Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Nakumbuka kipindi nipo darasa la 4, kuna nyumba ya jirani walivamiwa na majambazi , walimtoa mzee mwenye nyumba wakamvunja mguu na kuchukua vitu vingi mule ndani,
Wale jamaa walikua wanakwaruza Panga katika dirisha nyumba zote za jirani hivyo hakuna aliyethubutu kutoka kwenda kusaidia,
Mpaka kesho mzee wa watu ana kilema

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah!too sad,binafsi kabla sijaibiwa nilikua nakutana sana na matukio ya wezi kupigwa na hadi kuchomwa moto,nilikua nahuzunika na ni ukatili wa hali ya juu wa kumfanya vile binadamu mwenzako,sasa nilipokuja kuibiwa yale machungu yake nikasema siku ambayo nitakuta mwizi anapigwa sehemu na nikajiridhisha ni mwizi kweli,bhasi nitakachomfanya Mwenyezi Mungu atanisamehe,toka hapo sijawahi kukutana na tukio la kupigwa mwizi,ila hiyo siku yake hiyo
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 mbavu zangu
 
Mimi nilikuwa natoka kuangalia Mechi UEFA,2005 Finali ebwana wewe Sasa Mtaa wangu ulikuwa Mbali na Center kwenye Umeme/Banda umiza.Nilikutana na Majambazi yametoka kuvunja Maduka yanagawana na kupanga vitu kwenye Hilux mbili.Wajinga walivyoniona wakasema JIIIIIINI HILO LIACHENI mmoja alianza kuikoki SMG (Hahaha! Nilipofika nyumbani ndiyo nikajua kumbe UREA ilitiririka unknownly).

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulienda kushuhudia AC MILAN akilala kwa matuta.
 
Zamani nilikuwa nasikia roba ya mbao tu, hii isikie tu, wiki nzima shingo yangu nilikuwa naigeuza kama ngongoti, nilikutana na wajanja wajiji mitaa ya sinza walishuka kwenye gari ndogo aina ya corola nilidandiwa shingoni na njemba ya miraba minne huku mwingine akinipiga bapa za panga miguuni. wahuni sio watu wazuri hata kidogo
 
Mwaka Jana tulikua tunatoka kasulu mida ya jioni tulikua watu saba hivi kwenye cruiser tunaelekea mtendeli. Kwa wanaoifaham hii njia kuna utekaji magari sn, kwa hiyo mazungumzo ya kutekwa yalitawala na kuulizana kama kila mtu ana hela angalau kuanzia elfu 20 ili msala ukitokea angalau uwe na cha kuwapa LA sivyo utachapwa vibaya. Safari ikaendelea huku hofu imetawala, tukaipita malagarasi salama maana ndio eneo hatari zaidi, tukaendelea na safari hapo ishafika SAA mbili kasoro na angalau amani ikatawala. Sasa kuna eneo moja linaitwa nduta nako huwa ni hatari kwa matukio ile tunaimaliza tu tukaliona gogo kubwa limewekwa katikati ya barabara dereva akasema hapa tayari, lakini akapata ujasiri wa kulipita pembeni, baada ya kama dakika moja tukalipita fuso mbele yetu kwa kasi tukaenda kusimama mbele kuna kijiji dereva akaenda kununua maji. Tukiwa pale baada ya muda lile fuso tulilolipita njiani likatukuta pale kijijini. Yule dereva wa fuso akaja kutugongea dirishani huku yupo tumbo wazi na kaptula akawa anaongea kama kapagawa akasema yani nyie mna Mungu. Kumbe tulipowapita ndo walikuwa wahanga wa lile gogo na majambazi walikuwa bado wapo eneo LA tukio wamejificha coz waliposikia gari letu likija wakadhani ni askari doria hivyo ikawa pona yetu. Ila walimpiga yule dereva vibaya wakampora nguo na kila kitu, alikuwa na mpenzi wake naye wakamvua akabaki na sidiria tu mpaka wigi wakamvua, aisee nguvu zilituishia kila MTU alibaki na butwaa dereva akaondoa gari. Nakumbuka tulikua kimya ndani ya gari mpaka karibu tunafika nyumbani ndo akili zikakaa sawa tukaanza kuambiana kwa nn hatukuwasaidia wale watu hata hela kidogo ya kununua nguo au kumpa yule Dada angalau mtandio ajisitiri. Yaani kwa kweli sikulala karibia wiki lile tukio linanijia nawaza kama tungetekwa na kubakwa ingekuwaje. Toka siku hiyo sitakaa nitembee hiyo njia kuanzia SAA nane mchana maana ni hatari mno.
Mlikua mnaenda Kaliua au Urambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazee wa kazi walivamia kwa jirani yetu alikua ametoka kuuza gunia zake za mpunga,Kahama hiyo. Picha linaanza mida ya saa mbili mbili za usiku.Home nipo mimi ,bibi na mbwa .Mimi nimekaa nje ,bibi anaunga unga mboga maharage kwenye jiko la mkaa.Bwana wee ikavurumushwa risasi huko ,kwa lile wenge bibi akapiga katafunua chungu cha maharage na moto akamwagia maji kisha kwa speeed ya umeme ndani akafunga mlango akazima taa zote.Mimi nimebaki nje peke yangu kwa mbinu na medani za kivita nikavua shati nisionekane kisha nikajisunda kwenye jalala kimya.Baada ya sereka kuisha tafuta sana mbwa kuja kumkuta kumbe na yeye kaingia ndani zamani sana yuko chini ya uvungu wa kitanda.
mbwa ningemtupa porini uko ndani ndani sifugi mbwa Koko mimi
 
