Ahaha ! nimecheka saana leo mkuu wangu hilo shimo lilozungukwa na nzi inatosha kabisa kunipa picha... Tutaendelea kesho ngoja nipate daku kwanza .. duh umenipa usingizi leo..Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama asali, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amrbski hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?
Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.
Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.
Je unajua kuwa kuna watumishi wa serikali wenye mishahara mikubwa sana lakini utendaji wao umejaa rushwa tu?
Nafahamu, hilo la misahara ni moja tu!
Ni wafanyakazi wangapi wana mishahara mikubwa?
Si unajua Vodacom wana mishahara ya haja tu?
Kuna mengi zaidi ya hilo
Maelezo ya kina ameyatoa Mkandara #16: Njaa, Ujinga, Maradhi na katika haya matatu, ujinga ndio unaoweza kusababisha yote hayo na zaidi ya hayo. Juzi tulikuwa tunajadili hapa ilikuwaje Korea ya Kusini kuendelea ndani ya utawala wa kidikteta? Pamoja na mengine, S. Korea imeedelea kwa sababu ya kuweka elimu kuwa ni kipaumbele cha mwanzo. Hapa sitetei udikteta, lakini "kama hakuna budi" basi bora udikteta wa muda lakini nchi ikawa na lengo maalumu, kuliko demokrasia ya kulazimishwa daima bila malengo. Tanzania imepoteza malengo, achana na nyimbo ya MALENGO YA DUNIA YA MAENDELEO; hiyo ni ya kutembezea bakuli tu, tunapewa sumu katika katika kichupa kiliansikwa tiba.MAMMAMIA
..................hilo haswa ndilo jawabu, lakini je wazalendo hao tutawatoa wapi iwapo wote wameshaharibika? Kumbuka kuwa unahitaji kuondoa karibu mahakimu wote, polisi wote, wanajeshi wote, watumishi wa serikali karibu wote.
Sikuishi miaka hiyo lakini nimeelewa unacho maanisha... Naagalia driving forces zinazoijenga na kuifanya Tanzania iilivyo hivi leo. Tulikuwa na Chama kimoja Tukiite CCM ambacho kipo hadi leo na serekali yake ndiyo imeijenga hii nchi.Kwa watu walioshi miaka ya sitini na ile ya sabini wakati bado kuna siasa za Ujamaa na Kujitegemea, mtakubaliana nami kuwa mambo hayo hayakuwamo miongoni mwa jamii yetu. Yalianza kukua kidogo kidogo mwanzoni mwa miaka ya themanini baada ya vita, na yakaua kwa kasi sana kuanzia mwishoni mwa miaka hiyo ya themanini, ambapo miaka ya leo hii tumefikia mahali ambapo ni alarming sana.
Nina maswali mawili ya kujiuliza:
(a) Ni wapi tulipokosea hadi tukajenga element mbovu hizo katika maisha yetu?
Kichuguu,
Ndivyo Tulivyo inaambatana na ulemavu wa UTU kutokana na Umaskini, Ujinga na Maradhi..Hao wote walioendelea ukitazma kwa makini wamepigab hatua kubwa sana kuondoa kwanza maadui hao ktk jamii zao. Hata tukisema Kenya wao wamesoma kuliko sisi, sii maskini kama sisi na poengine naweza sema hata vifo ni vichache zaidi kwa sababu unapoondoa Ujinga na umaskini hata maradhi na vifo pia hupungua..
Sisi kwa kuacha vita yetu, tumeingia ktk Ubepari bila Mtaji isipookuwa Kiburi, kile kiburi cha maskini jeuri na ndi maana hata tunapoomba msaada husema huwezi kunipangia nitaufanyia nini, wewe kama unanipa nipe halafu mimi nitajua la kufanya kama vile msaada ni sadaka au Zaka. Na kwa ujinga ule ule hufikiria neno MSAADA ni lina maana unapewa bure na hudaiwi wala hauna riba.
