Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Kuna vibaka walikuwa wanasumbua sana mtaani. Hasa nyumba niliyokuwa nimepanga. Tulikuwa kama wapangaji 7 ukiachia mbali kijana wa mwenye nyumba. Mwenye nyumba alikuwa haishi hapo ila kijana wake tu

Sasa siku ya siku saa tatu usiku tumefunga geti dogo nje akapiga kelele kuashiria kuna kibaka karuka ukuta. Watu fasta wakawahi kwenye sehemu ya kurukia ukuta ili asitoroke. Tuka mweka mtu kati.

Jamaa mpangaji mmoja akaanza kumpiga kichwani mapigo hatari. Nikaogopa anaweza kufa. Halafu ni uani. Kesi ya kuua hiyo. Mtu mwemyewe mdokozi tu kwa jinsi nilivyofikiria. Nikamzuia na bahati nilikuwa nasikilizwa. Niliwaambia hiyo kazi niachiwe mimi.

Nikachukua vyuma Vya kutundikia mashati kama sita hivi halafu nikawasha jiko LA gesi. Nikawa naweka kwenye jiko LA gesi mpaka viwe vyekunduuu. Halaf namtumbukizia ndani ya jeans yake au ndani ya shati lake. Haloooo

Si kuruka na Makelele hayo. Harufu ya nyama kuungua ikasambaa kama tunachoma nini sijui.

Ikabidi aanze kumtaja boyfriend wa mpangaji mwenzetu kwamba wanafahamiana

Yakaanza kama mabishano kati yao. Boyfriend wa mpangaji mwenzetu akidai hamjui kabisa mwanzo. Lakini kibaka anakomaa na kutoa maelezo ya kina kuthibitisha kufahamiana. Dah.

Mimi Niko bize kuweka vyuma kwenye jiko LA gesi na vikiwa vyekundu nambambikia mwilini. Halafu yeye anaropoka kuomba msamaha na kusema ni jamaa yake na huyo jamaa.

Ikabidi T-shirt na jeans avichanechane ikabidi kumwekea vyuma vya moto katikati ya mapaja na kwapani huku akiwa kashikiliwa. Aisee

Walikuwa wawili Mwenzie alitutoroka.

Baada ya hapo hatukusikia tena purukushani za vibaka mtaani
 
Mi nilikutana na vibaka tu kama wanne. Narudi zangu hostel nilipanga za nje ya Chuo nikakutana na njema zimesimama njiani. Nikasema haina noma ngoja nipite tu!

Nilipitia Shaolinji Kempo kwa hiyo sio boya kihivyo. Nilichokifanya cha kwanza nikacheza na akili zao. Nikawa natembea huku mdogo mdogo napandisha suruali juu wala sina presha nikaibana fresh na mkanda.

Nikapita pembezoni yao wakakausha! Nilivyowaacha hatua kuwapa mgongo nikasikia kishindo nyuma watu wanakuja mbio. Nikajiuliza nikimbie au nibaki? Kama wana mbio kuliko mimi itakuwaje?

Nikageuke nyuma kuwasubiri ndiyo walikuwa wananikaribia kuona hivyo wakasimama ghafla! Wakaniogopa bhana! Wakageuza wao.
 
Nikiwa na miaka 14 au 15 kona ya msimbazi na uhuru kariakoo. Hapo jengo lililoandikwa Rupia. Nlikuwa natokea mtaa wa Kongo, nikaingia msimbazi sasa niko hapo ndo nataka nianze na njia ya kuelekea shule ya Uhuru.

Ilikuwa kama saa 10 au 11 watu wengi hapo kona wanapishana kila mmoja na mishe mishe zake na safari zake.

Ghafla mbele yangu nikaona jambo la ajabu. Katika wale watu wengi nikaona vijana watatu hivi wamenzunguka mama mwenye mtoto na wote wanakuja upande wangu. Kijana mmoja kushoto mwingine kulia halaf mmoja nyuma. Mama alikuwa amembeba mtoto mkono wa kushoto na kulia hand bag ilikuwa inaning'inia.
Sasa yule wa upande wa mtoto akawa bize kumliza mtoto nafikiri kumfinya au kumbugudhi mtoto ili mtoto asiwe na utulivu. Katoto kakawa kanalia na kuruka ruka. Sasa mama akawa anahangaika kumtuliza mtoto.

Sasa kijana wa upande wa handbag alikuwa na kiwembe anakata handbag kwa chini. Mimi niliona kabisa. Na kwautoto wangu nijua si sawa maana huyo mama anaharibiwa handbag na anaibiwa.

Haraka haraka nikanyoosha mkono kutaka kumtahadharisha huyo mama. Weweeeee

Huyo wa kiwembe akaona nnachokata kufanya. Akaniangalia usoni na kunionyesha kiwembe. Hayo macho yake na jinsi alivyokishika kiwembe ilikuwa ujumbe tosha kuwa ntakatwa viwembe. Nikatulia. Nikapishana nao kama sijawaona.

Vibaka noma
 
Kuna jamaa you tube anafundisha jinsi ya kujihami ukivamiwa na watu wenye silaha huku na wewe unamiliki silaha(bastola),comment hapo juu kuna visa kadhaa vya watu kuuliwa walipojaribu kutoa silaha soon ilipotokea ambush,..kwa mujibu wa maelezo ya yule muelimishaji wa you tube namna ya kujihami ni kwamba ukivamiwa ghafla baa au nyumban kwako usikimbilie kutoa silaha kwa sababu wao wanakua tayar wamejiandaa kwa lolote wewe haujajiandaa...jifanye unacooperate kwanza ,hakikisha unajua silaha ilipo na utaichukua pasipo kutazama na macho na ukiishika had kushoot iwe ni kitendo cha kushtukiza yan usichukue muda mrefu kuiset au kulenga...otherwise bora uwe mpole maana kitendo cha kuishika wakakuwahi wao matokeo yake ndio hayo wanakuua au kukujeruhi zaidi kuliko wenzako waliotoa ushirikiano
Kutoa ushirikiano kwingine mtihani sana. Kuna wajuba huwa wanawala tigo wahanga, je utoe ushiriano na silaha kiunoni?
 
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nikiwa shule O-level ilikua boarding.
Siku hiyo ilikua week end tukatoroka shule kwenda mitaani kuinjoy, kula vitu adimu na kutafuta mademu.
Basi bhana tulikua wanne tumeenda mitaani tumefanya kila kitu mpaka mida ya saa tatu hivi usiku( ilikua ni kijisehemu kimechangamka sana, CENTER)
Wakati tunajiandaa kuanza safari ya kurudi shule mara ghafra wazee wa kazi wakavamia pale kwenye maduka, basi bwana purukushani za hapa na pale kila mtu akatoka nduki.
Wengi tulikimbilia makaburini coz hayakua mbali halafu ndo sehemu iliyokua walau mtu unaweza kujificha.
Basi bwana tumejificha kwenye makaburi wazee wa kazi wakaendelea kukiwasha duka baada ya duka, kati ya hayo maduka kulikua na frem ya salon na kuna wateja walikua wananyolewa(baada ya kuvamia jamaa walizima taa wakawa kimyaaa) basi majambazi si yakafungua mlango wa salon,hahahahaaaa!
Alitoka mshkaji mmoja amenyolewa upande na shuka jeupe shingoni nduki ya ajabu sana kama mshale, jamaa nae akakimbilia uelekeo wa makaburini, ile kufika akatukurupua( maana alikua nduki mbaya halafu anakimbia juu ya misalaba huku shuka linapepea kwa nyuma) kuona vile group lote tuliojificha tukadhani jamaa alikua kafufuka basi tulitoka nduki kumkimbia, na yeye kuona tunakimbia akadhani nyuma kuna jambazi linamkimbiza akaongeza spidi kutufuata, jamani jamani ilikua mshike mshike wa hatari, tulikimbia kama wendawazimu,.
Huku nyuma majambazi yameshaondoka sie tunakimbizana na jamaa. Tulijikwaruza sana kwenye vichaka pamoja na kuanguka kwenye makaburi, tuliumia sana.


