Tukutane hapa tuliowahi kuvamiwa na majambazi tupeane uzoefu/ushuhuda

Kuna jamaa you tube anafundisha jinsi ya kujihami ukivamiwa na watu wenye silaha huku na wewe unamiliki silaha(bastola),comment hapo juu kuna visa kadhaa vya watu kuuliwa walipojaribu kutoa silaha soon ilipotokea ambush,..kwa mujibu wa maelezo ya yule muelimishaji wa you tube namna ya kujihami ni kwamba ukivamiwa ghafla baa au nyumban kwako usikimbilie kutoa silaha kwa sababu wao wanakua tayar wamejiandaa kwa lolote wewe haujajiandaa...jifanye unacooperate kwanza ,hakikisha unajua silaha ilipo na utaichukua pasipo kutazama na macho na ukiishika had kushoot iwe ni kitendo cha kushtukiza yan usichukue muda mrefu kuiset au kulenga...otherwise bora uwe mpole maana kitendo cha kuishika wakakuwahi wao matokeo yake ndio hayo wanakuua au kukujeruhi zaidi kuliko wenzako waliotoa ushirikiano
 
It's true, kwa wale popo Kama wenzangu na unamiliki Chuma (sijui Ni Glock, Beretta, etc.) Cha kwanza unatakiwa silaha Kama kwenye gari umeiweka sehemu (let's say glove compartment) inakua tayari ushafungua usalama na ngoma iko chemba. Ngoja nitarudi
 
Ni kweli kabisa

Sent from my M1 Lite using JamiiForums mobile app
 
Katika Uchaguzi mdogo wa Biharamulo Magharibi kufuatia kifo cha Fares Kabuye (kiboko ya Magu -Ubunge) by then, nilivamiwa na Red Brigade wa Chadema usiku hotelini. Robert Hotel wakataka kunivunjia mlango lkn hawakufanikiwa, waliwahiwa na Mkuu wa FFU Telesphory Anaclet akauawa Chacha Werema mdogo wake Mwita Waitara. Najiuliza ingekuwaje wangezama ndani?
 

Mkuu hapo umekutana na VIBAKA tu ,Jambazi anatembea na CHUMA ,Ukikutana naye lazima Ukae Chini.

Ebu sikiliza matukio ya Ujambazi yanavyokuwa.
your_browser_is_not_able_to_play_this_audio


your_browser_is_not_able_to_play_this_audio
 
Me nilikutana nao mwaka jana. lakin hao tuseme ni vibaka wako na bodaboda. ilikua arusha njiro natoka kwenye sherehe kwenye kotaz za fidforce njiro .basi nikatembea mpama barabara kuu .ikapita boda nikasimamisha . nikapanda jamaa akaenda simama sehemu.kumbe kuna wenzie wawili .duuu wazee sjui nilipata wapi ujasiri yaani kama movies nilishuka .kwenye pikpk mazima nikamvaa mwenye sime wengine hawakua na siraha .nilishika ile sime kwenye makali uku wengine wakinipiga ngumi za uso .sikuhachia sime mpaka nilipofanikiwa kuwanyanganya .baada ya kuona nmechukua sime wale jamaa wanakimbia kuwasha toyo haiwak lkn na mimi hapo sina nguvu tena . najaribu kuwafata nashindwa . baada ya hapo natembea kuomba msaada watu wananikimbia maana niko na panga ina damu nyingi na mimi mikono inamwagika damu .mpaka leo vidole vi wili havifanyi kazi.
staki kumbuka iyo siku
 

how were you able to accomplish this ? ebu elezea vizuri...
 
Miaka ya 2003 nilivyamiwa na majambazi mitaa ya karibu na beria ya oldonjoshambu....nikiwa natokea kenyaa,walikuwa Ni wasomali aka mashiftaa,mamaeee nilikua kwenye Nissan patrol,Niko Mimi na swaiba wangu tunasafirisha magendo.jamaa waliweka mawee makubwa mawili barabari,tulikuwa speed sana Kama mita Mia hivi tuliona Yale mawee jamaa nikamwambia man boraa tufee kwa ajali bro hakuna kusimamaa,jamaa aka chepuka speed ile ilee porini ngomaa ikapenyaa mbele akatokea msomali kashika bunduki la mkanda Kama Rambo,nikamwambia jamaa mpelekeee chumaaaa walaaah nisikia kishindo puuuuuh na vidamu kwenye kioo ngomaaa ikanyooka break beria ,kucheck kwenye ngao naona Kuna kipandee Cha mguu
 
Duh
 
Bro em ongezea nyama kdg aisee aliweza fyatua risasi? Na damage ilikuaje kwenye gari
 
Bro em ongezea nyama kdg aisee aliweza fyatua risasi? Na damage ilikuaje kwenye gari
Mkuu jamaa wa mbele hakuweza kufyatua risasi,maana walizani tutapunguza mwendo na kusimama Ila kwa speed ileile 190 tukachepukaa so alitokea barabarani kwa ghafla ndo tuka mgonga,Ila wezake walijaribu kutufyatulia risasi kadhaa zikapika tairi ya nyumaa spea na kuvyunja kioo Cha nyuma,kwakweli mnyama Nissan patrol zilee chura Ni nomaa,polisi walituambia kweli nyie Ni wanaume washoka,kipindi hicho na miaka 19 mwezangu 23
 
ndo dawa yao mbwa hao,wapemba noma
 
Magendo yenu wakayasamehe au?
 
Pole Mkuu.
 
Duh!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…