Tulio na bibi/babu wenye vituko na vibwanga tukutane hapa

Mimi babu langu alikuwa na nyumba zake mtoni mtongani sasa likizo huwa namtmbeleaga
Kuna siku nilipomtembelea nilikuta anaugomvi na mpangaji wake nilipofika tu akanambia nakupa mtihani ukiweza utakaa hapa likizo yote ukishindwa kweeenuuu, nikamwambia poa aknipa peni na karatasi akanambia anataka nataka umuandikie barua joseph ahame hivyo andika kama ninavyoongea usipunguze hata herufi moja akaanza na fyonyoo akambia andika ,akaja nyoooo' akaendelea JOSE JOSE SIKUTAKI KWANGU KAMA UMESIKIA HIKI KITUO CHA KULEA MASIKINI SIO KWANGU ,MTOTO HUNA HAYA KUTWA KUMUANGALIA MKE WANGU fyonyo la pili,,,,akaendelea HUKUNISAIDIA MCHANGA WALA KOKOTO (tusi) hukuleta mchanga wala nondo (tusi) kazi kuning'iniza...(tusi) akanigeukia na mimi ole wako lipungue neno nami nikala tusi laini akaongeaaaaa jioni nikawakuta baa wanakunywa pamoja eti mimi ndo mbaya nimetunga maneno nalazimisha urithi nilikuwa 4m4...dah yule mzee wa bandari alikuwa burudani saaana na alikuwa anapenda mnoooooo mis him much
Hahahaha ikawaje sasa
 
Bibi yangu mzaa mama (RIP)alikuwa anapenda wageni jamani yaani hata mtu anapita njiani hapo kwake ni njia akimsalimia tu ataanza story nae hadi mtu anasimama masaa anamsimulia habari hata hazimuhusu. Alikuwa napenda kuteta watu "gossiping"
Dingi alinifukuza home nilipata ujauzito usio na maelezo mother akanipeleka kwa bibi. Yaani nilitetwa mimi halafu nasikia kabisa watu wakimuuliza tu Bibi mbona huonekani wee anaanza "nitaonekana vipi nimeletewa mzigo mzito kweli umo ndani, mzigo hauna mahari wala posa."

Ila alikuwa sio mchoyo wa chakula na hodari wa kulisha ila hazingatii ratiba breakfast babu anapewa saa sita lunch jioni kwa sababu ya kupenda kuongea na kila mtu kazi zake zinasimama. Ana ng'ombe wake anakamua maziwa anauza. Siku mteja akikosa maziwa tu akute maziwa yameisha ataanza kuniteta

"Kuna mzigo upo ndani unakunywa maziwa kama maji ya kunywa kwa kweli nashindwa kuelewa karibu nitakosa hata pesa ya madawa sasa maziwa ya biashara yote anamaliza "

Basi nikisikia naishia kulia tu.

Kituko sasa nimejifungua mwanangu bibi yangu anamwambia mama yangu ee uje upesi mtoto analia mdomo wake una sauti kali sijui kabila gani huyu mtoto halafu halali usiku kwani huyu mwanao kazaa na nani asije kuwa kazaa na majambazi maana ndio hayana adabu yanakesha usiku kuiba" anaongea hivyo kwa kutumia simu yangu hatanii anamaanisha. Halafu tupo wote hapo hapo.

Akimaliza hapo anakuletea uji wa maana na supu yaani nilikuwa nalia lakini misosi unafurahi na roho yako

Bibi yetu alikuwa hapendi kabisa ukae na Babu (RIP) kuongea chochote akikukuta tu lazima atawavuruga anasema mwacheni aongee na TV yake huyo si anaongea na wanawake zake wazungu. Kisa babu alizaa na mzungu watoto wawili miaka hiyo huko Uingereza wakati keshamuoa bibi alienda kusoma.

Babu alitangulia kufa baada ya siku tano bibi akafa wote walikufa wamelala. Walale salama huko waliko.
Jamani sanduku la bibi lilikutwa na pesa nyingi sana. Alikuwa ana pesa haishiwi. Pesa yake ya maziwa inakaa kwenye sanduku pesa ya matumizi watoto zake walikuwa wanampelekea kila mwezi. Na ile pesa babu hagusi. Ya kwenye sanduku hakuna aliyekuwa anajua kuwa kuna mipesa ndani Bibi yangu namkumbuka sana kwa kuteta na masimango mchaga yule mwisho.
Na bibi yangu akija mgeni anaanza kumsimulia,,
Bibi mzaa mama ukimtambulisha mtu kosa,,kuna ndugu yangu alichumbiwa akaleta mchumba kwa bibi,walivyoondoka sasa,,bibi akaanza kusimulia lea anaolewa kamwanaume kabaya ,kana kipara,kafupii ahahhaha
 
yaani wazee wangu basi tuu,halafu babu yangu anapenda kuuliza SAA(muda)hata uwe umeenda Pluto hamjaonana miaka 20,ukiingiza tuu mguu ndani cha kwanza kukuuliza ni "hivi sasa ni SAA ngapi hapo" yani hana kummisi MTU wala nn hajui umerudi ukechooooka au vipi yy ni SAA tuu usipomjibu utamsikia " najua nawakera ila hamnipendi tuu" ..na ukimjibu labda SAA 6:30 mchana baada ya dk 2 anauliza tena....eeeh unatamani umkate vibao akalazwe muhimbili
Hahahahahah hiyo kali
Mim bibi hana simu,akiomba apigiwe mtu flan halaf mkawa busy,anaanza nije tu ninunue simu yangu tu akitaka kununuliwa hataki tena
 
bas bibi angu akija mjini kaz yake kuokota vitu vilivyotupwa ka makopo ya lotion viboks na nin anaweka chumba anacholala,na mkitupa ni ugomvi mkubwa na anarudi tena kuokota,cku ya kuondoka anachukua roba chafu anaviweka na ole wako ubadilishe roba sasa,siku moja tukachukua roba usiku tukalitupa asubuh sasa anapelekwa stand akauliza mzgo wake na akasema siondok ad nipewe mzigo wangu ikabidi tukamtafutie roba lenye vitu vyake
Mgemuuliza anaenda kuvifanyia nini
 
Hahahahahah hiyo kali
Mim bibi hana simu,akiomba apigiwe mtu flan halaf mkawa busy,anaanza nije tu ninunue simu yangu tu akitaka kununuliwa hataki tena
wanavituko sio vya nchi hii,mpaka nikawa najiuliza niwazee wangu tuu auu??!ila Uzi huu umenifanya nipate faraja mweh!!!
 
Mashikolo mageni mayooo
Dinazarde nimecheka had machozi jaman !dah eti ukiomba ng'ombe anasema miguu imevunjika !jamani nimecheka !i can imagine kwa bibi yako !Mungu ampe maisha marefu jaman muendelee kuenjoy !
mie sijaishi karibu na bibi zangu walikua hawajui kiswahili na mie sijui kisukuma bas nikawa napishana nao tu round about !rip bibi zangu
 
Rip dearest bibi yangu. Alikuwa na vituko sana alinipenda kuliko wajikuu wote wa ukoo mzima, walikuwa na uchoyo Fulani ila kwangu hakuna kitu ambacho sikula kwake.

Historia inaonesha hakuwai kulala na babu (rip) yaan wakati wa kupata mimba wazee walikuwa wanakuja wanamkamata, babu anafanya yake, mimba tiyari ndo mwisho, hadi mtoto mwingine.

Wakati nakua nilikuta kila MTU analala kivyake. Babu ndo alitangulia mbele za haki.

Vituko vyake sasa uzee kweli fainali,walikuwa ana uwezo wa kukimbizana na wajukuu baadae ya kuiba maembe anakukimbiza umbali wa km hata 300

Alinipenda balaa, alikuwa akipika kabla hajala atatoa ndizi moja tu, aweke kwenye sahani aje kwetu, atauliza luckyline yupo WAP mama alisema hayupo atanisubiri hapo chakula amekifunika kitambaa nikija ananipa nakupa peke yangu ndo ataondoka.

Alikuwa awezagi kula chakula kilicjopikwa na MTU yeyote labda mm. Alikuja kula chakula kilichopikwa na MTU mwingine baadae ya kuzeeka sana.

Alinipenda kupitiliza mpaka kijiji kizima kilijua.
Alipoona nguvu zinapungua akamjulisha kila MTU kuwa siku akifa mm sio wasimzike, wanisubiri nifike,

Kweli mwaka 2015 bibi aliumwa uzeee, kila siku alimwambia mama niende nyumbani bibi nguvu kwisha, Bahati mbaya ndo nilikuwa nimepata kazi sehemu nyingine hata mwezi, nilikosa ruhusa.

Siku moja nilikosa usingizi usiku asubuhi nikamwambia mkurugenzi naomba niende kumuona bibi kabla hajafa ilikuwa j4 mkurugenzi akasema jitahidi uende jmosi kabla ya jos j5 bibi kafariki, nililia sana

Mama alinambia, mpaka anakufa alikuwa anauliza Niko wapi, sijui alitaka kunambia nini?

