Tulioharakia kuoa tukutane hapa

Tulioharakia kuoa tukutane hapa

Tit4tat

Member
Joined
May 31, 2022
Posts
58
Reaction score
171
Hello wanaJF

Mimi ni miongonI mwa wanaume waliooa wakiwa na umri mdogo.

Nikiwa na miaka 22 nilianzisha uhusiano na mwanamke X tulipendana saaana, mkwe (mama) alipogundua nina mahusiano na mwanae akaanza nichukia na kunisemea maneno makali.

Kadiri siku zilivyoenda uhusiano ulizidi kunawiri, mpenzi wangu akaanza kulala kwangu siku mojamoja na hatimaye wiki.

Wajomba wa mwanamke wakanifata wakaniambia nimuoe ndugu yao na kama sipo tayari nimuache binti yao.

Lakini mkwe alikuwa hanipendi kwa sababu ya umaskini, kiukwel sikuwa na kazi inayoeleweka zaidi tu ya kuishi kwa kubahatisha.

Mapenzi yana nguvu, nilikubali shauri la wajomba wa mke nikaamua nioe nikiwa na miaka 23 tu.

Kiukweli maisha yalikuwa magumu ila tulionekana na furaha sana haswa mke wangu kwani alizidi nawiri na kunenepa.

Nikaanza kujitolea kufundisha shule X nikawa napata kifuta jasho, punde Serikali ya Magu ikatangaza ajira kwakuwa nilisoma mbali na mkoa wetu nikamshauri mke tuuze simu yake smartphone nipate nauli ya kufata cheti chuoni.

Zoezi likakamilika nikafuata cheti nikaapply lakini nikatemwa sikubahatika kuchaguliwa.

Punde mke akashika ujauzito, nilianza kupata mawazo kwani sikuwa na kazi ya uhakika, niliwaza wapi nitapata pesa ya kuhudumia mtoto pindi atakapozaliwa au hata gharama za hospitali kwa lolote litakalotokea liwe dogo au kubwa.

Mungu mkubwa, nikabahatika kupata kazi English Medium ambapo nipo hadi sasa na umri wangu miaka 25 tu..

Kuna wakati najiuliza kwanini nilioa mapema? Lakini pia nawaza je bila kumuoa huyu mwanamke hela ya kufata cheti chuoni ningeipata wapi? Kwani hiko cheti ndio kimetusaidia nipate kazi hapa nilipo.

Nimeamini ndoa hufungwa mbinguni pia ukioa ridhiki huongezwa, maana maisha niliokuwa naishi wakati sijaoa yalikuwa magumu sana kuliko sasa hivi.

Bado sijafika ila nilipotoka na nilipo tofauti ingawa TAMISEMI wamenitema tena kwenye mkeka wa wiki iliyopita.
 
Naona ulioa mapema kwasababu ya ugeni wako penzini, ila kama ingetokea uachane na huyo mkeo kabla ya kuoana nae basi naamini ungeendelea kuwabadilisha tu.
Mmh ila nimefanya vurugu sana chuo kubadili wanawake, kwa ugeni upi labda au wa penzi jipya?
 
Mdogo wangu shukuru Mungu kwa hatua uliyofikia. Binafsi story yako inafanana ukitoa swala la kuchukiwa na ma mkwe ila leo baada ya miaka 8 ya ndoa najuta kwanini nilimuoa, maisha yangu yamerudi nyuma style ya 5g.

Somo: Mwanamke asikufanye u relax maana kuna siku na saa utashangaa maajabu yake, kikubwa weka mguu pande mguu sawa usijepotea kwenye ramani kikibuma.
 
Back
Top Bottom