Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,227
- 157,421
Vituko Vya Marais: Kisa Cha Rais Mfupi Aliyeogopa Maswali Ya Wanahabari...!
Ndugu zangu,
Afrika yetu ina mambo. ” Ex Africa simper aliquid novi”. Maana yake: “Kila kukicha kitazuka kioja kingine Afrika. Alipata kutamka Ptolemy, mwanafalsafa wa Kiyunani.
Kuna kisa cha Rais wa Liberia aliyeitwa William Tubmann, huyu alitawala Liberia kutoka mwaka 1944 hadi 1964. Enzi hizo, alikuwa ni Rais ‘ Mzee wa Makamo’ kwenye ‘Nchi kijana’- Liberia.
Rais Tubmann alikuwa na vituko haswa. Moja ya vituko vyake ni pale alipokwenda kwa mara ya kwanza nchini Ethiopia kushiriki mkutano wa Umoja wa Mataifa ya Afrika (OAU). Ni mwaka 1963.
Rais Tubmann alikuwa ni mwoga sana wa kupanda ndege. Basi, akafunga safari ya meli kutoka Monrovia, Liberia kwenda Ethiopia. Safari ilimchukua mwezi mzima. Akatua Ethiopia akiwa amechoka na kuwakuta Marais wenzake wa Afrika wanamsubiri.
Na akawa kivutio kikubwa pia kwa wanahabari. Lakini, Rais Tubmann aliwaogopa sana wanahabari na maswali yao. Yasemekana, katika Urais wake hakuwahi kujibu swali lolote gumu la mwanahabari.
Pale Ethiopia, akarushiwa swali kuhusu hali ya siasa nchini mwake. Rais akaliogopa swali, na alikuwa na mbinu zake za kuyakwepa maswali.
Akiulizwa swali huchukua kiko chake na kuanza kuvuta. Na kinachotokea?
Kama pale Addis Ababa enzi hizo. Rais akalisikia swali, akachukua kiko chake huku wanahabari wakisubiri kwa hamu kubwa kusikia jibu la Rais. Naye akiwa amekaa kwenye kiti chake hotelini akavuta ‘ugolo’ wake kwenye kiko chake.
Kabla hajajibu swali, mara akaanza kupiga chafya mfululizo. Akapiga chafya weee, mpaka machozi yakaanza kumtoka. Kila mmoja akamwonea huruma. Na wengine wakaangua vicheko. Wasaidizi wa Rais wakawataka radhi wanahabari ili kumruhusu Mheshimiwa Rais akapumzike.
Rais Tubmann akawa ametoka mahali hapo bila kujibu swali hata moja!
Naam, Afrika Kuna Mambo!
Kwa hisani ya maggid