Tulio wahi kunusulika katika ajali za vyombo vya moto tushee hapa na wenzetu

da irritant boy

JF-Expert Member
Oct 17, 2013
402
436
Lengo kubwa la uzi ni kutaka kutoa experience ya matukio ya kunusulika ajali na yamkini kutoa tahadhari kwa wengine ambao hawajawah kupitia visa hivo.

Binafsi nimepitia visa vingi vya kupona ajali za vyombo vya moto vingine nikiwa mm ndo dereva na vingine nikiwa kama abiria lakini siwezi simulia vyote bali ntachagua vile ambavyo vilitengeneza mstari mdogo sana uliokuwa ukitenganisha kifo na uhai. Hali ya kupitia matukio haya haswa yale ambayo yananihusisha mimi kama dereva yamkini yamechangiwa na kujua kutumia vyombo vya moto mapema sana chini ya umri stahiki.

Nimefundishwa kuendesha piki piki ilikuwa aina ya honda 110(Almaarufu kama wanteni) nyuma ina kitako kikuuubwa na haina clutch mwaka 1999 na mzee wangu nikiwa bado mdogo mno kiumri na gari nimefundishwa mwaka 2006 ilikuwa landcruiser mkonga 1hz.

Bhasi bila kupoteza muda moja kwa moja nirukie kwenye matukio yenyewe yaliyotaka kuchomoa uhai wangu lakini haikuwa imefika siku yangu

Kisa cha kwanza nikiwa kama abiria wa kawaida.

Ilikuwa ni Mwaka 2019 mwezi wa kumi, Safari yangu hii ilikuwa safar ndefu kuliko zote nilizowahi kusafiri kwani safar ilikuwa ni kuanzia Dar kwenda kigoma kupitia Mbeya na Sumbawanga. Safar ilikuwa nzuri wakati wa kwenda nikipanda Mbeya Express kutokea Dar mpaka Sumbawanga kupitia Mbeya mida ya saa 2 usiku na kufika Sumbawanga mida ya saa 6 usiku. unaweza shangaa kwann niliamua kuzunguka kupitia mbali wakati ningeweza kupanda basi za kupitia tabora mpaka kigoma, Nilifanya hivo kwan lengo kuu la safar ilikuwa ni kuhudhuria harusi ya rafiki yangu aliyekuwa akiishi kigoma na Sumbawanga kulikuwa na rafiki zangu ambao niliona ni vema nikiwapitia kwa ajili ya kampani. Sasa tuendelee Baada ya kufika sumbawanga nilipokelewa na washikaji zangu na saa 12 asubuhi safar ya kueleka kigoma kupitia mpanda ikaanza hapo tukipanda basi la saratoga.

Tufupishe stori zaidi Safar ya kwenda ilikuwa salama salmini ila wakati wa kurud nilipita ruti ile ile ya kwenda ila safar hii nilipo fika mbeya niliona ni vema nipite kumsalimia kaka angu aishie hapo nikae siku hata mbili then niendelee na safar. Siku ya kuondoka Mbeya ikawadia na hii ndo ilikuwa siku mbaya ya safari . Niliamka na kuaga kisha kuchukua boda ambae alipangwa na kaka kuhusu safar ile ya asubuhi na mapema, Mkosi unaanza wakat naondoka pale kwa kaka mitaa ile ilikuwa inaitwa Kabwe sasa ukiwa unaondoka kama unakatisha sehem ilikuwa airport ya zamani Ya mbeya pale tulikutana na kundi kubwa la mbwa na kutokana boda alikuwa mwendo kidogo ikawa ngumu kusimama japo alitaka kujaribu kusimama nikamsihi asipunguze mwendo na akaze mikono Tulikatisha huku wale mbwa wakirukia pikipiki dereva hakuguswa ila mm mbwa alibahatika kung'ata koti langu na kuning'inia kwa sekude kadhaa mpaka likachanika. Tukapita hapo ila sasa ikawa tumechukua njia ya mzunguko kwan wale mbwa wali tupotezea mwelekeo .tunaingia stend pale malengo yangu ilikuwa ni kupanda New force ila tayar ilikuwa imejaa muda nafika so nikaishia kupanda Rungwe Express na nafasi ilikuwa imebakia moja tuu.

