Tuliosoma Lugalo Sec Mpooo!!!!!!

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,235
4,949
Kwa wale tuliopitia Lugalo sec Iringa Tunamkumbuka mwalimu mmoja anaitwa mwalimu Materu alikua mwalimu wa Kilimo. Watu walikua wakimtajia majina ya uongo walipokutwa na makosa mfano wengine walidiriki hadi kutaja majina ya wachezaji wa Yanga Full list na akaja kuisoma Assembel. kama unakumbuka mengi unaweza kuongeza kuchangia
 
mie nakumbuka agriculture yake: castrate pigs! kwikiiii, matuta ya nyanya basi du
kutoroka na kwenda kula zambarawe za mama Kayugwa na kujificha mapango ya mlima Lugalo jamani! Nyali kabla ya msosi time wakati wa vipindi vya Agro.
mama Lambo(RIP?) na list ya watoro assembly - wapo hapo hapo lakini hawaoni!!!!!!
 
Hehehe Kabila naona mzee mara wana MOTCO sasa Lugalo si mchezo.
 
Hehehe Kabila naona mzee mara wana MOTCO sasa Lugalo si mchezo.
Unajua miaka ya Nyuma mfanyakazi alikuwa hakai miaka zaidi ya mitatu sehemu moja na ukipandishwa cheo tu ni pamoja na kuhama, hivyo usishangae watu chekechea tumesoma Dar, primary Mwanza, Sec Iringa, high sec Singida umezaliwa Mtwara. Ktk family ya watoto 7 kila mtoto na mkoa wake. Hii ilikuwa ni integration tactics ya Mwl Nyerere ndo maana kulikuwa hamna ukabila wala ufisadi
 
Oooh no, sikujua! RIP mwalimu Materu! Yule mwanae Rose Materu nae sijui yuko wapi. Hee nakumbukia enzi zile za kina mama Mwakasonda/Chigulu, Mwaisaka, Kibasa, Mzee Chikukula-RIP, mwalimu Mangula, Msasimela, Tweve nk nk! Ile shule ilikuwa nzuri sana, cjui sikuhizi! Hee mambo ya bustanini na mwalimu Materu ilikuwa si mchezo. Lile bonde lilikuwa linapendeza.
 
Si mchezo, mmenikumbusha mbali sana kwani nilikuwa mmoja kati ya watu waliosumbuana sana na Mwl. Materu (RIP) hasa katika vipindi vya kwenda shamba (self reliance). Mbali ya majina ya wachezaji wa zamani pia tulitumia majina ya wanamuziki wa zamani hasa wa nje. Mbali na hao mliowataja nawakumbuka pia Mwl Kisonga, Nade, Rubologa (mzee wa fegi), Mtavangu nk. Kipindi hicho ugomvi mkubwa na walimu ulikuwa kwenda shamba na kuvaa suruali kubwa (baggy).
 
jamani mnanikumbusha mbali, Chigo mnamkumbuka na maths zake, mzee mwenyewe lulandala na mikwara kibao, mzee Moses wa jikono siku za wali utamkoma,vile vile wagalatia na physics. Mnamkumbuka ng,ombe kipofu aliyenunuliwa na materu alikuwa anaitwa pundi. kada wa chama vile vile na Luwawilo
 
SIJASOMA LUGALO ILA NIMEKAA IRINGA...NAKUMBUKA LUGALO MLIKUWA MNAINGIA WENGINE ASUBUHI NA WENGINE MCHANA...MANISPAA NZIMA YA IRINGA ILIKUWA NA SHULE MOJA TU YA SERIKALI....BAADAYE IKAJA MAWELEWELE THEN NA NYINGINEZO...WANAFUNZI WALIKUWA WANATOKA IPOGOLO KWA MIGUU WANAPITA SHORTCUT YA KITANZINI HADI LUGALO...WENGINE MWANGATA, MKIMBIZI, KIHESA KILOLO N.K
 
Back
Top Bottom