Sent from my iPhone using JamiiForums
noma sana mkuu
 
Kuna siku Niko na jamaa yangu tuliamua kwenda Buguruni kucheki totozi zinazo danga mitaa ile, Nukumbuka tulifika buguruni mida ya SAA 5 usiku tukaanza na lile chimbo opposite na kituo cha daladala cha buguruni ukitokea Tazara tukafanya yetu pale mpaka mida ya saa7 usiku. Baada ya hapo jamaa yangu alinambia twende chimbo lingine ambalo lipo kwenye vichochoro chini ya buguruni sheli pale, basi mi bila hiyana nilimkubalia jamaa yangu tukaanza kujongea.

Baada ya kuvuka barabara pale darajani ( daraja la wavuka kwa miguu pale buguruni) ile tuna anza kuingia uchochoroni tuka kutana na jamaa mmoja akaanza kutuzingua basi tukawa tuna mpotezea tukijua kalewa. muda huohuo hatukujua jamaa katumia ishara gani kuwaita wenzake mara tukashangaa tumezungukwa na kundi la watu si chini ya 20 wenye mapanga, sime n.k. Fasta nikamtonya jamaa yangu kuwa asije akapaniki au kujionesha yeye ni mbabe maana namjua jamaa yangu ni mtu wa kupaniki mapema. Basi tukaambiwa tupige magoti tukapiga kwa kwa kuwa nilikuwa maji kidogo akili zikachaji fasta nikawaambia naomba kuongea na kiongozi/ mkuu wenu, wakati huo kulikuwa na walinzi wa maduka pembeni chini ya sheli pale lakini waliishia kutuangalia bila ya msaada wowote na virungu vyao. Basi wale vibaka walikubali mimi niongee na mkubwa wao, nika mwambia naomba niinuke tuongee kwa pembeni kidogo wakati huo rafiki yangu yeye kawekwa chini ya ulinzi na wale vibaka wengine, baada ya kutoka pembeni kidogo na bosi wao nilianza kupiga fix ( kumdanganya ), nilimwambia unajua nyie mnawezwa kamatwa kishamba sana na police? wewe unajua sisi ni akina nani? kwa taarifa yako sisi ni usalama wa Taifa hapa napo ongea na wewe nalindwa na askari si chini ya 50 na wako hapa hapa ni kitendo cha kutoa ishara tu ndani ya sekunde mnakamtwa, jamaa akaanza kutepeta kwa kufanya aniamini zaidi nikamtolea kitambulisho nikamuonesha then nikakiludisha mfukoni bila ya yeye kukisoma ( kilikuwa ni kitambulisho cha chuo hakuweza kukigundua) nilipo muonesha kitambulisho yani ndio alitepeta hatari mi kimoyomoyo nikasema yesi haya si ndio mambo. Baada ya kuona bosi wao kalowa nikamwambia naomba umwite na yule jamaa yangu aliye wekwa chini ya ulinzi aje hapa, basi akafanya hivyo wakati huo wale vibaka wengine wakajua mimi niko na bargain na boss wao mambo ya pesa. Baada ya jamaa yangu kuja nikamwambia yule boss wa vibaka atusindikize mpaka kituo cha police cha buguruni sheli pale. Jamaa akawaambia wenzake kuwa analudi basi njiani nikaendelea kumpiga fix za hatari na jamaa yangu naye baada ya kuusoma mchezo na akamuonesha kitambulisho then akakiweka fasta mfukoni ( kitambulisho cha chuo) jamaa akawa anaomba msamaha kuwa tusimpeleke kituoni. Baada ya kufika maeneo ya sheli nikamwambia yule boss wa vibaka kwa sauti ya juu na ya hasiraa "HAYA RUDI ULIKOTOKA NA KESHO TUTAKUJA NA DEFENDER MAENEO YALE YALE OLE WENU TUWAKUTUTE TENA, LEO ILIKUWA NI ONYO TU" baada ya kumwambia hayo jamaa alikimbia kwa wenzake, baada ya hapo tukapanda daladala kuludi maskani kwetu huku tukiwa tunapumua kwa nguvu kweli maana hatukuamini, kuwachoropoka watu zaidi ya 20 wenye mapanga n.k kwa kutumia maneno na akili za ujanjajanja.