Mwaka 2010 TDM nilichelewa kurudi home kukatiza mtaa flani Jamaa kaja na Silaha Nikafiliri ni Mlinzi.
Akaniuliza umetoka wapi saa hizi ? Nikamjibu hovyo: wewe ni Mlinzi wa Barabara? Kama Mimi ni lindo lako twende uendelee kunichunga.

Nikafika Home kwani hakukuwa mbali na pale Nikajilalia Nusu saa Nasikia polis wanafanya msako wa Majambazi wameiba milioni 50 kwenye Duka la Mabegi la wahindi palepale .

Nakuja kugundua yule alikuwa Mmoja wao kauli Mbovu zilinisaidia alijua sina habari nao .nilimshukuru MUNGU.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee mimi na kumbuka jamaa walivamia jirani kigogo wakapiga mashine kama mbili hewani asitoke mtu
Kuchungulia n nyumba ya mama mmoja kiarabu analia tu
Rafki angu mmoja askar piga sana simu haikupokelewa
Aisee wangemuua yule mama maana walistuliwa ana pesa
Akili ikaja hivi kweli asubuhi kukiwa na msiba nitasemaje kwa Mungu wangu
Nikakumbuka nilipaki gari nisan yenye ngao mbele kuelekea geti kubwa
Na geti lenyewe linafungukia nje tunafunga tu komea la kati kati
Nikanyata nikazama kwenye gari
Ile napga stata nimekanyaga klachi gia namba mbili mafuta nmekanyaga hadi mwisho
Aisee nilipiga kelele za kukanyaga exceleretor na honi huyoooooo
Nikielekea magomen polis kufika mikumi nikakuta wa kova wapo around wamepak wakaniwashia ful taa
Nmeshuka kuwaeleza maneno hayatoki.
Wakanambia ongoza njia twende

Nikaongoza kurudi ile tunafika mtaani jamaa wakaziwasha mzee wakapasua tair yangu.

Mzee manjagu waliwawashia kama kumi hivi,wezi wakasepa vchochoroni,wa kova hawakuwafata wakiogopa yawezekana wanasilaha kubwa zaidi.kuingia ndan kwa mama walishamkatakata mama wa watu ili atoe pesa zaidi wakachukua kama mil 5 hivi
Tukapga kwa ndugu zake wakatukuta muhimbili

Ujambazi usikie tu ndugu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom