Tulia Ackson mbona kapaniki hivyo, kulikoni?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Hotuba ya msomi nguli wa sheria imetuacha na maswali mengi hasa mbona anaelekea ana khofu ya kushindwa uchaguzi wa ubunge 2025?

Katika hotuba yake ya leo tumejifunza mambo mengi yakiwemo ufahamu wake wa sheria unatuacha hoi bin taabani.

Kwanza kapendekeza wawekezaji watafutwe na kuongezwa bandari ya Dar-es-Salaam ikimaanisha hata mkataba wa DP World hajausoma na hata kama aliusoma hajauelewa

Mkataba wa DP World umeipa kampuni tajwa uendeshaji wa hiyo bandari ya Dar-es-Salaam bila kuingiliwa na yeyote yule sasa wawekezaji zaidi wa bandari ya Dar-es-Salaam wapi na wapi?

Pili, kaongea kwa niaba ya wana Mbeya lakini hakutueleza ni lini na wapi maana wanambeya wengi wanasema hajawahi hata kukutana nao kwahiyo aache uongo na amwogope Mwenyezi Mungu.

Tatu, taswira yake ilikuwa ya ghadhabu na shari ikiashiria kuna alama za nyakati kesha zisoma hususani za matumizi ya maneno ya ."...... kuna maneno mengi yamepita hapa Mbeya...."

Maneno yapi yamepita Mbeya zaidi ya wapigakura kukujadili utendaji wako mbovu bungeni?

Na ya kuwa, tayari wamepata msitiri anaitwa Msomi Boniface Mwabukusu ambaye sasa ni Mbunge Mtarajiwa wa Mbeya mjini?

Kwa khali tunayoiona huyu mama anaweza kupata kiharusi wakati wowote ule maana hii tafurani siyo ya bure ina jambo linakuja bado lipo jikoni.
 
Hotuba ya msomi nguli wa sheria imetuacha na maswali mengi hasa mbona anaelekea ana khofu ya kushindwa uchaguzi wa ubunge 2025?
99% ya Ubunge wake ulitokana tu na Mbeleko ya Hayati Mr. 17 Machi, 2021 kwa kutumia Vyombo vyake na Watendaji wake ila Yeye kama Yeye hana Uwezo, hakubaliki, haaminiki na amejaa Unafiki mwingi.

Kama Mama ( Rais ) Samia atagombea 2025 nakuhakikishia nguvu ile ile itampitisha na atashinda hilo Jimbo huko Mbeya hata ikiwezekana Damu Kumwagika ili aendelee kuwa rubber stamp wa Maslahi ya Serikali mfano kwa hili la DP World.

Na nikusaidie tu kuwa moja ya sababu Kubwa kwa Yeye ( Madam Speaker ) Kuunga mkono hawa Wawekezaji wa DP World ni kumuonyesha Mama ( Rais ) kuwa yupo nae ili na Yeye Rais ( Mama ) aendelee Kumuamini na amsaidie kupita Ubunge hiyo 2025 na aendelee kumpigia Chapuo azidi kuwa Speaker wa Bunge ukizingatia ni Mwanamke Mwenzake.
 
99% ya Ubunge wake ulitokana tu na Mbeleko ya Hayati Mr. 17 Machi, 2021 kwa kutumia Vyombo vyake na Watendaji wake ila Yeye kama Yeye hana Uwezo, hakubaliki, haaminiki na amejaa Unafiki mwingi
Hata wana ccm wenzake wanajua hilo. Anajikomba komba tu.

Yuko tayari kushawishi Bunge liuze hata viwanja vya ndege ikiwa tu Mh Rais Atamhakikishia ubunge wake.
 
Tatu, taswira yake ilikuwa ya ghadhabu na shari ikiashiria kuna alama za nyakati kesha zisoma hususani za matumizi ya maneno ya ."...... kuna maneno mengi yamepita hapa Mbeya...."

Maneno yapi yamepita Mbeya zaidi ya wapigakura kukujadili utendaji wako mbovu bungeni?
Kwani kana akili basi?
 
Back
Top Bottom