Tukiongelea Katiba Mpya!

katokumbi

Senior Member
May 19, 2012
195
77
KWAMBA, Katiba ya Tanganyika itawezaje
kutengenezwa ndani ya mwaka mmoja (1) mara
baada ya Katiba ya Shirikisho itakayoainisha uwepo
wa serikali tatu (3) kupitishwa 26 Aprili, 2014 halafu
tuingie kwenye uchaguzi 2015 na Katiba zote tatu?


NA KWAMBA, Wabunge wawili Jimbo moja, ni nani
atawajibika kwa nani kwa maslahi ya nani na kwa
eneo gani? Je, tusipoona utekelezaji wa Ilani
tutamuuliza Mbunge yupi? Vipi kama wabunge
wakiwa wa vyama tofauti? Watashirikiana vipi?


NA KWAMBA, bado kuna minong'ono ya Zanzibar
kutaka usawa wa mgawanyo wa rasilimali kwenye
mambo ya Muungano. Zanzibar kwa mujibu wa
Sensa ya watu na makazi ya 2012 wako 1, 303, 568
na TZ Bara (Tanganyika) 43,625,434. Wakati huo
huo Mkoa wa Dar es Salaam ukiwa na watu Million 4.36, ukifuatiwa na Mikoa ya Mwanza watu
2,772,509, Mbeya watu 2,707,410, na Mkoa wa
Kagera watu 2,458, 023. Kwa uwiano huu wa watu,
ni usawa upi Zanzibar inahitaji zaidi ya usawa
uliooneshwa kwenye Rasmu ya Katiba? Mfano
wabunge 50 watoke Tanganyika na 20 Zanzibar na Watano (5) wa kuteuliwa?

Tujadili kwa hoja Tafadhali....
 
Back
Top Bottom