GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Wanabodi, Viwanda vyetu vikifanya kazi kwa uhakika umeme wetu hautoshi kabisa, Umeme wetu unatosheleza matumizi ya nyumbani tu hapa Tanzania.
Kwa sasa huu umeme kidogo tunagombania matumizi ya nyumbani na Viwandani, Aidha tugawane kidogo kidogo au kukata viwandani na kuacha majumbani, Au tuendelee na ukarabati na kufufua nguvu ya gesi ili tuwe na umeme wa uhakika.
Wakati wa JPM umeme ulikatwa viwandani kwa makusudi ili Raia wanyonge wasiozalisha kitu washangilie na kufurahia huku uchumi ukielekea ukingoni kutoka ukuaji wa asilimia 7% mwaka 2014 mpaka asilimia 4%mwaka 2020.
Leo hii mwaka 2022 mapato ya Tanesco yameongezeka sana hasa kutoka kwa watumiaji wakubwa, Viwanda vina lipa bili inayotakiwa ya umeme kwani wanapelekewa umeme wa uhakika, Kuna viwanda sasa vinalipa kwa mwezi Bilioni mbili za matumizi ya umeme baada ya Mama Samia na January Makamba kuruhusu ukarabati wa mitambo, Hapo awali umeme ulikatwa hovyo viwandani na kusababisha uchumi wa awamu ya tano kuwa hoe hae yaani chakali kwa uzalishaji hafifu
Hakuna mitambo iliyokuwa chakavu kama ya Tanesco, Kuna maeneo umeme ulikuwa unawaka lakini miundombinu yake imeoza kabisa hasa nguzo za umeme, Unaangalia na kujiuliza huu mtaa siku nguzo za umeme zilizooza zikidondoka usiku itakuaje kwa Raia wa maeneo hayo?
Suluhisho letu la umeme lilikuwa ni Kuongeza nguvu umeme wa gesi mwaka 2014 mpaka 2020, Lakini ukabila, chuki na sifa Taifa liliingia hasara la kujenga bomba la gesi, kulipa watu wa Lindi na Mtwara maeneo halafu mtu mmoja akazuia mpango wa Taifa wa umeme wa gesi
Haukufanyika ukarabati wowote kwa miaka mitano yaani 2015 mpaka 2020 kwenye mitambo ya umeme kufurahisha wanyonge na kuhadaa wananchi, Kulikuwa na Tear and wear ya kutosha, Kama uchumi ulivyokuwa unakufa kufurahisha wanyonge ndivyo ilivyo mitambo ya umeme ilikuwa inakufa kufurahisha wanyonge wapate mwanga wa umeme huku viwanda vikipunguza wafanyakazi wake kimya kimya
Hakuna nchi iliyoendelea bila kuwa na Fedha za kigeni ambazo zinapatikana kwa utalii au uzalishaji Mali yaani viwandani ambako umeme ulikatwa hovyo kwa miaka mitano iliyopita ya awamu ya tano kukomesha matajiri
Kwenye utalii huko Ngorongoro bado tunataka tena kufurahisha wanyonge, Tutafurahisha watu wa Ngorongoro wanyonge kwa gharama ya kuharibu utalii na uhifadhi wa Taifa zima hivyo kukosa pesa za kigeni, Kuna siku tena tutakuja hapa kulalamika kwanini Ngorongoro hakuna watalii na wanyama wakati tunataka kufurahisha wanyonge
Nini kifanyike kuondoa tatizo la umeme Tanzania
Mosi, Mpango wa gesi ndio suluhisho mambo ya kutegemea mvua zitanyesha lini yamepitwa na wakati, Tulipoishia kwenye gesi ndio tuendeleze
Pili, Turuhusu kipindi cha mpito cha ukarabati wa nguzo za umeme unaendelea kwa kutoa nguzo za miti na kuweka nguzo za sasa zenye hadhi ya kimataifa maeneo mengi zoezi linaendelea
Tatu,Katiba ni muhimu sana sana. Kutoruhusu masuala ya kitaifa kurekebishwa na kila Rais aingiapo madarakani, Mipango ya Taifa isiingiliwe na nguvu ya Urais kuanza kurekebisha mambo wakati yalipitishwa na Bunge zima mfano mpango wa gesi Mtwara na mpango wa bandari ya Bagamoyo
Matumizi ya vyanzo mbadala vinavyotunza mazingira kama Solar system za kisasa na umeme wa upepo, Kodi ipunguzwe kwenye vifaa vya umeme mbadala kama Solar system na kuelimisha wananchi matumizi sahihi ya solar system
Kelele zote hizi Leo ni kutokana na mtu mmoja kuamua kufurahisha wanyonge kwa gharama ya kuliangamiza Taifa, Maamuzi kama ya kukwapua kodi kinguvu ilikuwa kufurahisha wanyonge huku ajira na uchumi ukijifia
Kelele zote hizi za umeme ni kutokana na wanyonge wasiozalisha kuwashiwa umeme mdogo tuliokuwa nao wote wao huku Uchumi wa viwanda ukikosa umeme na kujifia taratibu na kusababisha mfumuko wa bei wa bidhaa kwenda juu
Kumbuka umeme tulionao Tanzania kwa sasa unatosheleza matumizi ya nyumbani tu, Vikiongezeka viwanda vya magari hata kimoja tu, Huu umeme hautoshi mahitaji ndio maana watu walianzisha miradi wa gesi Kuongeza umeme viwandani
Wakati watu wanaambiwa Serikali ya awamu ya tano imekopa zaidi walikuwa wabishi sana kwani zilitumika Propaganda kuwafurahisha wanyonge kuwa ni pesa za ndani kumbe ni mikopo ya gharama kubwa
Hakuna siri tena, Awamu ya tano uzalishaji Mali ulishuka sana viwandani kutokana na gharama za uzalishaji mfano mzuri Dangote alilalamika fitina za Tanesco watu hawakumuelewa wakati ule, Sasa wameelewa kuwa viwandani umeme ulikuwa unakatwa ili wanyonge tupate mwanga wa kutosha kwa gharama za kuua uchumi na ajira
Propaganda hazina msaada kwenye mambo ya msingi kama umeme wetu huu ni kidogo sana, Kikwete JM hakuwa mjinga kuanzisha miradi ya umeme wa Gesi na kuachana na kutegemea mvua ambazo kwa sasa hazieleweki kwa mabadiliko ya tabia nchi
Ninaunga mkono kipindi cha mpito cha kuweka tatizo la umeme sawa hasa kwa Kuongeza nguvu ya uzalishaji toka kwenye gesi ili viwanda vipate umeme wa uhakika