Tukutane hapa tuliowahi kufanya na kufanyiwa matukio ya Kikatili na kutisha maishani

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,468
23,744
Nakumbuka tukio hili kama vile ni jana. Ilikuwa miaka ya 80s nimeenda Mkoani likizo kumtembelea bibi. Kulikuwa na tabia za kibabe sana hiyo sehemu.

Bahati mbaya mimi nlikuwa mweupe, mnene naonekana kama mayai mayai sana wakataka kuwa wananionea sana mpirani.

Siku ya tukio nilienda kucheza nikiwa na mpira wangu wa kujazwa na pump ya baiskeli. Gozi. Ilikuwa nadra sana miaka hiyo kuwa na gozi lile la mabaka ya white and black. Mzee aliniletea toka UK alipokuwa masomoni.

Jamaa wakaanza rough kiasi nikawa naogopa hata kucheza mpira nikatoka nikawaacha wacheze wao kumbuka hapo mpirani mimi tu ndo nmevaa viatu. CHACHACHA.

Baadaye nikaona ni muda wa kurudi home, bibi ataanza nitafuta, mpira ulipotoka nikaufuata na kusema naondoka. Jamaa mmoja mbabe alinifuata akaupiga mpira mikononi mwangu ukaanguka. Nikamfuata akamrushia mwenzie, nilipomfuata naye akamrudishia huyu mwingine.

Nlisumbuliwa hivi kwa muda huku watu wakicheka. Alipoona wanafurahi akakimbia pembeni sehemu ya fundi fenicha akachukua kipande cha mbao na kilikuwa na msumali akautoboa mpira, nachokumbuka nliona kipande hicho hicho cha mbao na kumpiga nacho kichwani. Alipasuka na ule mshtuko akaanguka.

Nlimfuata nikamkalia juu nlimpiga ngumi nyingi usoni nikilia. Watu wengine wakaanza kimbia kwa hofu. Jamaa nadhani alipoteza fahamu maana aliangukia kisogo na hakuwa aki respond ingawa alikuwa mkubwa kwangu.

Then nilianza mburuza barabarani kutaka enda naye home kwa bibi. Watu walinishangaa maana nlikuwa napiga kelele kama mtu aliyepagawa nilimburuza mpaka sehemu moja kuna shamba nikaanza zoa mabua ya mahindi kumfunika nayo nikiomba kiberiti nimchome moto.

Maana watoto wa kule walikuwa wana tabia ya kutembea na viberiti ili jioni wakoke moto kutengeneza matanuru ya kuchomea mahindi na kuota pia.

Hapo ndio alipokuja bibi yangu anakimbia akipiga kelele na kuja nikamata huku akiongea maneno fulani ya kilugha akaja nishika kichwa na kifua, aliongea kama dakika kadhaa nikatulia.

Bibi alinishika mkono kunirudisha home. Akakimbia jirani kumwita mama wa yule kijana. Mimi niliwekwa chini ya ulinzi wa Baba Mdogo pale home nikiwa nimefungiwa chumbani.

Yule bwana alipelekwa Hospital na sikutoka kwenda nje kwa muda wa week moja mpaka alipokuja nichukua mzee kunirudisha Dar. Mpaka leo huwa nakumbuka hicho kitendo.

Baba yangu mdogo alikuja patwa na kesi ya kupiga askari wawili kisha akawa anawavuta kwenda kuwalaza shambani akawakanyage na tractor, kelele za watu zilimrudisha akili akakimbia hatukumwona tena mpaka after 15 years kumbe alitorokea nchi jirani. Bibi alipata kutuambia tulikuwa na shida flani hivyo tujiadhari sana na hasira au watu wanapotukwaza.

Kilikuwa ni kitendo cha kikatili sana nikiwa na umri mdogo sana.
 
Mimi nilikua nikiishi na kaka yangu, hapo ni baada ya mzee kufariki, kaka alioa kwa hiyo tulikua tukiishi mimi wifi na kaka

Siku moja alikuja mama yake huyo wifi, alitokea tu kunichukia sikumfanya chochote, nakumbuka walikua wanapika na walikuwa na mtindo nikitaka kuosha vyombo naambiwa acha yanai nikae tu hivyo nilikua nimejilalia chumbani ila sikulala usingizi.

Nikamsikia mama yake wifi anamwambia mwanae na leo hatokula kwanza tukila tutamfungia mlango, mimi niliwasikia wao hawakujua kama nimewasikia na nikajisemea ngoja nione kama watafanya hivo, kweli chakula kiliiva sikuitwa na mlango ukafungwa kwa nje.

Kweli walikula walipomaliza wakanifungulia na mimi nikatoka sikuulizia chakula sikuulizia chochote nilikaa njaa mpaka jioni na walikuwa na mtindo wanapenda kunisema wakati wa kula sikuzoea hayo maisha nikawa najikuta naacha kula.

Mwisho wa siku nilimuomba kaka anirudishe nyumbani tu na nilirudi baada ya kuwa na mimi kuchoshwa na manyanyaso nikawa naweka mgomo sitaki kula sitaki chochote mpaka kaka akaambiwa kuniita jibu langu likawa moja tu nirudishe nyumbani asubuhi ya pili nikarudishwa.

Sitasahau hilo mpaka naingia kaburini yaani nilipitia kipindi kigumu sana kwenye maisha yangu, nashukuru nilishasamehe maisha yanaendelea sasa.
 
mimi nilikua nikiishi na kaka yangu, hapo ni baada ya mzee kufariki, kaka alioa kwa hiyo tulikua tukiishi mimi wifi na kaka

siku moja alikuja mama yake huyo wifi, alitokea tu kunichukia sikumfanya chochote, nakumbuka walikua wanapika na walikua na mtindo nikitaka kuosha vyombo naambiwa acha yan nikae tu hivyo nilikua nimejilalia chumbani ila sikulala usingizi....

