Tuko vitani: Msingi imara wa familia ya asili unashambuliwa kwa nguvu zote kutoka kila upande

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,848
20,697
Tuko vitani, msingi na uimara wa familia ya asili unashambuliwa kutoka kila upande. Angalia uharibifu uliopo: watu wachache leo wanaoa. Na wale wanao-oa, ndoa zinavunjika, watoto wadogo kabisa wa hata mwaka mmoja wanapekwa shule za bweni. Majukumu kwenye familia yamebadilika, kazi za baba sasa anafanya mama, na za mama anafanya baba. Uasherati sasa umekuwa kawaida. Ndoa za jinsia moja ziko sasa kisheria katika mataifa fulani fulani,na harakati zinafanyika ili ziwe jambo la kawaida. Ni wazi kabisa kwamba ndoa ipo kwenye kamba.

Kwa wastani sasa wanne kati ya watoto kumi duniani wanazaliwa nje ya ndoa. Uwezekano wa mtoto kukulia kwenye familia ya mzazi mmoja ni makubwa zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote. Watoto wanaishi kwenye vituo vya kulelea watoto au shule za bweni ambapo uasi na utovu wa nidhamu unavumiliwa au unahamasishwa. Uzinzi ni sehemu ya maisha. Picha za ngono ziko kila mahali.Mimba nje ya ndoa na magonjwa ya zinaa leo yako kila mahali. Mimba takribani ishirini millioni zinatolewa kila mwaka duniani.Familia inatoweka. Ndio,ipo vita kali katika familia, na vita hiyo haijawahi kuwa kali kama ilivyo sasa. Baada ya miaka mingi ya kushambuliwa na adui aliye mbaya kabisa,iliyokuwa familia imara kabisa,sasa inajikongoja kuendelea kuwepo.

Kama hutasimama imara kumkabili adui huyu, wewe na familia yako mtakuwa sehemu ya majeruhi. Umeshaathirika sana na adui kuliki unavyo-dhani. Ili uweze kufanikiwa katika mapambano haya hatari kabisa, unahitaji kuifahamu nguvu iliyoko nyuma ya vita hii na kwa nini vita hii ipo. Unahitaji pia kuelewa kwa nini vita ni kali sana.Unahitaji pia kujua mipango madhubuti ya mapambano katika vita hii.

FAMILIA MIGUU JUU KICHWA CHINI!
Leo ukengeufu wa jamii, familia zilizoharibika na sheria za ndoa zisizo-linda ndoa zimegeuza ndoa kuwa kituko na kichekesho. Watu sasa wanaona talaka kama kitu cha kawaida na kukubalika kabisa kimaadili katika harakati zao za kukwepa ndoa wanayo-ona haifai. Sio tu kwamba tumekubali tauni ya talaka, lakini wengi sasa wanaona talaka kama kitu kilicho halali katika mazingira mengi. Zile ndoa ambazo zinabaki bila kuvunjika nazo haziko salama, zina matatizo mengi: ngono isiyokidhi haja, matatizo ya kifedha, sintofahamu katika majukumu ya baba na mama, utovu wa nidhamu wa baba, mama, watoto nk.

Katika miaka ya zamani,familia ziliweka wazi majukumu ambayo baba na mama walipaswa kuyatekeleza.Majukumu ya baba na mama yaligawanywa kwa umakini makubwa, ili kuondosha mifarakano na ili kazi zifanyike vizuri.Kazi za mme na mke zilichangia katika maendeleo ya familia bila kuleta migongano. Mahusiano yote ya nje ya familia yalikuwa yanafanywa na mwanaume.Biashara na siasa pia zilikuwa shughuli za wanaume. Wanawake walikuwa hawategemewi kufanya kazi za nguvu kwa sababu ya maumbile yao.Hakuna familia iliyokuwa maskinu kiasi cha kukiuka sheria hii.

Ni kweli kwamba familia iliyokuwepo zamani ni ile ambayo Mungu aliikusudia iwepo tangu mwanzo. Katika kitabu cha Mwanzo sura ya pili,Mungu aliunda familia ya kwanza ya wanadamu kwa kuumba mwanaume kwanza halafu mwanamke kutoka kwenye ubavu wake. Katika mstari wa 18, alimuita mwanamke msaidizi. Ni vema watu wakaelewa kwamba ingawa mwanamke na mwanaume wameumbwa kufanya majukumu tofauti katika familia, majukumu yote umuhimu wao ni sawa.

Leo majukumu haya yamegeuzwa. Wanaume leo wameacha majukumu yao kwenye familia kama viongozi wa familia,watafutaji, walinzi na waelimishaji, tena kwa kuhamasishwa kufanya hivyo na vikundi, watu au mashirika yenye nia ovu ya kuisambaratisha familia.Wanawake na watoto wengi sasa hawaoni umuhimu wa baba ikilinganishwa na mama kwenye familia!