Kwa Umaskini na Ujinga tulokuja nao ktk Ubepari tumejikuta sisi wenyewe ni virusi vya maendeleo yetu wenyewe. Hatuwezi kuwa na Ethics mkuu wangu haiwezekani. Umaksini wetu ndio adui wa maendeleo yetu wenyewe. hatukurogwa wala kurudishwa nyuma zaidi ya sisi wenyewe kushindwa kujipanga kuweka mfumo bora zaidi ktk kuhakikisha Umaskini, Ujinga na maradhi vinaangamizwa..
Na Unapokuwa na kilema hicho ustaarabu nao unatoweka.. Nimeshatoa mfano zamani ya kwamba Jaribu siku moja weka makundi mawili ya watu. Kundi la kwanza wapange mezani kila mtu na sahani yake ale kwa kisu na uma, halafu kundi la pili wamwagie sinia la biriani mkekani halafu uone tofauti ya jinsi watu hawa watakavyo behave ktk chakula.
Wa mkekani hawataweza kula na uma na kisu wala hata kijiko maana it's about speed, quantity na shibe..Wa mezani wakaweka ustaarabu fulani na pengine hata kuwacheka walioko mkekani, lakini hata yule mtu alokuwa mezani jana ukimweka mkekani kesho utamwona akigombania nyama na yule wa mkekani ukimweka mezani utamwona akibadilika.
Hivyo mimi na wewe mkuu wangu tumekuja huku mezani umebadilika na kuwa na ustaarabu fulani lakini tukikumwaga Bongo tu haitachukua miezi sita wewe mwenyewe utaanza kugombania biriani.. lazima utatia akili..
Uchumi wa nchi za kiafrika ni sawa kabisa na sinia la mkekani, hatukufanya maandalizi ya mageuzi ktk mfumo wa kiuchumi kwa kutazama kwanza WATU na MAZINGIRA tulokuwepo ila tuliiga tu Ubepari wa nchi za Ulaya.. Huweiz chukua watu wmaskini, wajinga na wenye matatizo makubwa ya kifaya ukawapachika mfumo wa Ulaya.. Sisi tulipigania Uhuru lakini tulichopewa ni Demokrasia hatua ambayo haikulingana na mazingira yetu..Hivyo kwetu sisi maskini hata hata kama tukiacha biriani tukawekewa vianzi vya mbatata (Fries) na kuku bado watagombania. Na yule ulomweka(msomi) Jikoni atajiona yeye ndio mwenye shughuli, mpishi na mgawaji chakula na bila shaka ataona ni haki yake kuacha chakula kingine pembeni abebe nyumbani kwake baada ya shughuli mbali kabisa na malipo alopewa.
Kwa Umaskini, Ujinga na maradhi, usitegemee kabisa kwamba kuna kujituma hapa. Sisi wote ni waaliwka tu ktk dunia hii ya demokrasia maana hatujui kilichopikwa. Zamani tulikuwa tukisisitiza zaidi Kilimo na kusema ndio uti wa mgongo, Tukipambana na Umaskini, Ujinga na maradhi lakini badala yake tukaletewa Demokrasia na ndio ikawa vita yetu kwa sababu Ulaya ndio wanachopigania na wachosisitiza. Sasa wewe nambie kwa Mtanzania maskini, mjinga na mwenye afya mbovu hii demokrasia itamsaidia nini zaidi?..Yet ukiwauliza watu wengi sasa hivi kila mtu atakwambia Demokrasia, demokrasia kaa vile UTU wa binadamu aumaendeleo ya Mtanzania yatathaminika kwa Demokrasia..
Kwa kumalizia tu ni kwamba sisi tupo ktk mfumo mbaya usolingana na WATU wala MAZINGIRA yetu..Tumeacha maadui wetu na kuvamia maadui wa nchi za magharibi na ndio maana hadi leo sisi bado ni watumwa wa kimfumo. Umaskini hautakwisha na wala Ujinga hautakwisha kkutokana na kwamba sisi tuna maradhi tofauti kabisa.. Tunaumwa Malaria wanatupa dawa za mafua kwa sababu tu mafua inaua watu wengi Ulaya nasi tumeweka vituo na karantini za matibabu ya mafua - Tutapona wapi?..
