Tukumbushane habari njema hizi pia

BoyOfGod

JF-Expert Member
Jan 3, 2019
478
638
Mhubir12:1
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.

Salaam
Tunaishi, tunaondoka

Miaka 70,80,90,100 au chini ya hapo ndiyo maisha tuko nayo duniani na baada ya hapo Kuna trillions of years ya milele
👉Swali gumu la kujiuliza ukifa leo utakuwa wapi⁉️
Na unaandaaje kesho yako?

Bibilia inasema
Ufunuo wa Yohana 21:8 (KJV) Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Mbinguni kupo
Jehanum kupo
Kifo kipo
Sizungumzii dini au dhehebu fulani Mimi

Naongelea kuhusu imani yenye matendo sawa na vile Mungu anataka. Yakobo 2:26 Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Tugeuze macho yetu na Nia zetu tumgeukie Muumba dunia imefika mwisho kupita maelezo
Unahitaji vitu vifuatavyo
1.kumkubali Yesu
2.Kubatizwa kwa maji mengi
3.Kujazwa roho mtakatifu
4.Kuishi katika utakatifu na hofu ya Mungu

Otherwise if you think this is a joke, am so sorry for you
God bless you

Nakaribisha maswali Kama yapo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom