Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,808
- 218,460
Unaikumbuka ile ajali ya gari ya ya Nditiye , uliwahi kuambiwa ?Nimepigwa na butwaa baada ya kuona clip ikisambaa kwenye mitandao ikimuonesha Naibu Spika Tulia Ackson akidai kuwa alishawahi kuugua Covid 19 mara mbili.
Clip hii inamuonesha mwanamama huyu akitoa salamu za rambirambi kwenye msiba wa aliyekuwa Katibu Mkuu Hazina Dkt. Likwelile.
Mbali ya kudai kuugua Covid 19 mara mbili, Naibu Spika amedai kuwa huwa havai barakoa sababu ya kuwa na matatizo ya kupumua. Hivyo sio kwa sababu kuna kiongozi anayemuogopa kwamba hatamfurahisha pale akivaa barakoa.
Lakini swali kubwa la msingi, lini huyu kiongozi aliugua Covid 19? Kama aliugua huko nyuma bona hakutaarifu umma? Mbona hatukupewa taarifa kama kuna maabukizi mapya? Je, hata mwaka 2020 wakati baadhi ya wabunge wanafariki, walifariki kwa Covid-19?
Maoni; Kusubiri vifo vitokee alafu ndio mtuambie kuwa mliugua Covid 19 ni unafiki wa kuwaduza watanzania kisasa. Haufai kabisa bora mkae kimya.