Tulioingia kwenye kilimo tukaangukia pua tukutane hapa

ZINGINALI wenyewe wanapaita.
 
Mimi nililima mpunga heka kumi ukakubali kweli kweli shamba lilikua langu bwana bwana kukaa hivi napigiwa simu wasukuma wameingiza ng'ombe usiku wamekula shamba lote aisee nilidata. Alafu washenzi wale wamehonga polisi ukienda kushtaki unapigwa danadana tu nilitamani nikapige risasi ng'ombe wote. Morogoro iyo
 
Duh aisee pole sana hayo maumivu yake kama nayaona vile.
 
Faida yote itaishia kulipa hilo Fuso, maana utakua unazunguka nalo kutwa.
 
Hiki ndo kilimo cha online, kinashawishi kinoma.
 
Mi niliingia ktk kilimo kwa partnership na ndugu zng wa huko bush ili km ikibuma basi maumivu yawe ½!

Msimu wa kwanza tulilima cabbage kwa kumwagilia! Niliwatumia ndugu zangu wa huko shamba kama nguvu kazi! Mimi nikatoa fund kwa ajili ya pembejeo!Cabbage ikatupiga hatari! Ilipigwa na ugonjwa, ikazaa chini ya Makadirio! Kidogo iliyopatikana tuliuza pale pale Kijijini!

Changamoto!
1. Mtu tuliemuamini km mtaalamu wa cabbage hakua na utaalamu husika na hivo alitupeleka chaka ktk maeneo km mbolea na sumu za wadudu waharibifu!

2. Tulilima kwa kutumia maji ya mto, kutokana na wingi wa wakulima, maji haya yalikuwa na zamu lini na lini wamwagilie akina nani. Ilifika wakati ikifika zamu yk let's say Juma5, mto hauna Maji!

Suluhisho!
Tumechimba kisima shambani. Pump tunayo!

Msimu huu tumelima MAHINDI Gobo gobo! Kila kitu kimeenda sawa! Yamezaa vizuri sana!

Hofu:
Tuna hofu na bei ya sokoni ya MAHINDI ya kuchoma!

Plan B:
Km MAHINDI ya Gobo gobo hayatakuwa na bei nzuri, tutayaacha yakauke ili tuvune MAHINDI ya Ugali! Kwa sasa sokoni bei ya ipo vizuri. Kijijini kwa sasa debe ni 20k!
 
Safi mkuu hapo ujipange namna ya kuhifadhi gobo isishambuliwe na wadudu au kuoza shambani ktk kipindi cha mvua unaposubiri ikauke
 
Kunaitwa NDUNGU mkuu unaingilia hapa mombo nimefika kote kule hadi gonja ila nimeuliza nimeambiwa ule mchele sio mtam kama wa kyela na ifakara ni mbegu za Kijapan.
We lima uza mbona watu wanatoboa tu huko Same.
 
Mimi nilishapigwa na kilimo kwasasa sina ham nacho kabisa,ninachokifanya nachukua mazao kwa mkulima then nayaweka store bei ikipanda nauza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…