Tukutane hapa tuliowahi kufanya na kufanyiwa matukio ya Kikatili na kutisha maishani

....Unasamehewa kwa sababu tu ilikuwa bado mdogo!
Huu ndio unsfiki wetu waafrika ambao tunatakiwa kuupiga vita kwa nguvu zetu zote!
Umemsikia dhahiri shemeji yako na mama yake wanakusema na kukupangia ubaya wa kukufungia mlango ili wakunyime chakula alichonunua kaka yao, halafu Wewe ndio unasusa na kukimbilia kwenu hivi hivi?
Hapo Mimi ungenipenda Comrade.
Pamoja na Udogo wangu ningeliwatokea na kuwaambia nilichosikia na mipango yao dhalimu waliyopanga kunifanyia...na kaka ningemjulisha kilichotokea mbele yao na ndio ningeomba anipe nauli nirejee home nimuache na wajinga wake roho mbaya wale!!!
Sio rahisi hivyo. Unadhani kaka angekubali mdogo wake amdhalilishe mkwewe kimasikhara hivyo, kaka mwingine anakutia mibao na kukufukuza juu. Madam S alifanya vyema kuondoka kwa hekima tu maana ni kweli pale si kwake hana maamuzi nako. Ndugu akishaoa au kuolewa kwake wewe huna maamuzi ya chochote cha msingi ni kuwaacha tu maana ubaya huwa una mwisho wake
 
Mimi hii nilishawahi ileta humu. Siku moja niliwahi sana shule nikafika kabla mtu yeyote kufika. Likaja tu wazo nikajikuta nimeandika matusi ubaoni na kuchora nyuchi nikajaza ubao mzima na nilikuwa najifurahisha tu nilipanga niyafute. Nikasahau kuyafuta mpaka muda ukafika kukimbia mchakamchaka then parade. Kufupisha ni kwamba walimu shule nzima alikuwa anaingia darasani anatoka anatikisa kichwa huku sisi tukisubirishwa nje.

Wanafunzi wengine nao wanajiuliza kunanini kumbe mi najua. Ikabidi tuambiwe kuna mtu kaandika matusi na kuchora viungo vya kati inabidi tumtaje. Kwanza tukala tanotano afu tukapewa vikaratasi tumuandike kwa siri aloandika. Mimi sikutajwa sababu nilikuwa mpole balaa na class nilikuwa njema. Wakatajwa kwa wingi watu kama watatu hivi ambao ndio walikuaga wamepinda class. Ebwana walitembezewa fimbo hadi nikawa nimeinama nalia maana ilikua maticha wanachapa zamzam jamaa wanalia vibaya mno, fimbo zinakatikakatika unaletwa mzigo mwingine.

Aisee toka hapo nikawa kama na mfadhaiko flan nikikumbuka jamaa walivyochapwa. Na ile siri mpaka kesho sijawahi muambia mtu kama niliandikaga mimi yale matusi japo ni zaidi ya miaka 20 sasa.

🤣🤣🤣 Laana hiyo 🤣🤣🤣🤣
 
niliwahi kwenda kwa ndugu fulani hivi .

Tena nilifika usiku kama saa 4 na sio kwa kupenda japo kwa kulazimishwa

Mwenye hio nyumba ni kaundugu nae kwa mbali anadai mzee wangu alikuwa msaada mkubwa Sana kwake way back akkwa shule na chuo na hata kitaa akiwa hana kazi

Sasa nimekaeibishwa usiku maana nilikuta na huyo jamaa katika mazingira tatanishi

Yule jamaa akanibia dogo uwe unakuja hapa kila wikiendi kurefresh ukipata upenyo was huko shule na ukikwamba nicheki kwa simu nikasema poa .

Sasa mke wa yule jamaa hakunipa friendly welcome yaani kanuna muda nikiwa pale

Nilimsalimia hakuitikia

Nikasema tabu za nini wako watu wengi wanaweza Nipa tafu sikuwahi kanyaga ile nyumba Tena Wala kukutana na wale watu tena ni miaka 17 Sasa
 
Miaka 15 nyuma nikiwa na miaka 16 hivi nilifanya tukio ambalo limeniacha maombolezo yasiyo na namna na feel am guilt hadi leo am not comfortable, ingawa yaliisha ila moyoni mwangu hayajaisha bado naona kama jana tu ili tukio lilitokea.

Ilitokea kwenye gheto la brother tulipokuwa tunaishi nilimuingilia kwa nguvu msichana tuliyekuwa tunasoma nae form two darasa moja pia ni mdogo wa rafiki yangu sana, alifuata daftari zake pale nyumbani na bahati mbaya hapakuwa na mtu zaidi yangu siku hiyo ingawa mimi ndio niliazima hizo daftari ila alipozitaka nilimwambia nimesahau nyumbani ni kweli nilizisahau ila alipokuja ndio ghafla wazo la kishenzi likanijia kichwani.

Lengo halikuwa kumkatili yule binti wa watu, nilikuwa nalenga kumbembeleza ili akubali kile nilichokuwa nataka ila hakukubali na alitaka kuondoka haraka nikaona isiwe tabu nilitumia nguvu sana na nikamshinda na kufanya lile nililokuwa nataka kuja kutahamaki akili imenirudia damu nyingi zinamtoka mtoto wa watu hali ikawa sio hali tena kelele za kilio ziliwavuta majirani kuja kujua kuna nini ilikuwa aibu kubwa kwa upumbavu wangu mwenyewe, nilichoshukuru yule binti hakutamka kama nilimbaka kwa nguvu aliishia kulia sana sana sana ajabu mtaa mzima hadi kwao walimgeuzia kibao yule binti kwa kumuita malaya aliyekubuhu, imagine mimi ndie nimefanya tukio ila balaa likaanguka kwake alihamishwa pale kwao akaenda kuendelea na masomo mkoa mwingine kwa ndugu yake maana pale kitaa palichafuka.

Ajabu zaidi kaka yake baada ya kama mwezi alinifuata na kuniambia najua wewe hauna makosa ni umalaya wa mdogo wangu mimi nilikaaa kimya huku nahofu kubwa na kuniakikishia urafiki wetu hautakufa, aisee huku mimi moyoni nilikuwa na hofu kubwa sana nilikonda sana ndani ya mwezi nilipungua kilo 6 nilijaribu kumkwepa sana huyu rafiki yangu ili nisahau lile tukio maana kila nilipokuwa nikimuona nakumbuka lile tukio na confidence inapotea kabisa hadi leo hii huwa siku mojamoja ananipigia simu ingawa sasa kila mtu ana familia yake na maisha yake ila akipiga siku tu nakumbuka lile tukio nililofanya na jinsi jumba bovu lilipomdondokea yule mdogo wake.

Tatizo lingine sasa kila ninapoona habari ya matukio hasa ya ubakaji basi huwa jasho zinanitoka sana naishia kuzima tv kabisa au nabadili stesheni nyingine, mke wangu huwa anaulizaga sana mbona upo hivyo wewe nababaika kumjibu kwa hali hii nahisi kuna siku nitajikuta namwambia huu mkasa sijui itakuwaje..

Kuna siku nilimuona yule binti sasa na yeye ni mtu mzima tu mdada ila nilimkwepa sikupata ujasiri wa kumuangalia kabisa, nashukuru hakuniona ile siku sijui ingekuwaje.
Huyo binti hata sasa hivi akiamua kukupeleka jela anaweza
 
Mimi nilifichiwa chakula na shangazi yangu. Mwaka jana mtoto wa huyo shangazi ALINIOMBA NIMSAIDIE KUMPELEKA MAREKANI KUSOMA. Kweli usitende ubaya kwa mtu sababu ya kesho hauyajui. Full story hapa chini....

Nilikuwa nasoma Ilboru, mjomba (mdogo wake mama) na mke wake (shangazi) alihamishiwa kikazi Arusha tokea Dar, wakawa wanaishi Sanawari. Nilifurahi kupata ndugu wa karibu Arusha, tena Sanawari na Ilboru secondary ni karibu mno. Mama mzazi ndio alimsomesha huyo mjomba sekondari hadi chuo. Basi nikadhani nao watanijali. Uncle alikuwa mtu wa safari sana za kikazi, kwa hiyo mara nyingi mkewe ndio alikuwa home Arusha.

Mara mbili au tatu kwa mwezi (siku za Jumapili) nikawa naenda kuwasalimia. Mara za kwanza mambo yakawa sawa tu. Huwa wanakula vizuri sana, kwa hio nilikuwa nabadili diet vizuri sana.