Sitokuja sahau hiyo siku, kwa ujanja wetu na jamaa yangu VITAMBULISHO VYA CHUO VILITUSAIDIA SANA INGAWA WAO WALIJUA NI VITAMBULISHO VYA MAAFISA USALAMA.
Hii chai..uongo wa kijinga.
 
January 2021 nimeporwa na majambazi mara mbili ndani ya wiki 1hapa Johannesburg. First time nimetoka ofisini jioni saa kumi hivi naelekea home,mara gari ikaminya break kisha zikashuka njemba mbili na bastola huku nikisikia sauti wanazikoki kabisa. Nili freeze pale wakachukua sim, begi la mgongoni na hela nilikua nazo mfukoni kiasi. Hapo watu wanaendelea na mishe zao kama kawaida na hakuna mtu alikua bothered na lile tukio. Nikaamua kuendelea na safari mpaka home .

Siku 4 baadae asubuhi nimenunua smartphone mpya ,nimeingia ofisini ndio naiset ili nirudi hewani mara kuna mteja kaingia,then wa pili kafuata na ile kumfungulia mlango tu mwingine akaingia nae. Suddenly tuna wateja watatu halafu ukizingatia kila mtu kavaa mask ya covid19. Jamaa wawili wakato bastola kisha wakatokomba kila kitu pamoja na sim yangu mpya,,nilitamani ningekua Rambo. Jamaa yangu akaniambia Rambo hawezi purukushani za mjini labda ningekua van Damme ningewamudu .
 
January 2021 nimeporwa na majambazi mara mbili ndani ya wiki 1hapa Johannesburg. First time nimetoka ofisini jioni saa kumi hivi naelekea home,mara gari ikaminya break kisha zikashuka njemba mbili na bastola huku nikisikia sauti wanazikoki kabisa. Nili freeze pale wakachukua sim, begi la mgongoni na hela nilikua nazo mfukoni kiasi. Hapo watu wanaendelea na mishe zao kama kawaida na hakuna mtu alikua bothered na lile tukio. Nikaamua kuendelea na safari mpaka home .

Siku 4 baadae asubuhi nimenunua smartphone mpya ,nimeingia ofisini ndio naiset ili nirudi hewani mara kuna mteja kaingia,then wa pili kafuata na ile kumfungulia mlango tu mwingine akaingia nae. Suddenly tuna wateja watatu halafu ukizingatia kila mtu kavaa mask ya covid19. Jamaa wawili wakato bastola kisha wakatokomba kila kitu pamoja na sim yangu mpya,,nilitamani ningekua Rambo. Jamaa yangu akaniambia Rambo hawezi purukushani za mjini labda ningekua van Damme ningewamudu .
Duh!
Pole mkuu,inachekesha na kusikitisha at the same time..
 
January 2021 nimeporwa na majambazi mara mbili ndani ya wiki 1hapa Johannesburg. First time nimetoka ofisini jioni saa kumi hivi naelekea home,mara gari ikaminya break kisha zikashuka njemba mbili na bastola huku nikisikia sauti wanazikoki kabisa. Nili freeze pale wakachukua sim, begi la mgongoni na hela nilikua nazo mfukoni kiasi. Hapo watu wanaendelea na mishe zao kama kawaida na hakuna mtu alikua bothered na lile tukio. Nikaamua kuendelea na safari mpaka home .

