Tukizeeka tutaishi vipi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukizeeka tutaishi vipi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kisanduku, Nov 1, 2011.

 1. K

  Kisanduku Member

  #1
  Nov 1, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ni kwamba tunaishi kwa kubahatisha bila kujua hatima yetu itakuwaje huko mbeleni.

  Ninachojua nchi nyingi Ulaya na America, wao kwa kulijua tatizo hili basi wazee wanapofika umri wa kutojiweza wanawekwa kwenye quarters zao na huko kuna wangalizi maalum.

  Hapa kwetu hakuna hilo. Ukimuuliza mzee akiishiwa nguvu kila mmoja ana jibu lake mwenyewe.

  Kuna majibu kwamba watoto watakutunza. Lakini huko sasa hivi ni kubahatisha kwani huyo mtoto huna hakika atakuwa katika hali gani au nafasi gani katka dunia hii. Na anaweza akafa vilevile. Pia wategemezi wa hali hii inabidi sasa ukizeeka unyenyekee sana hao watoto ata kama unanyimwa stahili zako, maana wanaktunza.

  Mimi nadhani tunajidanganya kutoliona hili kama ni tatizo. Leo tunachemka, tunabinyeza keyboard lakini ukweli ni kwamba tutazeeka na tutaishiwa nguvu. Je, tutaishije kipindi hicho.

  Nimetoka majuzi kumtembelea shangazi yangu. Utotoni pale kwa shangazi kulijaa watu wa kila aina na kulichangamka kwa shughuli mbalimbali. Leo nimeguswa kuona shangazi yuko peke yake na anamuuguza mume wake kama vile hana watoto wakati ana watoto wanne wakubwa na kila mmoja anasema yuko bise na familia yake!

  Shangazi anasema walitumia akili sana kujenga nyumba ambayo wameweza kuweka wapangaji ambao binafsi niliona wanamsaidia kumuuguza yule mume wa shangazi! Bila hivyo basi ina maana shangazi angekaa bila kupangisha basi angekuwa anauguza mwenyewe.

  Wakati mnaleta maoni yenu, mimi wazo langu ni kwamba tujipange kuleta system kama ya Ulaya niliyosema. Walioko Ulaya watueleze inafanya kazi kwa kiasi gani. Kama ni kukatwa hela ili zitumike kukutunza uzeeni basi ni heri hizi pensheni ziwe zinalenga huko.

  Bila kufikiri hivyo, basi ukweli ni kwamba kizazi cha wazee wa sasa hivi kina nafuu lakini kizazi chetu na uchumi mbovu kila waka sijui hali itakuwaje.

  Nawasilisha.
   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Kisanduku,fainali uzeeni.Ukiwa kijana unakuwa na nguvu za kufanya lolote unalotaka,ila uzeeni kama hukujipanga wakati una nguvu ndo unaipata fresh.In comparison bora mama zetu kuliko baba zetu maana watoto wengi huwa na tendency ya kuwa na soft heart kwa mama zao kuliko baba zao na hivyo watoto wanawaangalia zaidi kuliko baba.Ujanani baba utahangaika kusomesha na hata kutoa mtaji wa biashara kwa watoto lakini akili yao itakuwa kumtunza zaidi mama.Ushauri wangu ni kuwa wakati bado tuna nguvu tujipange kwa ajili ya uzee ambao tutakuwa hatutegemei serikali wala watoto.Unaweza kununua vipande UTT,hisa,bonds au kuwa na nyumba za kupangisha.
   
 3. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ujana maji ya moto!!! wengi wanajisahau!!
   
 4. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ujanani ndio wakati wa kulima, kupanda na kupalilia mazao,then uzeen ni mavuno,so uzeen utavuna ulichopanda ujanani!
   
 5. Mmasi

  Mmasi Senior Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mi naona twende vijjni.
   
 6. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Sasa hivi watu, hasa vijana, wanakimbia vijijini kwa kasi kubwa. Ndiyo sababu ya ongezeko la watu mijini (urbanization). Miaka ishirini ijayo watu wengi watakuwa mijini kuliko vijijini. Ongeza mchakato wa sasa kwa ardhi kupokonywa na hao wanaoitwa 'wawekezaji', huko vijijini hapatakuwa pa kukimbilia tena. Mimi binafsi tayari ninalo tatizo hilo kwa sababu huko kijijini amebaki mama yangu ambaye ni mzee. Watoto wangu wote wamezaliwa mjini, wako vyuoni na sitegemei kuwa watarudi kijijini. Sijui hatma ya kaya yangu mimi mwenyewe nikizeeka au kufa. Kuhusu mipango ya uzeeni tayari vyombo vipo. Ni kujua namna ya kuvitumia: Mifuko ya pensheni, uwekezaji katika hisa, uwekezaji katika majumba, bima, n.k. Tunapaswa kuanzisha na vingine kama mutual funds au collective investment schemes. Tatizo ni kwamba hatujui namna ya kuvitumia au hatuna imani navyo.
   
 7. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,374
  Likes Received: 3,204
  Trophy Points: 280
  Kwa mfanyakazi atakuwa na pensheni, hofu ni kwa wakulima na wasiokuwa na ajira rasmi au zenye uhakika
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,089
  Likes Received: 6,555
  Trophy Points: 280
  nitarudi,
  nawahi daladala.
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Ni jambo ambalo kama mambo mengi muhimu nchini limeachiwa liende kienyeji hakuna juhudi maalum za wahusika kuliangalia na ndio maana tunayashuhudi ya Tanzaznia legion na ya wataafu wa iliyokuwa EAC.

  Ni kweli kizazi cha vijana wa sasa kitakuw an wakati mgumu sana hapo baadae!Mie pia naliunga wazo la kurudi sisi tulionanguvu tukashiriane na wenzetu kule vijijini kwa kuwekeza huko
   
Loading...