Baada ya miezi miwili hivi kuisha tokea wahamie Arusha, mambo yakawa sio mambo. Nikienda kuwasalimia, huwa naenda mida ya saa nne, nakula lunch, halafu naondoka saa kumi hivi. Ikawa sasa naenda hadi naondoka hakuna msosi.

Hiyo ya kwenda na bila kupata msosi ilitokea kama mara tatu hivi. Mara ya nne sasa.. kitu hicho hicho.. nikakaa, hakuna kitu, njaa kweli yani hadi akili hafikirii vizuri kiasi cha mimi kusahau MADAFTARI YANGU hapo kwa uncle sababu nilikuwa naenda nayo kujisomea.

Basi kufika njiani nikakumbuka nimeyasahau hayo madaftari, nikarudi kwa uncle kuyachukua. Nikakuta WAMEJAZA MEZA CHAKULA WANAKULA. Hapo hata dakika 20 tokea niondoke hazikuisha. Manake chakula kilishapikwa zamani na walikificha.

Ilini-pain sana, lakini hio ni moja ya mambo yaliyonipa uchungu na maisha. Niliandika barua mbaya sana kwa uncle kumshitaki, ila ndugu wakasema nimekosea heshima. Ndugu nao wakamsapoti aunt.

Leo hii katika familia YOTE UNCLES NA AUNT, mimi ndio fogo kupita wote. Nimejenga sana, magari kibao, na pia nina projects zangu USA ambako nilikuja baada tu ya kumaliza form IV na ndio palinisaidia ku-win life. Na ndio hao walionitendea ukatili kama huo leo wananinyenyekea ili niwasaidie.
Wakaushie bro hii tabia ya kulipa wema kwa wakosefu itajenga jamii kosefu

Jamii inapaswa kuona mifano ya malipizi pia
 
Sitasahau wakati namaliza advance kuna maza wa mtaani aliniambia nimtafutie magodoro af mm atanipa cha juu kweli wakati tumeua pepa nkanunua magodoro nikawasiliana nae kma saa moja na nusu nkampelekea shule ipo kijijini kufika kwake kama nusu saa kumbe yule maza kashaandaa wahuni wakunimaliza yeye achukue magodoro nilipokaribia nkampgia cm tukaongea kumbe hakukata tulipomaliza kuongea naskia anawaambia atakuja kavaa koti na kofiii wewe mpge nondo akizimia tunamtupa mfereji wazeeee daaah nlipasuka moyo ndukiii kurudii nlipotoka xul
 
Sitasahau wakati namaliza advance kuna maza wa mtaani aliniambia nimtafutie magodoro af mm atanipa cha juu kweli wakati tumeua pepa nkanunua magodoro nikawasiliana nae kma saa moja na nusu nkampelekea shule ipo kijijini kufika kwake kama nusu saa kumbe yule maza kashaandaa wahuni wakunimaliza yeye achukue magodoro nilipokaribia nkampgia cm tukaongea kumbe hakukata tulipomaliza kuongea naskia anawaambia atakuja kavaa koti na kofiii wewe mpge nondo akizimia tunamtupa mfereji wazeeee daaah nlipasuka moyo ndukiii kurudii nlipotoka xul
Hio ilikua Mungu aisee alifanya yote hayo Mpaka hujafanyiwa kitu mbaya mm Kuna manzi enzi za sec tulipanga miadi Usiku kukutana Kumbe alipanga kunipora simu Kama Mungu vile Kuna sms ikaja inasema Akija tu mnamkwapua mnakimbia nkamuuliza hii sms ulikua unamtumia nani na amkwapue nani akabaki kujiuma uma
 
Sitasahau wakati namaliza advance kuna maza wa mtaani aliniambia nimtafutie magodoro af mm atanipa cha juu kweli wakati tumeua pepa nkanunua magodoro nikawasiliana nae kma saa moja na nusu nkampelekea shule ipo kijijini kufika kwake kama nusu saa kumbe yule maza kashaandaa wahuni wakunimaliza yeye achukue magodoro nilipokaribia nkampgia cm tukaongea kumbe hakukata tulipomaliza kuongea naskia anawaambia atakuja kavaa koti na kofiii wewe mpge nondo akizimia tunamtupa mfereji wazeeee daaah nlipasuka moyo ndukiii kurudii nlipotoka xul
Alikujuaje kwamba umevaa hivyo
 
Back
Top Bottom