Tulio lelewa na ndugu tukutane hapa

Tulio lelewa na ndugu tukutane hapa

BILGERT

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2015
Posts
6,532
Reaction score
11,028
Habari wakuu,katika kipindi tunacho elekea kumaliza mwaka kuna jambo kuu ambalo ninalitafakari saana,hivyo sina budi kumshukuru muumba kutokana na mema aliyo nitendea katika haya maisha.nitaelezea japo kwa ufupi.

Binafsi nilizaliwa katika familia ya kawaida saaana,nilivyo fikisha umri wa miaka miwili familia yangu ilisambaratika kabisa baada ya ugomvi mkali uliotokea kati ya baba na mama,kutokana na umri wangu kuwa mdogo sikuweza kutambua chanzo hasa cha ule ugomvi.

Ule ugomvi ulipelekea wazazi wangu kuachana,Mama aliweza kurudi kwao na huko kwao hakukaa saana,aliweza kuolewa na mwanaume mwingine ambaye ndo anaishi naye mpaka sasa na wamefanikiwa kupata watoto wengine.

Baba mzazi alijiingiza katika ulevi wa kupindukia,hivyo mimi ilibidi nilelewe na bibi mzaa baba mpaka nilipofikisha umri wa miaka 6,Ndipo shangazi yangu ambaye ni dada yake na baba yangu alikuwa akiishi mjini,alikuja kunichukua na ndipo nikaenda kuishi naye huko mjini.

Yeye ndiye aliye nilea na kunipatia mahitaji yote muhimu pia elimu kuanzia primary mpaka namaliza chuo,hatimaye 2015 nikapata Kazi serikalini. Kiukweli amenilea bila ubaguzi wowote ule.

Kila siku namuombea kwa mwenyezi MUNGU aweze kuishi umri mrefu,maana binafsi sina cha kumlipa kwa kweli.Naamin bila yeye nisingefika hapa nilipo hivi leo.yeye namchukulia kama baba na pia kama mama.

Habari ni ndefu mno wadau.ila naamin nimeeleweka japo kwa ufupi.
 
Mimi Baba yangu alifariki mwaka 1967 nikiwa na miaka 7 tukachukuliwa kulelewa na baba mkubwa nae 69 akafariki tukachukuliwa na mtoto wake ambae ni mkubwa aisee mpaka leo na uzee huu sina upendo na watoto wake na baadhi ya ndugu nawapenda watu wa pembeni walioshuhudia mateso manyanyaso yetu niliteseka sana ikanifanya kwa miaka saba tu nikasoma shule tatu tofauti nisiongee sana huwa naumia sana BINADAMU NI WABAYA SANA HUWA NI WAZURI TUKIWA TUMELALA MAKABURINI TU
 
Pole sana
 
daaah,pole saaana mkuu.najua unayo mengi moyoni
 
Mkuu licha ya kumpenda shangazi yako mkumbuke pia mama yako maana pengine hakupenda ndoa ivunjike. Wapende pia wadogo zako wa baba mwingine
 
Sina la kusema, Mungu amzidishie Baraka alonilea.
 
Mimi Baba yangu alifariki mwaka 1967 nikiwa na miaka 7 tukachukuliwa kulelewa na baba mkubwa nae 69 akafariki tukachukuliwa na mtoto wake ambae ni mkubwa aisee mpaka leo na uzee huu sina upendo na watoto wake na baadhi ya ndugu nawapenda watu wa pembeni walioshuhudia mateso manyanyaso yetu niliteseka sana ikanifanya kwa miaka saba tu nikasoma shule tatu tofauti nisiongee sana huwa naumia sana BINADAMU NI WABAYA SANA HUWA NI WAZURI TUKIWA TUMELALA MAKABURINI TU
Pole sana mkuu.
 
Nimelelewa na dada alikuwa mkali ila ananipenda balaa na hivi hana watoto mimi ndo kama mtoto wake. Watu wengine walikuwa hawajui uhusiano wetu wakawa wanamuita mama Khantwe. Alikuwa ananichunga hadi nikitaka kukwichikwichi nahisi ananiona then naimagine hilo sekeseke lake wee naahirisha kiroho safi [emoji23] [emoji23] [emoji23] ...wanaosema ukali hausaidii watoto kukua kwenye maadili nawaangalia tu mimi binafsi ule ukali ulinisaidia kuniweka kwenye mstari kile kipindi cha balehe
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] so unataka kusema ujafanya yale mavitu????
 
Nimelelewa na dada alikuwa mkali ila ananipenda balaa na hivi hana watoto mimi ndo kama mtoto wake. Watu wengine walikuwa hawajui uhusiano wetu wakawa wanamuita mama Khantwe. Alikuwa ananichunga hadi nikitaka kukwichikwichi nahisi ananiona then naimagine hilo sekeseke lake wee naahirisha kiroho safi [emoji23] [emoji23] [emoji23] ...wanaosema ukali hausaidii watoto kukua kwenye maadili nawaangalia tu mimi binafsi ule ukali ulinisaidia kuniweka kwenye mstari kile kipindi cha balehe

hahha mshukuru kwkweli
 
Mungu awabariki wote walioshiliki kwenye malezi yangu hadi nimekuwa hivi.

Awabariki wao na vizazi vyao
 
Nililelewa na aunt yangu alinilea vzur na kikubwa alisstza nisome who i am right now asilimia kubwa ni mchango wake! I love her with all my heart n soul!
 
Nimelelewa na dada alikuwa mkali ila ananipenda balaa na hivi hana watoto mimi ndo kama mtoto wake. Watu wengine walikuwa hawajui uhusiano wetu wakawa wanamuita mama Khantwe. Alikuwa ananichunga hadi nikitaka kukwichikwichi nahisi ananiona then naimagine hilo sekeseke lake wee naahirisha kiroho safi [emoji23] [emoji23] [emoji23] ...wanaosema ukali hausaidii watoto kukua kwenye maadili nawaangalia tu mimi binafsi ule ukali ulinisaidia kuniweka kwenye mstari kile kipindi cha balehe
Kabsa ukal ni muhim kwa watoto nlkuaga sipend shule afu ctak kuleta report ila kwa zile stick za aunt nlkua naleta kila term na ilfkia hatua nabadl matokeo ili fimbo zpungue but wapi zipo palepale tu ukipata below 40 zile stick hazkua za nch hii
 
Acha ninyamaze mie niliyelelewa na baba wakambo ctaki hata kukumbuka ilikuwa balaaa
 
Back
Top Bottom