Tulia aonya wanaume kupiga wake zao. Kama wewe unasikia maumivu ukipigwa basi na mwanamke anasikia maumivu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
NAIBU Spika wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Ackson, amezindua kampeni ya Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia, huku akiwataka wanaume kuacha kuwapiga wanawake na kuwafanyia ukatili wa aina mbalimbali.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, jana, jijini Dar es Salaam, Dk. Tulia alisema jamii haipaswi kuwaona wanawake na watoto wa kike kama viumbe dhaifu, hivyo kuwanyanyasa kwa vipigo na kingono.

Dk. Tulia alisema wanawake ambao wamepewa nafasi kwenye nafasi za uamuzi, wameonyesha uwezo mkubwa kama ilivyo kwa wanaume, kutokana na ukweli huo, alisema hakuna sababu kwa jamii kuendelea na mtazamo hasi dhidi yao.

“Kwa nini umpige mwanamke? Kama wewe unasikia maumivu ukipigwa basi na mwanamke anasikia maumivu, hivyo hakuna sababu ya kumpiga mwanamke pengine kwa kuona kwamba ni mtu dhaifu asiyewezaa kujitetea,” alisema Dk. Tulia.

Aliitaka jamii kutumia siku hizo 16 kutafakari na kuanzisha mijadala ni kwa namna gani nchi inaweza kuondokana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuzungumza na wanafunzi vyuoni na mitaani ili waeleze yanayowakuta.
 
Chukueni maamuzi magumu ya wenzenu wa Kenya wanawadunda waume zao nusura kuwatoa roho
 
Back
Top Bottom