Tukumbushane riwaya za kusisimua

Vilivyosahaulika: UTUBORA MKULIMA, MAISHA YANGU NA BAADA YA MIAKA 50, KUFIKIRIKA, KUSADIKIKA, WASIFU WA SITI BINTI SAADI, MASOMO YENYE ADILI vya Shaaban Robert. NJOZI ILIYOPOTEA cha Mng'ong'o miaka ya sabini, PEPO YA MABWEGE cha Harrison Mwakyembe miaka ya themanini, BURIANI mwandishi kanitoka kidogo, MIRATHI YA HATARI,
 
Ikibidi Kufa Nife
Kikomo
Hadithi za Allan Quatermann
Alif Lela Ulela
Dunia Hadaa
Robinson Crusoe na Kisiwa Chake
Na ile riwaya tulikuwatunaisoma shule kwenye fasihi jina nimesahau ila kulikuwa na mtu anaitwa Bwana Mkubwa Lyanda wa jamhuri ya Unono!!

ooh my, yaani mmenikumbusha mbali sana. Nimesoma vitabu vingi sana na ilikuwa my main source of happiness. Kuvitaja itatake siku nzima labda nitaje baadhi au watunzi
John Msimbe Simon Simbamwene
Hammie Rajab
Fakhi S. Fakhi
Elvis Musiba
Ben R. Mtobwa
Kajubi D, Mukajanga
Zainabu Mwanga

na wahusika
Inpector Fog na Kachero Haji
Willy Gamba
Joram Kiango
Eddie Khaki
Dr. Motown
Kabwe Makanika n.k

Na hawa wandishi wako wapi, mbona hawatoi kazi? nadhani Ben Mtobwa is dead na najua Elvis mUSIBA ALIKUFA. WENGINE WAKO WAPI?

Where are the good old days nilipokuwa napiga misele kwenda kibanda pekee cha magazeti Bukoba Stand kuulizia ni kitabu gani kimetoka latest?

Hiv sasa kuna wandishi uchwara wanaotoa hadithi saba tofauti kwa wiki moja tu? huo sio uandishi...ni kuandika
 
Mkuu Rosa Mistika imeandikwa na Prof. E.Kezilahabi
Naomba nikumbushe kitabu kimoja kimeandikwa na Kezilahabi kina muhusika mkuu anaitwa Tumaini na theme yake nadhani inaingiliana na utaifishaji na siasa za ujamaa na kujitegemea, setting yake ni vijijini mwanzoni then mjini (Dar) I think. Katika kitabu hico kuna mtu anaitwa John, alitembea na mke wake Tumaini. Mwishono kama sikosei Tumaini alimpiga risasi kiongoz mmoja wa kisiasa akafungwa. Nakumbuka sentensi ya mwisho kabisa "akamfunika kitambaa cheusi usoni, Tumaini akastuka" Kinaitwaje na kinapatikana?
 
Jaman nisaidieni kuhusu riwaya ya zaka la damu na pepo ya mabwega. Zote za H. Mwakyembe naombeni maelezo yake kwa ufupi kwa aliezisoma.
 
Naomba nikumbushe kitabu kimoja kimeandikwa na Kezilahabi kina muhusika mkuu anaitwa Tumaini na theme yake nadhani inaingiliana na utaifishaji na siasa za ujamaa na kujitegemea, setting yake ni vijijini mwanzoni then mjini (Dar) I think. Katika kitabu hico kuna mtu anaitwa John, alitembea na mke wake Tumaini. Mwishono kama sikosei Tumaini alimpiga risasi kiongoz mmoja wa kisiasa akafungwa. Nakumbuka sentensi ya mwisho kabisa "akamfunika kitambaa cheusi usoni, Tumaini akastuka" Kinaitwaje na kinapatikana?
Hiki kitakuwa "Dunia Uwanja wa Fujo"
Kipo madukni. Nilikinunua posta mwaka jana kwa ajili ya maktaba yangu.
 
Aliyeonja pepo
kaptula la marx (kilifungiwa kwa kumkebehi Nyerere)
Chungu Tamu
Mzimu wa watu wa kale
Siri ya Sifuri
Nyota ya Rehema
Morani (Kinamuhusu Sokoine)
 
Duka liko posta hapo kwenye mzunguko wa sanamu ya bismin, jengo linalofuata baada ya benki ya posta kama unaenda Bills.
Ukiulizia hapo utaoneshwa.
 
Waandishi wa siku hizi hamna kitu hao ndiyo walikuwa waandishi bwana wa riwaya ujinga mtupu siku hizi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom