Tukio usilolisahau ukiwa Primary School

Tukio usilolisahau ukiwa Primary School

zile mishe za kuwahi namba asubuhi kuna siku ilikua zamu ya ticha mnoko balaa..
nliamka saa kumi na moja kwenda shule kufika karibu na kimto fulani hivi kulikua na kundi la mbwa kama tisa hivi walikua wanagegedana aisee kuniona wakajua nimekuja kuwala chabo wakaanza kunifukuza aisee ile siku ndo niliamini nina mbio zaidi ya usain bolt
 
Nakumbuka nilipata demu nikiwa darasa la sita 1998 baada ya kumchomolea kumtajia jibu kwa mtihani, eti ananiuliza "hauchi hauchi..... ) nikamchomolea asije nipita marks. Basi tokea siku hiyo akawa demu wangu.
 
Mwalimu Selina naoma uendelee kunisamehe... ulikuwa utoto tu. Tabia yako ya kufundisha ukiwa umekaa kwenye kiti ndio ilinifanya nikafanya vile... Japo nilikula mboko za kutosha lakini bado nakuomba uendelee kunisamehe... Dah!!
 
Huwaga nasema, kunamazingira mengine watu tumekulia hayakuwa na adventure za kitoto kabisa, kwa hiyo tunaona kama kuna kitu tulikosa pitia kabisa, mtu unasoma day school kuanzia kindergarten mpaka university, mtu hujawahi mwagilia maua shule na kudeki darasa au hata kufuta vumbi meza yako darasani, kuchapwa au hata kurudishwa nyumbani kwa makosa yoyote.
 
Mi nakumbuka kuanzia darasa la kwanza hadi la nne sikuwa navaa viatu. Sasa wakati wa kiangazi muda wa saa nane parade mchanga ulikuwa unaniunguza nyayo kinooma. Nilijikuta napiga makitamu bila kuambiwa.
 
Nakumbuka nikiwa darasa la tano hivi kuna siku mimi na rafiki yangu tukiwa darasani tulikuwa tunapeana zamu ya kumkumbatia kimahaba mdada mmoja ambaye pia alikuwa ni mwanafunzi mwenzetu..tulifanya vile kwa muda mrefu mara nikiwa ktk harakati za kumchezea yule mdada nikafumaniwa na madam wa kiswahili...daah ilikuwa bonge la msala ...kweli sitosahau....karibun wadau

Darasa la pili mmoja wa walimu wetu alikuwa na tatizo la kifafa. Kwa wanafunzi kulikuwa na imani kuwa mtu wa kifafa akianguka na akajamba, ukivuta hewa ya ushuzi ule kifafa kimekupata!!!

Bahati mbaya mwalimu siku hiyo kifafa kimemshika akiwa darasani kwetu; ile kadondoka tuu....SCRAMBLE ya kutokea madirishani kukwepa kupumua hewa ya ushuzi wake hadi leo sintakaa niisahau🙂
 
Nakumbuka wakati nasoma shule ya msingi mandu nyakato Mwanza. Mapumziko tukaenda kucheza mpira, jamaa mmoja alikuwa anasoma darasa la nne nikampiga chenga kama tatu hivi na kanzu juu, baada ya mechi alinifuata nakuanza kunipiga ngumi nyingi sana mpaka bukta ya shule akachanika! Niliamua kukimbia kwenda nyumbani jioni nikaenda kuangalia picha ya tazani na wanyama. Kesho nikaenda shule Yule jamaa wakati tuko mapumziko akataka kunipiga tena, nilichofanya nikampiga kabali fasta kama nilivyo angalia kwenye picha ya tazani hakuchomoa mpaka walimu wakaitwa kusaidia Kumtoa, kalegea na anatoka damu puani. Nikawa shujaa niliye jihami mapema nikaogopwa shule nzima kwa kukaba kabali.
 
Back
Top Bottom