Kwanza lazima nikushukuru kwa kunielewa niloyaandika hapo nyuma na utata wa hali na maisha yetu kwa ujumla... Na kusema kweli sisi tuko ktk serious trouble economically na sidhani kama viongozi wanaelewa uzito wa janga hili.Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama asali, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amrbski hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?
Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.
Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.
Now this is a billion dollar question!Je Tanzania tuchukue hatua gani ili kurudi kwenye uchumi huo iwapo viongozi wetu walishasaini mikataba ya miaka 99 na makampuni ya nje?
Kusema kwlei binafsi yangu sina hope tena baada ya Dr.Slaa pengine sijui mipango ya Chadema lakini kutoka ndnai ya CCM sina hakika maana tayari najua kinachokuja..Wapo watu wanao amini kila kitu kina mwisho.. Well Afrika tulikoloniwa kwa zaidi ya miaka 500, are ready to wait that long?.Mkandara
Ukweli wa mambo ni kuwa kutokana na mfumo mbovu uliokwisha jengeka kwenye jamii yetu mabadiliko yanaweza kutokea kwa hatari pia. Iwapo tu raia kuandamana ikiwa na haki yao ya kikatiba wanapigwa risasi na kuuwawa tena mchana kweupe na vyombo ambavyo jukumu lake ni kulinda na kutunza usalama wa raia, unadhani kweli serikali inayolindwa na vyombo vya namna hiyo itakubali mabadiliko?
Unaonaje iwapo outsider huyo ndani ya serikali ndiye akitumika kuchochea mabadiliko hayo? (I am just wondering). Outsider huyo akipewa madaraka makubwa zaidi kama uwaziri mkuu, je unadhani ataendelea na moto huo huo siku zote, au akishasettle atasahahu na kurudi tulikotoka? Tumewahi kuwa na wabunge vocal sana kuishambulia serikali na "kuwatetea wananchi" lakini walipopwea uwaziri mdogo tu wakawa ndio wanaongoza kwa ufisiadi. Kwa tabia yetu watanzania huwa hatuna 'sustained effort,' tuna kitu kinajulikana "nguvu ya soda" tu, au nguvu ya upepo tu utapita.
Kichuguu,Mfumo unaojulicana kama "mixed economy" yaani mchanganyiko wa ujamaa na ubepari ndio mfumo uliozikomboa nchi nyingi sana duniani hasa huko Asia. Serikali inasimamia maswala ya elimu, huduma za afya, na kumilik biashara nyeti kwa taifa kama mali asili, nishati, na njia kuu za usafirishaji kama treni, usafiri wa anga huku ikiwahimiza raia wake (siyo raia wa nje) kuwekekaza katika biashara hizo. Wakati huo huo ikiwaachia watu binafsi wajifanyie biashara zao nyinginezo.
Kichuguu,
...Tatizo sio mfumo wa uchumi, bali ni kujiongopea na kukubali kuongopewa. Pale Mwl. Nyerere aliposema waTanzania ni wajamaa -na kuukumbatia u african socialism- alikuwa anamwongopea nani? Kila kitu alisema waTanzania wameamua. Je, kuna kura ya maoni ilipigwa?
...Hata sasa, utasikia watu wanasema ....."serikali yetu sikivu". Wanamwongopea nani? Hebu waulize walimu kuhusu hili.
...Tukiacha huu uongo, tutakuwa tumeanza kuelekea tunakotakiwa kwenda, kiuchumi and otherwise.
...I doubt this. Na utamaduni huu umeendelea toka kipindi kile. Kumbuka fikra za mwenyekiti zilikuwa "sahihi". I very much respect and admire Mwl. but that doesn't make me blind to the facts.Sera zote zilizotokea Tanzania miaka hiyo zilikuwa zinapitishwa na organs halali zilizokuwa zinawakilisha wananchi kwa mujibu wa katiba iliyokuwapo. Vikao hivyo vilikuwa vikifanyika kwa mujibu wa sheria za nchi zilizokuwapo wakati huo.