Basi upendo wa bibi kwangu ulisababisha wajukuu wengine wasinipende, baada ya bibi kufa wakataka wazike kisa mm Niko mbali, kijijin hakuna mochwari, wajukuu wanakomalia wazike, wazee nao wakakomaa, wanisubiri bibi alisema.

Tangu naanza safari nililia kwenye basi nilishindwa kujizuia, nakumbuka upendo wa bibi, yaani zamani bibi akijua nakuja likizo alikaa barabarani na kusubiri Gari nikishuka alitamani anibebe, jamani bibi alinipenda.

Anyway nilipofika msibani nilikuta wapumbavu wajukuu kaka zangu Dada zangu midomo wameivuta hawaniongereshi, sikukuta maandalizi yoyote, namaanisha zile mbwembwe za wajukuu, maua/shada na nilijua hawatafanya, nilivyofika Mjini nikatengeneza yakutosha na nikatafuta waandaaji wa sehemu ya ibada.

Nilipofika nilipokelewa wazee waliopigania wasizike waliponiona walifurahi sana huku wengine wamenuna kuwa wananisubiri mm nani,simnajua mambo ya kijijini, nilipofika nilipata nguvu process zote zikaanza upya. Na bibi yangu akazikwa kama nilivyotaka mm.

Kweli mpaka sasa siamini kama bibi yangu siko nae tena ,nilimkuta kashakuwa wa baridi ndani ya jeneza macho hanioni tena nililia sana nikamuomba msamaha kwa kutofika mapema nilitamani nimbebe mgongoni ila haikuwezekana. Ila naamini alinisikia kuwa nimefika maana niliambiwa kuwa kabla sijafika mambo yalikuwa hayaendi walikuwa wakilazimisha wazike kabla sijafika hata jeneza liliwashinda. Nilipofika tu kila kitu kilikuwa chepesi

Apumzike kwa amani, alifariki akiwa 96-age.nampenda hata Leo.
 
Bibi yangu kila nikienda kumsalimia ilikuwa lzm nilale nae kitanda kimoja, naweza nikampa sababu kibao bhana bibie mm nimeshakuwa mtu mzima bhana acha nikale mwenyewe kwani ananielewa,ila yote hiyo ni kwasababu ndio alinilea toka nikiwa na nilikuwa nalala nae,kitu alichokuwa ananifurahisha zaidi ni imani yake kwa kanisa katoliki,kila siku yy ilikuwa ni kanisani hamna anaacha kwenda labda anaumwa sana,Ila ndio hivyo Mungu alimpenda zaid
RIP bibi
 
Alikua na maana gani kuchemsha jiwe kwenye chungu?
Hiko ni kipindi cha njaa ndio wazazi walikuwa wanafanya hivyo,wamama wanaweka mawe kwenye chungu mnayachochea moto kuanzia asubuh hadi jion wakati huo mzee anapambana huko mpate chakula
 
Rip dearest bibi yangu. Alikuwa na vituko sana alinipenda kuliko wajikuu wote wa ukoo mzima, walikuwa na uchoyo Fulani ila kwangu hakuna kitu ambacho sikula kwake.



Apumzike kwa amani, alifariki akiwa 96-age.nampenda hata Leo.


Pole sana. RIP bibi
 
Bibi yangu alikuwa akitupikia chakula inabidi tule tubakize kidogo, ukimaliza chote haamini kama umeshiba, akija kututembelea nyumbani akiona tunakula bila kusaza anaanza kumgombeza mama kuwa utaua watoto kwa njaa, mama kwa hasira anaamua kupika tena, halafu anashangaa hakuna mtoto anayekula maana mama alikuwa anajua kukadiria. Neno pekee la Kiswahili alilokuwa analijua ni UTASIBA? akimaanisha UMESHIBA? Alikuwa mkarimu mno, nimemmiss mno bibi yangu, R. I. P Bibi
 
Bibi yangu alikuwa akitupikia chakula inabidi tule tubakize kidogo, ukimaliza chote haamini kama umeshiba, akija kututembelea nyumbani akiona tunakula bila kusaza anaanza kumgombeza mama kuwa utaua watoto kwa njaa, mama kwa hasira anaamua kupika tena, halafu anashangaa hakuna mtoto anayekula maana mama alikuwa anajua kukadiria. Neno pekee la Kiswahili alilokuwa analijua ni UTASIBA? akimaanisha UMESHIBA? Alikuwa mkarimu mno, nimemmiss mno bibi yangu, R. I. P Bibi
 
Back
Top Bottom