Safari ilianza vizur na mwendo ulikuwa sio wa kujutia, Ila mambo yalibadilika baada ya kutoka Comfort Hotel pale kitonga, Dereva alianza kuendesha kana kwamba katumiwa meseji na mchepuko kwamba akichelewa hatamkuta,
Abiria tulikuwa kimya japo watu walianza kuonekana wana hofu kubwa mioyoni na moja ya dalili ya kwamba abilia wanahofu utaona tuu wanaanza kutaka kuangalia mbele kuna nn na wanaacha shughuli zao haswa wakat wa kuovertake, Tuyaache hayo sasa tuendelee

Baada ya kutoka comfort mbele mbele kuna kona moja sijui inaitwaje Ebhana dereva alikuwa akijaribu kuovertake gari karibia 6 zilizokuwa zimefatana na bila kuchukua tahadhar maana mbele alikuwa hajui ni kitu gani kinakuja, Hamad kuja kutahamaki lori la mbao hili hapa nalo limeiva balaa, watu wa kushoto hawawez kusimama kutoa fea na hawawez kubana kushoto kwa sababu kuna korongo, Mimi nilikuwa nimetoa kichwa koridoni kuangalia mbele kuna nn kwani abiria walianza kupiga kelele Ile lori ya mbao Dereva hakuyumba kushoto wa kulia ila sisi dereva wetu sasa alianza kuangaika na kupiga honi nyingi lakini haikusaidia Maamuzi aliyoyachukua hata ningekuwa ni mimi ningeyachukua hayo hayo.

Kulikuwa na ngema kubwa upande wa kulia ambayo huwezi kusema utaipanda lakini yule dereva aliifata ile ngema kwa kasi na kuigonga kwa upande wake, ..........

Sikumbuki kitu kingine kilichoendelea Bali nilikuja kupata fahamu naning'inia kwenye mkanda damu ikiwa inanitoka na maumivu makali,Ndani kulikuwa na vumbi kubwa sana likiambatana na vilio vya watu waliokuwa wakiugulia maumivu Sikuwa na nguvu ya kujinasua kwenye mkanda na mm nilikuwa siti ya kulia ile ya koridoni na gari ilikuwa imelalia ubavu wa kushoto, Nilijaribu kutoa sauti ya kuomba msaada lakini sauti ilikuwa haitoki Baada ya dakika kadhaa watu walikuja kutoa msaada na kunitoa pale kwenye siti kunilaza nje ya gari ambako nilijiona vioo kadhaa vikiwa vimeniingia mwili maeneo ya shingoni na begani lakini havikuwa vimeingia ndani sana kiuno kilikuwa kinauma sana mpaka nkahisi nimevunjika. Kimbembe simu yangu ilipotea kwenye lile sakata Namba ya kaka nilikuwa sijaishika bali ya mama, Niliomba nipewe simu ila netwek ilikuwa changamoto.... Tufupishe zaid ili niende kisa cha pili ila ile siku sijaisahau mpaka leo...

kumbuka kukalili namna kadhaa za msingi kichwani mwako

Kumbuka kufunga mkanda uwapo safarini , kwani unaweza kukupunguzia madhara kwa kiasi kadhaa Mfano mm pale nisingekuwa na mkanda lazima ningerushwa rushwa sana na kujibamiza sanajapo nao unaweza kukuweka pia kwenye hatar mfano ya moto sio rahisi kujitoa kwenye mkanda

Kingine kwenye ajali sio wote wanauwawa na ajali wengine wanauwawa na mizigo mfano watu wengine mabegi magumu utadhan wamebeba mawe au vyumba, sasa fikiria umejibamiza weeh afu na mizigo inakuja kukukandamiza

La mwisho tuache kiherehere, usijaribu kutaka kuruka katika ajali kama haujafunga mkanda karibu kujishikiria kwenye siti maana ile siku walifariki raia wawili ambapo mmoja wao alilaliwa na gari akijaribu kujichomoa dirishan

La mwisho tumkumbuke mola wetu mda wowote kwani maisha haya kifo na uhai vinatenganishwa na ufito mwembamba mno. Tusijifu kwa kupona bali tumshukuru mungu kwa kutupa nafasi ya pili

️Mimi sio mwandishi wala mtunzi so naomba mvumilie mwandiko wangu wa hovyo na mipangilio mibaya ya lugha,

NB: visa vingine ntaendelea navyo chini kwenye comment
 
Pole sana
 
Tarehe 16-7-2022 sitasahau hii siku,nipo na mshikaji wangu tunatoka Handeni to Dodoma,nimekaa kushoto Jamaa anaendesha.Tumevuka njia panda ya chamwino ikulu dah mara coster hii hapa tumegongana uso kwa uso.Mungu aliniokoa nikatoka ingawa hadi Sasa Nina maumivu ya viungo.Mshiksji wangu alifariki tukiwa kwenye ambulance.RIP ma nigga
 
Back
Top Bottom