Tulichagua hovyo na sasa tunatendewa hovyo, je tukae kimya ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tulichagua hovyo na sasa tunatendewa hovyo, je tukae kimya ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Dec 8, 2010.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Huyo alikuwa ni Twaha Jenerali Ulimwengu akituasa katika makala yake ndani ya gazeti la Raia Mwema la Septemba1, 2010 kabla ya uchaguzi.Alituasa kuwa tukichagua hovyo na halafu tukajikuta tunaanza kutendewa hovyo, tusiseme hovyo.

  Watanzania kama kawaida yetu tulipuuzia ushauri wake na tukamrudisha madarakani Raisi yule yule, chama kile kile, mafisadi wale wale na sasa tunaanza kuonja machungu yale yale ! Kwa kifupi tulichagua hovyo na hivyo tunaendelea kutendewa hovyo, je tukae kimya ?

  Ndani ya mwezi moja tayari lile zimwi lisilo na sura tulilokuwa tunapambana nalo ghafla limefufuka na safari hii limeingia kwa kwa staili mpya na ya kutisha. Majeraha tuliyompa yalimfanya akimbilie Ulaya kwa matibabu na sasa kapona na karudi kwa ari na nguvu zaidi.

  Hata hivyo linaloogopesha zaidi ni kuwa hii ya Dowans ni rasharasha tu, dhoruba yenyewe ya miaka mitano inatusubiri. Katika hii awamu ya pili, tutashuhudia ambayo yataifanya awamu ya kwanza ionekane kama vile tulikuwa peponi - si tumechagua wenyewe ?
   
 2. M

  Meshacky Member

  #2
  Dec 8, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuliowengi tulichagua vizuri ila watendaji wa serikali wasio na maadili kama wa NEC na UWT ndio waliotuangusha kwa sababu ya maslahi binafsi. hawakuwa na uzalendo walituuza. Lakini mchuma janga hula na wa kwao, hivyo athari za matendo yao zitawatafuna hata wao na ndugu zao.
   
Loading...