Tulio safarini leo, tusalimiane hapa 😇!

Tulio safarini leo, tusalimiane hapa 😇!

Binti wa zamani

Platinum Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
15,079
Reaction score
37,010
Uzuri hatujuani ila wana JF kwenye hizi treni za asubuhi tuko wengi sana 🤣

Mtu wa pembeni yangu nilipokaa mkaka nimeona tunaperuzi wote JF, siti ya mbele yangu mdada naye anaperuzi JF na anasoma mada za siasa sijui ni wewe ShesRise_1 au asije akawa Lamomy, hapa nawaza tu tungekua tunajuana sijui tungesalimiana au tungekaushiana tu.

IMG_5568.jpeg

Anyway wasafiri wote tulio safarini leo, piteni hapa tuchangamshane safarini.
  1. Unasafiri kutokea wapi?
  2. Uko peke yako na umeshaanza kumsemesha huyo stranger uliyekaa naye karibu?
  3. Unatumia chombo gani cha usafiri?
  4. Kwa wakaka, kwanini mnapenda sana kujitanua miguu yenu mkiwa mmekaa, na hamjali hata kama mnabana wenzenu wa pembeni?

Asubuhi njema!
 
Mimi nilikua naperuzi jf nikiwa kwenye panton, ikatokea nikageuka nyuma nikamuona mzee mmoja shingo ipo juujuu kuchungulia nahisi alikua na hamu nijiroge nifungue profile yangu ili ajue mimi ni nani.

Nikaishia kumpa tabasamu😊
 
umenikumbusha miezi miwili imepita nipo mpakani mwa iringa na moro darajan ruaha panamadalali wa vitungu akaja dada moja hivi mlanguaji vitunguu

nikaona huyo kachukua simu pochiyake nikapiga jicho nikaona anafungua JF app nilicheka sana na humu namfahamu sijawahi kumsanua nikajiuliza niombe nambayake

nafsi ikasema fanya kilichokuleta mpakani hapa gari zilikuwa zinakaguliwa balaa
 
Ni shida tu zinanifanya nionekane mzee ila bado age haijasonga kiivo, kumbe yule ni wewe.
 
umenikumbusha miezi miwili imepita nipo mpakani mwa iringa na moro darajan ruaha panamadalali wa vitungu akaja dada moja hivi mlanguaji vitunguu

nikaona huyo kachukua simu pochiyake nikapiga jicho nikaona anafungua JF app nilicheka sana na humu namfahamu sijawahi kumsanua nikajiuliza niombe nambayake

nafsi ikasema fanya kilichokuleta mpakani hapa gari zilikuwa zinakaguliwa balaa
vipi ni mrembo au mrembo ukilewa pombe ikiisha una jilaumu
 
Back
Top Bottom