Siku 4 baadae asubuhi nimenunua smartphone mpya ,nimeingia ofisini ndio naiset ili nirudi hewani mara kuna mteja kaingia,then wa pili kafuata na ile kumfungulia mlango tu mwingine akaingia nae. Suddenly tuna wateja watatu halafu ukizingatia kila mtu kavaa mask ya covid19. Jamaa wawili wakato bastola kisha wakatokomba kila kitu pamoja na sim yangu mpya,,nilitamani ningekua Rambo. Jamaa yangu akaniambia Rambo hawezi purukushani za mjini labda ningekua van Damme ningewamudu .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya 2003 nilivyamiwa na majambazi mitaa ya karibu na beria ya oldonjoshambu....nikiwa natokea kenyaa,walikuwa Ni wasomali aka mashiftaa,mamaeee nilikua kwenye Nissan patrol,Niko Mimi na swaiba wangu tunasafirisha magendo.jamaa waliweka mawee makubwa mawili barabari,tulikuwa speed sana Kama mita Mia hivi tuliona Yale mawee jamaa nikamwambia man boraa tufee kwa ajali bro hakuna kusimamaa,jamaa aka chepuka speed ile ilee porini ngomaa ikapenyaa mbele akatokea msomali kashika bunduki la mkanda Kama Rambo,nikamwambia jamaa mpelekeee chumaaaa walaaah nisikia kishindo puuuuuh na vidamu kwenye kioo ngomaaa ikanyooka break beria ,kucheck kwenye ngao naona Kuna kipandee Cha mguu
Poleni Sana ndugu,,,,, naamini mlitoa maamuzi magumu lakini sahihi sana
 
Kumbe mwamba kapanga na walee warombo wezake wanekabee mitaa ya mbelee waniibie simu na pesa,saa tumetembea Kama atua 30 hivi jamaa angu akawa Kama anajisaidia,mi Niko mbele Mara paaap nikapigwa robaa,katika kufurukuta jamaa akawa ameshika t-shirt kanifunika usoo...asee nilikua na vimazoezi vya shotokani walijuta Yule wambelee yangu Nika mpiga finger printi ya macho nilikua nitoboe macho akaachia t-shirt,analia Nika mgeukia Yule mwingine Niki weka stensi Nika mpiga washgelii mojaaa ya maana,baada ya hapo niliwaachia t-shirt na kutoka nduki mpaka camp
Hahaha hilo pigo la finger print ndo likoje mkuu

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Me nilikutana nao mwaka jana. lakin hao tuseme ni vibaka wako na bodaboda. ilikua arusha njiro natoka kwenye sherehe kwenye kotaz za fidforce njiro .basi nikatembea mpama barabara kuu .ikapita boda nikasimamisha . nikapanda jamaa akaenda simama sehemu.kumbe kuna wenzie wawili .duuu wazee sjui nilipata wapi ujasiri yaani kama movies nilishuka .kwenye pikpk mazima nikamvaa mwenye sime wengine hawakua na siraha .nilishika ile sime kwenye makali uku wengine wakinipiga ngumi za uso .sikuhachia sime mpaka nilipofanikiwa kuwanyanganya .baada ya kuona nmechukua sime wale jamaa wanakimbia kuwasha toyo haiwak lkn na mimi hapo sina nguvu tena . najaribu kuwafata nashindwa . baada ya hapo natembea kuomba msaada watu wananikimbia maana niko na panga ina damu nyingi na mimi mikono inamwagika damu .mpaka leo vidole vi wili havifanyi kazi.
staki kumbuka iyo siku
Eeeeh!! Pole Sana.... Kuna mikoa haifai kutembea usiku Kama hauna usafiri
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom