Sungurampole
JF-Expert Member
- Nov 17, 2007
- 984
- 205
Maneno haya manne yamekua maarufu kwa siku za karibuni. Leo nimeyasikia kutoka kwa Mh Lembeli, akiwa mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi, Mazingira (Fahamu 12.6.12)
Tumeyasikia kwa Mwakyembe na huenda hata Hosea angeulizwa angesema aliwasafisha Richmond ili kuiokoa serikali. Mh Lowassa amekua akisema aliwajibika ili kuiokoa serikali. Majuzi Waziri wetu 'mpya' wa Nishati alisema alipoenda TANESCO amekuta madudu ya kutisha ila hakutuambia ni yapi, naye huenda ni ili 'kuiokoa serikali'
Watanzania hii serikali wanayoiokoa ndio tuliweka madarakani na ndiyo tunayoipa mamlaka ya kutawala.
Tujiulize na tutafakari:

- Je, ni sawa serikali yetu kutegemea kulindwa kwa viongozi wake kudanganya?
- Hivi inakuaje kiongozi anadiriki kutuambia alificha ukweli?
- Hivi ni kweli watanzania tumekufa ganzi au tumepofuka?
- Na hao wanaosimamia maadili ya viongozi wanajisikiaji juu ya haya?