Mbaya zaidi, matamshi ya wanasiasa, wanaharakati, wanasaikolojia, mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs), tamthikia filamu nazo zinapigilia msumari kwamba mwanaume sio umuhimu zaidi ya Wanawake kwa ustawi wa familia na jamii!

Wanawake nao wameacha majukumu yao muhimu kwenye familia: kuwa msaidizi na mama mwenye upendo kwa mume wake na watoto. Katika miaka ya 1950 kwa wastani mmoja kati ya Wanawake wanne walio-olewa wenye miaka 44 waliajiriwa nje ya familia. Leo watatu kati ya wanne wameajiriwa nje ya familia! Wakati masaa ya mwanamke na mwanaume wanayofanya kazi yako sawa, kama yalivyokuwa miaka 50 iliyopita, masaa ya Wanawake wanayofanya kazi nje ya familia yamezidi mara tatu! Kuangalia watoto wakati baba yuko kazini sio tena jukumu muhimu la akina mama wengi. Matokeo yake ni kwamba watoto wengi wanaachwa wenyewe au kwenye mazingira hatarishi kimalezi: mazingira yasiyo na hofu ya Mungu kwenye vituo vya kulelea watoto, shule za bweni au hata wasichana wa manyumbani. Watoto wa namna hii wakiwa watu wazima na kuwa na familia zao wenyewe,hawawezi kabisa kulea familia zao inavyopasa au hata kuwa na familia imara.

Itaendelea...
 
Wakati nasoma nikahisi labda ni uzi wangu mwenyewe ila nilipoendelea kusoma nikaja gundua mleta mada ameoteshwa maono na fikra sawa na zangu na ameamua kuzileta hapa Jf.

Umeongea ukweli mzito sana. Huu ni ukweli ambao jamii wanaufumbia macho ila siku za baadae utakuja tugharimu sana kupita maelezo na tutataka kurejea hapa tulipo ila haitawezekana.....
 
"......... tutataka kurejea hapa tulipo ila haitawezekana!" Ni maneno mazito sana,lakini yanayowezekana kabisa.Inauma sana.
 
Mkuuu you nailed it. Yani mkuu achaaa mimi ni mzazi mwenye msimamo na kwa upande mwingine naona najitahidi kama mama ila kwa dunia ya leo bila Mungu, kulea na kuishi na kufuata misingi bora ya kifamilia itakua kazi.

Tumshirikishe Mungu kwa kila jambo, kina mama wenzangu kila siku ikibidi kila saa tuziombee familia zetu watoto na waume zetu. Shetani yupo kazini na anaharibu familia maana ndo mzizi wa yote. Mungu atusaidie sana
 
Tuko vitani, msingi na uimara wa familia ya asili unashambuliwa kutoka kila upande. Angalia uharibifu uliopo: watu wachache leo wanaoa. Na wale wanao-oa, ndoa zinavunjika, watoto wadogo kabisa wa hata mwaka mmoja wanapekwa shule za bweni. Majukumu kwenye familia yamebadilika, kazi za baba sasa anafanya mama, na za mama anafanya baba. Uasherati sasa umekuwa kawaida. Ndoa za jinsia moja ziko sasa kisheria katika mataifa fulani fulani,na harakati zinafanyika ili ziwe jambo la kawaida. Ni wazi kabisa kwamba ndoa ipo kwenye kamba.

Kwa wastani sasa wanne kati ya watoto kumi duniani wanazaliwa nje ya ndoa. Uwezekano wa mtoto kukulia kwenye familia ya mzazi mmoja ni makubwa zaidi sasa kuliko wakati mwingine wowote. Watoto wanaishi kwenye vituo vya kulelea watoto au shule za bweni ambapo uasi na utovu wa nidhamu unavumiliwa au unahamasishwa. Uzinzi ni sehemu ya maisha. Picha za ngono ziko kila mahali.Mimba nje ya ndoa na magonjwa ya zinaa leo yako kila mahali. Mimba takribani ishirini millioni zinatolewa kila mwaka duniani.Familia inatoweka. Ndio,ipo vita kali katika familia, na vita hiyo haijawahi kuwa kali kama ilivyo sasa. Baada ya miaka mingi ya kushambuliwa na adui aliye mbaya kabisa,iliyokuwa familia imara kabisa,sasa inajikongoja kuendelea kuwepo.

Kama hutasimama imara kumkabili adui huyu, wewe na familia yako mtakuwa sehemu ya majeruhi. Umeshaathirika sana na adui kuliki unavyo-dhani. Ili uweze kufanikiwa katika mapambano haya hatari kabisa, unahitaji kuifahamu nguvu iliyoko nyuma ya vita hii na kwa nini vita hii ipo. Unahitaji pia kuelewa kwa nini vita ni kali sana.Unahitaji pia kujua mipango madhubuti ya mapambano katika vita hii.