...Kuonyesha baadhi ya mambo yaliyotufikisha hapa tulipo si kulaumu bali kubaini upungufu na kujifunza. Mwl. atatumika kama rejea -katika mambo mbalimbali- siku zote za maisha ya Jamhuri hii. Na wanaomfanya scapegoat wamepotoka! Simply, we learn from mistakes, or we don't learn at all.Kulaumu maamuzi ya mwaka 1960 ni kujirudisha kwenye sifa hiyo hiyo niliyosema kuwa watanzania hatutaki kuchukua responsibility, kila wakati tunatafuta mtu mweingine wa kulaumu, na tunapomkosa, basi tunasingizia Mungu. Nyerere (RIP) amekuwa ni scapogat rahisi sana kwetu kutumia lakini kwa vile katanguliea mbele ya shria hatuwezi kubaki tukilia na Nyerere badala ya kutafuta namna ya kujiendeleza.
Hiyo doubt uliyo nayo kuhusu ukweli huo ndiyo inayoondoa uzito wa hoja yako. Angalia kuwa Azimio la Arusha lilipitishwa na kikao halali cha TANU wakati huo na kupitishwa kwa pamoja pale kwenye mkutano wa Arusha chini ya misingi iliyokuwapo kihalali. Baadaye ukafuatia Mwongozo wa TANU uliotoka mwaka 1971 pale Dar es Salaama na kupitishwa na kikao halali kilichokuwa kinatambuliwa kikatiba; kuna maamuzi mengine kama Siasa ni Kilimo, Mtu ni Afaya, Azimio la Musoma na mengineyo yaliyofuatia; yote yalikuwa halali katika mazingira yale. Hebu angalia swala hilo intellectually kama unaweza kuona uharamu wa maamuzi yale kisheria uuonyeshe....I doubt this. Na utamaduni huu umeendelea toka kipindi kile. Kumbuka fikra za mwenyekiti zilikuwa "sahihi". I very much respect and admire Mwl. but that doesn't make me blind to the facts.
Mkandara umetoa jibu zuri sana na la kina; unaloongea ni kama vile mtu aliyekuwa anapanda mlimani kutafuta asali halafu kabla hajafika huko mlimani akaona ndani ya shimo kuna maji ya taka yanayoonekana kama asali huku yakiwa yamezingirwa na nzi walioonekana kama nyuki, basi yeye bila kuwa makini kujiuliza kama kweli ile ni asali akaamua kujirusha humo kwenye shimo la taka bila ya kuwa na ngazi na hivi sasa amebaki hana asali na wala hawezi kujitoa humo shimoni mpaka apatikane mtu wa kumletea ngazi. Swali sasa ni wapi tutapata ngazi ya kututolea huko shimoni kwenye maji machafu tulikojitupa tukidhani ni asali? Kwa maana nyingine ya swali langu hili ni kuwa, je tutapambanaje na hao maadui wa wakuu wakati tumeshajiweka katika mazingira ambayo ni vigumu tena kupambana nayo?
Asilimia 90 ya watoto wetu hawapati elimu nzuri ya kuwafanya waone mambo kwa kina, na hao ndiyo generation ya kesho: kwa hiyo adui ujinga anazidi kukua. Huduma za afya ndiyo hivyo tena, tuliowapa mamlaka ya kuteletea huduma za afya nzuri wao wanatibiwa nje ya nchi na kutuacha tukiwa hatuna huduma zozote; na mbaya zaidi wanatufukuzia hata waganga wetu tubaki bila kuwa na waganga. Ardhi yenye raslimali yote imeuzwa na viongozi wetu kwa wageni, na kutuacha sisi bila chochote; hivyo kuzidi kututumbukiza kwenye dimbwi la umaskini. Bila elimu, tukikabiliwa na maradhi na kuzungukwa na umaskini, ni kweli kuwa wengi wetu tunakuwa hatuni mambo kwa mbali na kila mara tunakuwa tunafanya kazi kwa ajili ya kesho tu.
Kwa vile matatizo haya hayawahusu viongozi wetu, wamekuwa hawayashughulikii kutokana na tabia hizo hizo nilzosema hapo juu: wao wanajiskia kuwa wako entitled kila kitu kizuri, hawawabijiki kwetu, na wala hawalazamiki kufanya kazi zao kama inavyotakiwa, na hatuwachukulii hatua yoyote.