Jokajeusi
JF-Expert Member
- Jun 1, 2018
- 6,305
- 10,583
Tanzania sifaham kwanini hawaruhusu bangi.
Mbona iliruhusiwa Mke wang. Umekumbuka msokoto uliokuwa ukinisokotea
Tanzania sifaham kwanini hawaruhusu bangi.
Dah!too sad,binafsi kabla sijaibiwa nilikua nakutana sana na matukio ya wezi kupigwa na hadi kuchomwa moto,nilikua nahuzunika na ni ukatili wa hali ya juu wa kumfanya vile binadamu mwenzako,sasa nilipokuja kuibiwa yale machungu yake nikasema siku ambayo nitakuta mwizi anapigwa sehemu na nikajiridhisha ni mwizi kweli,bhasi nitakachomfanya Mwenyezi Mungu atanisamehe,toka hapo sijawahi kukutana na tukio la kupigwa mwizi,ila hiyo siku yake hiyoNakumbuka kipindi nipo darasa la 4, kuna nyumba ya jirani walivamiwa na majambazi , walimtoa mzee mwenye nyumba wakamvunja mguu na kuchukua vitu vingi mule ndani,
Wale jamaa walikua wanakwaruza Panga katika dirisha nyumba zote za jirani hivyo hakuna aliyethubutu kutoka kwenda kusaidia,
Mpaka kesho mzee wa watu ana kilema
Sent using Jamii Forums mobile app
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 mbavu zanguNakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.
Sent from my iPhone using JamiiForums
We fara kweriii. Hadi nacheka peke yanguTandika temeke nimekabwa sana miaka ya 2009 mpaka wakasema mwacheni huyu wa jana
Ulienda kushuhudia AC MILAN akilala kwa matuta.Mimi nilikuwa natoka kuangalia Mechi UEFA,2005 Finali ebwana wewe Sasa Mtaa wangu ulikuwa Mbali na Center kwenye Umeme/Banda umiza.Nilikutana na Majambazi yametoka kuvunja Maduka yanagawana na kupanga vitu kwenye Hilux mbili.Wajinga walivyoniona wakasema JIIIIIINI HILO LIACHENI mmoja alianza kuikoki SMG (Hahaha! Nilipofika nyumbani ndiyo nikajua kumbe UREA ilitiririka unknownly).
Sent using Jamii Forums mobile app
Kupitia posti hizi nishaijua Id ya mke wangu.Asante Swahiba japo ni zamani kidogo. Nimekumiss tho.....
Mlikua mnaenda Kaliua au UramboMwaka Jana tulikua tunatoka kasulu mida ya jioni tulikua watu saba hivi kwenye cruiser tunaelekea mtendeli. Kwa wanaoifaham hii njia kuna utekaji magari sn, kwa hiyo mazungumzo ya kutekwa yalitawala na kuulizana kama kila mtu ana hela angalau kuanzia elfu 20 ili msala ukitokea angalau uwe na cha kuwapa LA sivyo utachapwa vibaya. Safari ikaendelea huku hofu imetawala, tukaipita malagarasi salama maana ndio eneo hatari zaidi, tukaendelea na safari hapo ishafika SAA mbili kasoro na angalau amani ikatawala. Sasa kuna eneo moja linaitwa nduta nako huwa ni hatari kwa matukio ile tunaimaliza tu tukaliona gogo kubwa limewekwa katikati ya barabara dereva akasema hapa tayari, lakini akapata ujasiri wa kulipita pembeni, baada ya kama dakika moja tukalipita fuso mbele yetu kwa kasi tukaenda kusimama mbele kuna kijiji dereva akaenda kununua maji. Tukiwa pale baada ya muda lile fuso tulilolipita njiani likatukuta pale kijijini. Yule dereva wa fuso akaja kutugongea dirishani huku yupo tumbo wazi na kaptula akawa anaongea kama kapagawa akasema yani nyie mna Mungu. Kumbe tulipowapita ndo walikuwa wahanga wa lile gogo na majambazi walikuwa bado wapo eneo LA tukio wamejificha coz waliposikia gari letu likija wakadhani ni askari doria hivyo ikawa pona yetu. Ila walimpiga yule dereva vibaya wakampora nguo na kila kitu, alikuwa na mpenzi wake naye wakamvua akabaki na sidiria tu mpaka wigi wakamvua, aisee nguvu zilituishia kila MTU alibaki na butwaa dereva akaondoa gari. Nakumbuka tulikua kimya ndani ya gari mpaka karibu tunafika nyumbani ndo akili zikakaa sawa tukaanza kuambiana kwa nn hatukuwasaidia wale watu hata hela kidogo ya kununua nguo au kumpa yule Dada angalau mtandio ajisitiri. Yaani kwa kweli sikulala karibia wiki lile tukio linanijia nawaza kama tungetekwa na kubakwa ingekuwaje. Toka siku hiyo sitakaa nitembee hiyo njia kuanzia SAA nane mchana maana ni hatari mno.
mbwa ningemtupa porini uko ndani ndani sifugi mbwa Koko mimiWazee wa kazi walivamia kwa jirani yetu alikua ametoka kuuza gunia zake za mpunga,Kahama hiyo. Picha linaanza mida ya saa mbili mbili za usiku.Home nipo mimi ,bibi na mbwa .Mimi nimekaa nje ,bibi anaunga unga mboga maharage kwenye jiko la mkaa.Bwana wee ikavurumushwa risasi huko ,kwa lile wenge bibi akapiga katafunua chungu cha maharage na moto akamwagia maji kisha kwa speeed ya umeme ndani akafunga mlango akazima taa zote.Mimi nimebaki nje peke yangu kwa mbinu na medani za kivita nikavua shati nisionekane kisha nikajisunda kwenye jalala kimya.Baada ya sereka kuisha tafuta sana mbwa kuja kumkuta kumbe na yeye kaingia ndani zamani sana yuko chini ya uvungu wa kitanda.
Hahaha aliibiwa demu kwa kwelimkuu ni sim tu uliibiwa au dem?
Majambazi walijua gari lingeenda kituoni wangekamatwa.Daa imenichukua dakika kadhaa kukuelewa,kumbe huyo mama hakuwa sehem ya majambazi?,inaonekana majambazi yalikuwa yametoka kufanya tukio sehemu nyingine
Sent using Jamii Forums mobile app
Kupitia posti hizi nishaijua Id ya mke wangu.
not but pray.
Sasa karibu na home ndo mbaya zaidi...unaanza kuhesabiwa bia ngapi umekunywa, je leo umelewa hata wakikuingilia huwezi stuka.....kunywa mtaani uchawi Sana!