Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,685
Miaka ya 80's mwanzoni nilipata kuishi Tabora Mjini,baadae nikaja kusoma Tabora Boys miaka ya 90's....leo nimekumbuka maisha ya Tabora,Ujio wa Baba Mtakatifu,enzi za ukuu wa Mkoa Ndugu Gama....Timu ya mpira ya Milambo chini ya akina Job Ayoub "kwasakwasa",Quresh Ufunguo,Dadi Phares,Hamad Mwinyimkuu,Abas Mchemba na Bubu fulani alikuwa na mashuti sana wengine siwakumbuki.
Matajili wa wakati huo ni matajili wa mbao wakiitwa "Digala",kuna jamaa alikuwa tajili wa mbao mitaa ya Kiyungi karibu na Filter akiitwa Fifi(sijui kama yu hai)...mitaa ya ng'ambo mtaa wa Rehani alikuwepo Mavyombo, Msabaha...! Kulikuwa na kina Said Kindamba, Waarabu wa Kwihara na Mrema wa Cheyo!...
Miaka hiyo Tabora ilisifika kwa kuwa na Majambazi hatari, wengi wakitokea mitaa ya Ng'ambo..kuna jambazi mmoja walimkata mguu ili aache kuiba akawa anatembea na gongo(nimemsahau jina), Vichaa(wehu) wa kutosha na maarufu kama Athumani Nuna, Super Tall, Aman n.k...
Mitaa ya wajanja ilikuwa National na Cheyo!! Misosi kama ugali muhogo, makopa, mawese na ngazi... Vipi nani wa Tabora anipe update za leo?muda sijafika.
Chemichemi, Gongoni, Bachu, Kanyenye, Kiloleni, Isevya, K'koo, Mwanza Road na Ipuli.... Wapi vijana wa enzi hizo wa Mboka Manyema?