Huyo wifi yako mpaka leo bado wapo pamoja na Bro wako? Na je haoni aibu sshv mkionana?? Vipi kaka yako alikuja kugundua walikua wanakunyanyasa kula?
 
Huyo wifi yako mpk leo bado wapo pamoja na Bro wako? Na je haoni aibu sshv mkionana?? Vp kaka yako alikuja kugundua walikua wanakunyanyasa kula?
Yeah wapo pamoja mpaka kesho, kaka anajua kila kitu ila ndio hivyo tena tangu kipindi hiko hakuna aliewahi kumkumbushia mwenzie chochote kuhusiana na hayo maisha zaidi ya salam tena salam ni kaka ndio alianza, mimi niliondokaga kwa hasira nikawa sitaki hata kuwasikia ila mwisho wa siku niliona haina haja sote mavumbini tutarejea nikasamehe lakini wifi sijawahi onana naye na Mungu alivyo wa ajabu kila wakija home mimi sipo au mimi nikienda wasalimia kwao siwakuti sijuagi why inakua hivyo ni muda mrefu mnoo umepita na salam zenyewe ni kupitia mitandao ya kijamii
 
Tukio pekee kidogo la hatari miaka hiyo ni pale nilipompiga mtoto wa balozi wa nyumba kumi karibu nimuue, hii ni baada ya kutaka kunipokonya gari yangu ya udongo na niliyoitengeneza Mimi mwenyewe, kesi ilikuwa kubwa hadi familia ya babu yangu na familia ya balozi zikawa hazielewani pale kijijini hadi hivi sasa ninapoongea wajukuu wa familia yetu na ya balozi hawaelewani kabisa kisa ni hili tukio alafu cha ajabu aliyetenda na aliyetendewa(Mimi na MTT wa balozi) wala hatuna kinyongo.

Umri baina yetu ni mkubwa mno Ila tuko fresh kabisa, ndugu zangu ndio wanachukiana na baloz family, sijui kuna kipi cha zaidi kinaendelea maana kabla ya ugomvi zilikuwa familia rafiki tu.

Familia za kiafrika mambo yake ni mazito sana, zinatafutwa sababu ndogo tu.
 
Kwakweli ukatili mkubwa sijawahi kufanyiwa zaidi ya mimi mwenyewe kujifanyia ukatili!
Najiomba msamaha sana kwa niliyowahi kujitendea.

Kijana wa jana nisamehe sana ndugu yangu
Hii inafaa iingie kwenye kumbukumbu za Guinness World. Ukifunguka japo robo utatumiwa zawadi. Nahisi ulikuwa hupendi shule unajificha kwenye containers za MO kuleee juu kuvizia muda wa kurudi home gari la shule likurudishe nyumbani
 
Utotoni baada ya kucheza mpira tukawa tunapiga stori zetu dimbani huku kigiza kikiingia, kama mnayojua stori mida hiyo huwa tamu kinoma!! Mara akaja bro akasema ondokeni usiku sahizi basi kila mtu akawa mzito maana stori zimebamba kichizi.. tumekaa pale mara tukasikia jiwe kubwa limerushwa ule muda tunajiuliza nikashtukia kitu kizito kimetua kichwani na lile giza nikahisi kama nimepigwa na mfuko wenye maji maana nililoana dkk0 tuu ila maji yana harufu ya damu.

Nikapiga kelele akapita mzee flan akanishika mkono maana sioni akanipeleka hadi home na wale washkaj zangu, nikapelekwa hospitali nikapigwa nyuzi za kutosha! Maza akapiga kelele sana tabia za kukaa nje usiku, basi ikapita miaka 20 nimekuwa mtu mzima ndo bro anakuja kuniambia kwamba yeye ndio alirusha jiwe kututisha tuondoke kumbe likaja kwangu bahati mbaya. Ilibidi nicheke tuu maana kaniachia bonge la ngenya kichwani.
 
Siku hiyo nilichelewa kurudi nyumbani mida Kama ya tano hivi, usiku hapo kijijini kulikuwa na bonge la mti ambao ulikua katika njia ambayo ni maarufu Sana ila pale wazee wetu walikua wakitukataza Sana kupita hiyo njia ila sababu walikua hasemi ila ni msisitizo Sana hasa nyakati za usiku.

Basi bwana siku hiyo nmetoka zangu kwa washkaji kupiga stori kutokana na mda ilishaenda Sana nikaona kuzunguka ni mbali na huku tilishakatazwa kupita usiku hasa ukiwa alone

Nikaona poa mi mwanaume bhana potelea mbali liwalo na liwe nkavua yebo zangu na kuzishka mkononi safari ikaanza mwendo Kama wa mchaka mchaka baada ya kama nusu km hivi nakaribia jirani na ule mti mara ghafla naona macho makali yanang'aa Sana mbali kidogo na ule mti nkajikaza na kupita kwa mbali maana nakaribia home siwezi kurudi nlipotoka.

Ile namalizia tuu kuyapita ghafla hamadi dude hili hapa nyuma nilikimbia, sikuwahi kukimbia vile bahati nafika tuu homu namkuta mdogo wangu anafunga mlango huku Niko speed 260 ile naingia tuu, dogo kabamiza mlango pigwa Sana mikucha pale mlangoni tokea siku hiyo saa 12 jioni nipo ndani.

Mpaka leo sikuwahi na wala hatukuwahi kujua alikua ni mnyama gani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom