale au utaensdeleza sera zile zile ? kwa vile na wewe ulikuwemo kwenye Utawala ule.!

Nakuomba , na nakunasihi Usikubali kurithi Laana ya Mtangulizi wako,
Jikombowe angalau kwa maneno mazuri na Fidia kwa waathirika. Najua na natarajia kwa usikivu wako kwa raia na juhudi unazozifanya kurekebisha yale yaliyoharibika, Unaweza kufanya kitu kwa waathirika wote wa tukio lile.
Heri kwako na kwa serikali yako. Utapata Baraka za wengi ,kama ulivyowafanyia wafanya biashara walioporwa fedha zao na wenyewe kutiwa ndani kwa tuhuma za uhujumu wa uchumi.

Natumai Ujumbe huu utakufikia Mheshimiwa Raisi Dr. Samia Suluhu Hasan
 
Mleta uzi usitutoe kwenye swala la bandari ebu tupambane na swala hili kwanza pakitulia tutakuja kwenye hilo lenu .wanzazibar washatuvuruga,angekuwa anapenda haki asingewapa waarabu bandari zote za tanganyika kwa waarabu na kuacha za kwao zanzibar. Au umetumwa kututoa kwenye reli!?
Wewe hufuatlii yanayojiri?
Taarifa uliyopewa kuhusu Kuuzwa Bandari si kweli.
Waziri ametowa Ufafanuzi na kusema ile kampuni ni kama kampunu nyingine zilizo tangullia kuendesha Bandari yetu. TICS ilikuwa kampuni ya nje ambayo ilikuwa ikiendesha bandari kwa miaka 20 sasa. na mara baada ya mkataba kuisha tukatadhmni ufanisi na tukaiweka pembeni na kuchukuwa DP World.
Huu ni utaratibu wa kawaida Kutafuta muendeshaji mwenye uwezo wa kuongeza ufanisi wa Bandari.

Utaratibu huu uko nchi nyingi duniani, sisi si wa Mwanzo.
 
Fuateni sheria msijenge barabarani

Kitu kingine mtu msikivu anaweza kuuza nchi?
Kama suala la uvunjaji halikuhusu bora unyamaze.
Sisi ndio waathirika. Tulihamia pale Mwaka 1972 kwa mwito wa serikali za vijiji kututakaktuhamia karibuna Barabara ili kuwa karibu na huduma za jamii. Sisi tuliitika na kupimiwa eneo la kuishi na serikali ya kijiji.
Miaka hiyo Ardhi ilipimwa mwisho magomeni
 
Sheria ni msumeno

Kwasasa tupo kwenye jambo kubwa la kuidai nchi yetu isiuzwe kwa waarabu na hawa viongozi waliokalia kitu

Kama suala la uvunjaji halikuhusu bora unyamaze.
Sisi ndio waathirika. Tulihamia pale Mwaka 1972 kwa mwito wa serikali za vijiji kututakaktuhamia karibuna Barabara ili kuwa karibu na huduma za jamii. Sisi tuliitika na kupimiwa eneo la kuishi na serikali ya kijiji.
Miaka hiyo Ardhi ilipimwa mwisho magomeni
 
Vita iliyopo mbele ya Watanganyika kwa sasa ni kuikomboa bandari kwanza, haya mengine yote yasubiri Kwanza.
Umeaminishwa uwongo na watu wanaotumiwana Kenya ili kuzorotesha Maendeleo chanya ya Tanzania.
Tumia akili kubaini Whats behind this move.

Magufuli alishawishiwa na Odinga kuzuia Ujenzi wa Bandari ya bagamoyo na kaingia Kingi, Kumbe mwenzake Kenyata alikuwa anjenga Bandari kama Hiyo kule Lamu ili kuipa kenya uwezo wa kupitisha mizgo kwa wingi zaidi ya Uganda, Burundi na Rwanda, South sudan na Central Afrika.

Usipojua Ugaidi wa Kiuchumi ,utadhani kla kitu ni siasa.
Hawa Akina mbarawa, ni vichwa vimeona Mbali
 
Attachments

  • WAZIRI_PROF.MBARAWA_AWATOA_HOFU_WATANZANIA.(360p).mp4
    11.7 MB
Back
Top Bottom