Tukumbushane ya Dkt. Mwakyembe

Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
3,840
7,916
Anaitwa Harisson George Mwakyembe mzaliwa wa Mbeya mwaka 1955

Alihudumu kama mbunge wa Kyela mpaka pale Ally Jumbe alipompiga kumbo kinomanoma ktk kura za ndani ya chama

Lengo la kuandika ni baada ya kukumbuka baadhi ya matukio kumhusu huyu mwamba, alishiriki ktk tukio kubwa ambalo lilipelekea Waziri Mkuu kujiuzulu na baada ya hapo alipatwa na ugonjwa wa ajabu lkn kabla hajakaa sawa Waziri Mkuu aliyestaafu naye akapatwa na ugonjwa wa ajabu mpaka Leo hii wote hawa wawili hawapo sawa

Mengi yamesemwa kuhusu magonjwa ya hawa matembo wa siasa za bongo ikisemekana kuwa magonjwa yao yamesababishwa na visasi ingawaje hakuna kati yao aliyeliongelea hadharani

Msimu uliopita wa uchaguzi huyu mwamba aliangukia pua baada ya kushindwa vibaya ktk kura za ndani baada ya kushika nafasi ya tatu,wengi wetu tulitegemea anaweza pata zari km wengine jina likienda kwenye kamati za ngazi ya mkoa au taifa wanafanya mafekeche na kupindua meza kibabe lkn kwa huyu ilishindikana na ilikuwa kama mkosi.

Mwakye.PNG
 
Kuna siku alipata ajali, akatoka mzima na akanena"nilivyonusurika na niliyoyaona ni siri yangu" namshukuru Mungu. Ndio ligonjwa la ajabu likamjia kiaina, bado anapeta. Nampongeza mwamba Mwakiembe.
Huyu jamaa itakua poa sana akiandika kitabu kuhusu yaliyomtokea na aliyoyafanya tangu kuanza kwa utawala wa mkwere mpaka alipoondoka madarakan nadhan kipind hicho kwake kilikua na mambo mengi mno
 
Huyu jamaa ni moja ya wasomi wa hovyo kabisa walioamua kuweka matumbo yao mbele na elimu nyuma. Mpaka kuangushwa ubunge alikuwa ameshakuwa kituko mpaka watu wakadhani akili zake zimekuwa affected na ugonjwa alioumwa. Huyu na Lipumba (vu) ni aina moja.
Treni inayoenda Gongolamboto mpaka leo inaitwa treni ya mwakyembe baada ya kuifufua kwa jasho na damu.

Nyumbu wao ni kuponda tu.
 
Ajiajiri kama msemo wao
Hawawezi kuishi nje ya Mshahara hata uwape bilioni 26 kama mafao.
Kuna mmoja alipata bilioni 10 mafao na wizi alikaa miaka 5 baada ya kustaafu zilikwisha zote na kufa juu.
Alitumbua weee eti zimefika milioni 700 ndo anaenda kununua Mchele wa milioni 700 wakamchanganyia akapiga short mbaya.
Biashara ya Mchele ni biashara za watoto wanao jifunza ujasiliamali.level ya B inatakiwa ufanye investment na sio business.
 
Kura za maoni za ccm Kyela 2020 rushwa ya pikipiki za boxer ziligawiwa kwa kila Katibu kata kwenye zaidi ya kata 30 , Takukuru walipoingilia walinyamazishwa kutoka Lumumba
 
Hawawezi kuishi nje ya Mshahara hata uwape bilioni 26 kama mafao.
Kuna mmoja alipata bilioni 10 mafao na wizi alikaa miaka 5 baada ya kustaafu zilikwisha zote na kufa juu.
Alitumbua weee eti zimefika milioni 700 ndo anaenda kununua Mchele wa milioni 700 wakamchanganyia akapiga short mbaya.
Biashara ya Mchele ni biashara za watoto wanao jifunza ujasiliamali.level ya B inatakiwa ufanye investment na sio business.
Wamezoea kufungiwa mikanda kwenye magari
 
Back
Top Bottom