Tulijadili hili ....

Sasa wewe unaona hii mada inafaa kujadiliwa hapa JF kweli? embu soma mada za JF ya mwaka 2006 na 2007 uone!! Halafu linganisha na mada zinazoletwa hapa 2012!! Utanielewa vizuri.

kwa taarifa yako hao hao waliokuwa wanachangia miaka hiyo baadhi yao ndio hao hao wanachangia sasa. istoshe kama za siku hizi huzipend basi ondoka jamvini just like that.

pia unategemea kwa kuandika haya maneno yako ndipo utakapotubadilisha mtazamo wa kufikiri kwetu?? FYI shule haimfanyi mtu kuwa na akili bali humwongezea wigo na upana wa kufikiri tu. akili tulishazaliwa nazo mkuu huna uwezo wa kutufanya tuwe nazo tena.
 

ticha wangu achana na mwanamalundi , kaamua kabla mwaka kuisha aongeze idadi ya post maana hajafika 900 tangu hiyo 2007,so now kaamua tu kuchangia kila atakayepost ila ndo hivyo cha kuandika hana sa atafanyaje
 

kama huna uwezo huwezi fikiri kusafirisha familia, pia umejenga kwenu au lilelile banda la makutu ulimo zaliwa??? home is best
 
Tatizo lenu mnafikiri kila mwana JF yuko Dar kwenye mji wa mavurugu! Wengine tuko kwenye miji iliyotulia kama vile Mwanza, Arusha etc.
 
Kwani walikuruhusu uende kuishi na huyo mwanamume ili iweje? Mi mbona kwangu mama mkwe anakuja na sioni tatizo lolote!

yaani hiyo kwangu mwaka wa 11 huu mama yangu hajawah kuja kwangu akalala. atasalimia na kuondoka.
yaani alale kabisa ama baba si mbingu ingefunguka mkuu.

walijua wanaipeleka nikapigwe mpera sawa lkn sio kwenye upeo wa macho yao atii. nimejikuta kwamba hata nikiwa mjamzito siwez kwenda kwetu naona aibu baba atajua nilifanya so huwa nauchuna na kuonana na maza hadi nijifungue.
 

Sawa mama nimekupata. Endelea kutuelimisha. Tunafarijika sana tunaposoma michango yako yenye busara.
 
kama huna uwezo huwezi fikiri kusafirisha familia, pia umejenga kwenu au lilelile banda la makutu ulimo zaliwa??? home is best

Unafikiri kusafirisha familia ni uwezo au ni kukariri tu!
 
Different Strokes for Different Folks...

Kama wewe hupendi nadhani wengine wanapenda (labda ndio muda pekee watoto wamefunga shule kwenda kupaona walipotokea.... (The Roots...) au wewe huoni huu umuhimu
 

Jamani jikwamue kwenye mateso ya kijinsia!
 
Jamani jikwamue kwenye mateso ya kijinsia!

mateso gani?? wazazi wangu kutokuja kulala kwangu ni mateso?? ingawa inaudhi ila si mateso na ukiangalia kwa makini sana lazima heshima wepo ukweni wakizoeana sana wanaweza hata kujikuta wamejibizana vby ama baba akajamba mbele ya mkwewe bureee,
 
We umekuja na hoja ambayo naweza kukubaliana nayo japo si kwa asilimia 100; kuhesabiwa!!!

Waisrael wanajuana idadi ulimwengu mzima lakini hawalazimishani kwenda kubanana nchini mwao Israel.

Ndio maana wao ni Waisrael na sisi sio Waisrael. Hatulazimishwi kufanya wayafanyayo wao ha hakika hatuwalazimishi kufuata ya kwetu.

Karibu mlimani mkuu wangu.
 

gfsomnwin , hoyo haitakaa ibadilike, mm nimeolewa uchagani , baba na mama mkwe huwa wanakuja na wanakaa kwangu, lakini mm wazazi wangu ni watu wa kanda ya ziwa, hata siku moja hawajawahi kuja kula na kulala kwangu na nina ndoa ya miaka 9 sasa. ila mm napenda msimamo wao, kuja kwako na kukaa, kula, kulala ukweni ni AIBU kubwa, yaani ninamaanisha kwao wameishiwa kiasi wameolewa na mtoto wao. hiyo ndiyo tafsiri yao.
 
Ndio maana wao ni Waisrael na sisi sio Waisrael. Hatulazimishwi kufanya wayafanyayo wao ha hakika hatuwalazimishi kufuata ya kwetu.

Karibu mlimani mkuu wangu.

Atakayewabariki Waisrael atabarikiwa; Atakayewadharau Waisrael atadharauliwa pia.... kwa mwaliko wa kuja kwenu naweza, lakini si kubeba familia nzima.
 

  • Ina maana wewe huna haki sawa kaka zako? Aibu gani??
 
  • Ina maana wewe huna haki sawa kaka zako? Aibu gani??

Wala sijisikii AIBU yoyote ila, kwa sababu hizo ni mila na Desturi zetu a wala hazitokuja kubadilika kamwe. Na nashukuru Mungu katika kugawiwa urith kila mtu kapata sawa na mwenzie haijalishi ni mwanaume au mwanamke. Baba amegawa sawa kwa sawa.
 

lkn kweli ukishaolewa acha wazazi wako uende wewe kuwaona na sio wao kuja kukuona ni dharau kubwa sana.
 

It is an obvious question. Kwa nini harusi na sherehe nyingi hufanyika week end? Simple; ndo muda wengi wana nafasi. Same applies kwa sikukuu.
 
Atakayewabariki Waisrael atabarikiwa; Atakayewadharau Waisrael atadharauliwa pia.... kwa mwaliko wa kuja kwenu naweza, lakini si kubeba familia nzima.

Kiukweli kabisa nimekukaribisha wewe na wala si familia yako. Nyumba yangu kule mlimani inanitosha mimi na familia yangu (ambayo imeshatangulia) na mgeni mmoja tu.

Nakaa mbali na mlimani na familia yangu kwa zaidi ya miezi 11 kwa mwaka, kukaa nayo kwenye nyumba yangu mlimani kwa wiki mbili kwangu ni furaha isiyosemekana
 
Wala sijisikii AIBU yoyote ila, kwa sababu hizo ni mila na Desturi zetu a wala hazitokuja kubadilika kamwe. Na nashukuru Mungu katika kugawiwa urith kila mtu kapata sawa na mwenzie haijalishi ni mwanaume au mwanamke. Baba amegawa sawa kwa sawa.

hapo sawa bibie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…