FAMILIA MIGUU JUU KICHWA CHINI!
Leo ukengeufu wa jamii, familia zilizoharibika na sheria za ndoa zisizo-linda ndoa zimegeuza ndoa kuwa kituko na kichekesho. Watu sasa wanaona talaka kama kitu cha kawaida na kukubalika kabisa kimaadili katika harakati zao za kukwepa ndoa wanayo-ona haifai. Sio tu kwamba tumekubali tauni ya talaka, lakini wengi sasa wanaona talaka kama kitu kilicho halali katika mazingira mengi. Zile ndoa ambazo zinabaki bila kuvunjika nazo haziko salama, zina matatizo mengi: ngono isiyokidhi haja, matatizo ya kifedha, sintofahamu katika majukumu ya baba na mama, utovu wa nidhamu wa baba, mama, watoto nk.

Katika miaka ya zamani,familia ziliweka wazi majukumu ambayo baba na mama walipaswa kuyatekeleza.Majukumu ya baba na mama yaligawanywa kwa umakini makubwa, ili kuondosha mifarakano na ili kazi zifanyike vizuri.Kazi za mme na mke zilichangia katika maendeleo ya familia bila kuleta migongano. Mahusiano yote ya nje ya familia yalikuwa yanafanywa na mwanaume.Biashara na siasa pia zilikuwa shughuli za wanaume. Wanawake walikuwa hawategemewi kufanya kazi za nguvu kwa sababu ya maumbile yao.Hakuna familia iliyokuwa maskinu kiasi cha kukiuka sheria hii.

Ni kweli kwamba familia iliyokuwepo zamani ni ile ambayo Mungu aliikusudia iwepo tangu mwanzo. Katika kitabu cha Mwanzo sura ya pili,Mungu aliunda familia ya kwanza ya wanadamu kwa kuumba mwanaume kwanza halafu mwanamke kutoka kwenye ubavu wake. Katika mstari wa 18, alimuita mwanamke msaidizi. Ni vema watu wakaelewa kwamba ingawa mwanamke na mwanaume wameumbwa kufanya majukumu tofauti katika familia, majukumu yote umuhimu wao ni sawa.

Leo majukumu haya yamegeuzwa. Wanaume leo wameacha majukumu yao kwenye familia kama viongozi wa familia,watafutaji, walinzi na waelimishaji, tena kwa kuhamasishwa kufanya hivyo na vikundi, watu au mashirika yenye nia ovu ya kuisambaratisha familia.Wanawake na watoto wengi sasa hawaoni umuhimu wa baba ikilinganishwa na mama kwenye familia!

Mbaya zaidi, matamshi ya wanasiasa, wanaharakati, wanasaikolojia, mashirika yasiyo ya kiserikali(NGOs), tamthikia filamu nazo zinapigilia msumari kwamba mwanaume sio umuhimu zaidi ya Wanawake kwa ustawi wa familia na jamii!

Wanawake nao wameacha majukumu yao muhimu kwenye familia: kuwa msaidizi na mama mwenye upendo kwa mume wake na watoto. Katika miaka ya 1950 kwa wastani mmoja kati ya Wanawake wanne walio-olewa wenye miaka 44 waliajiriwa nje ya familia. Leo watatu kati ya wanne wameajiriwa nje ya familia! Wakati masaa ya mwanamke na mwanaume wanayofanya kazi yako sawa, kama yalivyokuwa miaka 50 iliyopita, masaa ya Wanawake wanayofanya kazi nje ya familia yamezidi mara tatu! Kuangalia watoto wakati baba yuko kazini sio tena jukumu muhimu la akina mama wengi. Matokeo yake ni kwamba watoto wengi wanaachwa wenyewe au kwenye mazingira hatarishi kimalezi: mazingira yasiyo na hofu ya Mungu kwenye vituo vya kulelea watoto, shule za bweni au hata wasichana wa manyumbani. Watoto wa namna hii wakiwa watu wazima na kuwa na familia zao wenyewe,hawawezi kabisa kulea familia zao inavyopasa au hata kuwa na familia imara.

Itaendelea...
100% True.
 
Mkuuu you nailed it. Yani mkuu achaaa mimi ni mzazi mwenye msimamo na kwa upande mwingine naona najitahidi kama mama ila kwa dunia ya leo bila Mungu, kulea na kuishi na kufuata misingi bora ya kifamilia itakua kazi. Tumshirikishe Mungu kwa kila jambo, kina mama wenzangu kila siku ikibidi kila saa tuziombee familia zetu watoto na waume zetu. Shetani yupo kazini na anaharibu familia maana ndo mzizi wa yote. Mungu atusaidie sana
Uko sahihi kabisa Dada yangu.Katika swala hili wa kutusaidia ni Mungu tu peke yake.Infact umeni preempt, nitaelekea huko Mungu akinipa kibali.The force directed to the family by Lucifer is too huge.Hatuwezi kushinda bila Mungu.
 
Back
Top Bottom