mazoea yana tabu.
Wewe badala ya kuwakaribisha waje kwako unaenda kuwapa shida huko uendako! Jiulize utawakaribisha lini?
eti mkuu fikiria kama babu yako yupo; wewe ukifunga safari kwenda kwa baba yako hautamkuta kwa kuwa naye atakuwa ameenda kwa baba yake ambaye ni babu yako. Mlolongo huu ukifuatiliwa hauna maana yoyote. Ni kuwafaidisha watu wenye vyombo vya usafiri pasipo sababu yoyote.
Haa!!!!! lazima niende kwetu 24th Dec. narudi 30th Dec
hata mseme nini/ kwetu tutakwenda tu, haiwezekani tukae mwaka mzima tusiende kusalimu wazazi na bibi zetu home, ndiyo matokeo yake watoto wanakuwa hawajui kwao kwa sababu ya kung'ng'ania mjini. Home is best>
tena ngoja nikwambie ni kwa nn sisi wa moshi tunapenda kwenda. Mf, unandugu yako anaishi mbeya, mwingine mwanza, mwingine sumbawanga na hamjaonana mwaka mzima basi pale ndipo pa kwenda kuonana na kuongelea mambo ya maendeleo, na kama umepata tatizo pale ndipo yanatatuliwa wewe pamoja na ndugu zako na wazazi.
Wewe kaa huku mjini udhani wanaokwenda kwao ni wajinga!!!!
Hao utakaowaalika,kwanini waje?Kama wewe unaona si vyema kwenda kwa watu nao hawatakiwi waje kwako!
Haujakatazwa kwenda kwa watu; tunaangalia umuhimu wa kwenda kwenu / kwa baba yako siku za sikukuu wakati na wewe una mji na watoto; na kibaya zaidi kubeba familia nzima eti "tunaenda kula sikukuu"
Inategemea. Nauli unayo? Unakokwenda kuna sehemu ya kulala? Nyie ndo mnakaa na watoto hata hawawajui ndugu zao wala asili yao. Alafu pia yafurahisha. It's like wazungu wanakuja kutalii Africa wewe utasema wanapoteza hela. It's an adventure. Utakaa mahali pamoja na beach za Dar tu? Be adventurous!
Unamkuta Baba na Mama wanabebana na watoto kutoka nyumbani kwao wanasafiri eti wanaeda nyumbani walikozaliwa kula sikukuu. Binafsi siliungi mkono hata kidogo. Mtu ukishakuwa na familia - basi inakubidi usherehekee sikukuu na familia yako na ikibidi nawe ukawaalike ndugu zako (wapwa na wajomba).
Wanaopaswa kusafiri kwenda majumbani kwa wazazi wao kula sikukuu ni wale ambao hawajawa na familia na zaidi watoto wa shule.
Sasa we baba / mama unaacha mji wako na kusafiri umbali mkubwa; ukikuta hapo kwako kumeharibiwa na vibaka kwa kushirikiana na watu ulowaacha hapo kwako eti wakulindie nyumba / mji wako mtamlaumu nani?