Tuliombee Taifa na Tumuombee Rais wetu

Tuliombee Taifa na Tumuombee Rais wetu

Ms Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2020
Posts
2,466
Reaction score
4,967
Ndugu Watanzania wenzangu, wapenda amani wenzangu. Nakuja mbele zenu jioni hii naomba wote kwa umoja wetu tuliombee Taifa letu.

Tuwaombee viongozi wetu, Tuombee familia zetu kwa ujumla lakini pia tumuombee Rais wetu Mhe. John Pombe Magufuli.

Nimeangalia picha za leo za Mheshimiwa ni kama mtu alieumia sana. Tumuombee apate Hekima na Busara🙏🏽 Tutafika.

Picha za Rais wangu zimenifundisha kitu kikubwa sana. Uchungu huwezi kuuficha kila siku ipo siku utakushinda.

Tuache mengine yote, tujikinge, tujilinde na tulinde taifa letu. Kila mmoja wetu anaumia.

1.jpg
2.jpg
3.jpg
4.jpg
 
Tusome mistari ya vitabu vitakatifu labda kila mtu akizungumza na Mungu wake atatusikia. Mwenye mstari wowote wa kitabu cha dini chenye kufariji. Tuandikie. Mimi naanza na Isaya 60. Yeremia 29:11
 
“Mwamini Mungu, lakini mfunge vizuri Ngamia wako”-Mtume Muhammad SAW.

Mungu huwa halipi maombi bali hulipa jitihada!Kupiga maombi ya nguvu wakati hakuna mipango pamoja na hatua madhubuti za kupambana na Corona ni kumkejeli Mungu.Ukimkejeli Mungu tarajia mapigo saba ya ghadhabu ya Mungu.
 
Hiyo picha ya chini mkulu anatia huruma!
 
Hiyo picha ya chini mkulu anatia huruma!
Yaani nimeiangalia hadi nimejiskia huruma na uchungu maana anajiona kama anapoteza watu wake wa karibu na watanzania. Mungu atampa hekima katika hili
 
Yaani ha act kama presdaa kabisa. Hii ishu tuiache ameamua atayepona sawa atakayetembea kwa heri. Makosa ya CCM 2015
 
Unamjua mwanasiasa? Utaumia sana!
 
Usitumie wingi tafadhali sema 'utamuombea wewe' nakutakia maombezi mema
Tupo wengi sana tutakaomuombea! Usijali, najua nilicho andika! Naamu hata sasa tutaendelea kumuombea rais wetu mpendwa Mh Dr JPM na serikali zetu zote! Mungu azidi ibariki Tanzania! Amen!
 
Sura inaonyesha huzuni masikitiko ila ndani yake kuna HASIRA kali. Au ndugu zangu mnaonaje?
 
Vitu vingine havihitzji elimu kuuubwaaa kuvielewa! Sasa wewe ulitaka hapo aoneshe furaha na wakati anajua kuna makamera yanamchukua............ukiwa kiongozi wakati mwengine unatakiwa uwe muigizaji/msanii ili kuteka mioyo ya watu kama wewe.
 
Niko tayari kuliombea Taifa langu ila sipo tayari kumuombeo huyo Rais aliye nidhulumu stahiki zangu kama Mfanyakazi kwa mwaka wa sita huu sasa.

Huyo nitamuombea njaa siku zote za maisha yake hapa duniani.
 
Hiyo picha ya chini mkulu anatia huruma!
Na alipo wasababishia vifo wale wafanyakazi alio watumbua kwa kuwaonea, uso na sura yake pia ilitia huruma hivyo hivyo?

Au ni kwa sababu safari hii na yeye amegongwa na kirungu kwenye ugoko?
 
Hawa watu niwakuharibu mda et unawaombea nikuombee ww na si hao maana mwana kulitafuta mwana kulipata sitasahau juz tu chato anadai ugonjwa haupo sasa unampa taarifa kwamba upo. Mungu hadhihakiwi
 
Mungu wangu. RIP my president. I prayed for you. Naomba Mwenyezi Mungu akupokee huko ulipo. Amen🙏🏽
 
Back
Top Bottom