Tukio la Mwita Waitara limedhihirisha kifo cha Intelijensia baada ya Ujio wa Edward Lowassa na genge lake

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,975
Ninadhani hakuna kitengo kilidhoofika sana kwa sasa ndani ya CHADEMA zaidi ya kitengo cha Ulinzi na Usalama.

Kitengo cha Ulinzi na Usalama kilichokuwa kinaongozwa na Wilfred Lwakatare ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bukoba Mjini kabla ya ujio wa Edward Lowassa na genge lake kilikuwa proactive katika kugundua hujuma kabla hazijafanyika na kuhakikisha unakuwepo usalama ndani ya CHADEMA.

Ninakumbuka hata Mzee Slaa aliwahi kusema waliweza kuzijua hujuma na siri nyingi kwa sababu baadhi ya watu na waajiriwa wa taasisi ya usalama wa Taifa walikuwa wanawaamini na kuwapa siri mbali mbali.

Baada ya ujio wa Lowassa baadhi ya watu nadhani waliamini kuwa Ulinzi na Usalama ndani ya CHADEMA ungeimarika zaidi hasa baada ya Mtaalam wa masuala ya Ulinzi na Usalama ajulikanaye kwa jina la Matson chizi ambaye ni rafiki wa karibu wa Lowassa kujiunga pia CHADEMA akitokea CCM.

Kilichotokea ni kinyume kwa sasa ambapo hoja hii imesadifiwa hasa baada ya Wilfred Lwakatare kuondoka katika nafasi hiyo ya Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama. CHADEMA ya sasa ni dhoofu na reactive kwenye masuala ya hujuma, ulinzi na Usalama.

Katiba ya CHADEMA Toleo la 2016 katika Ibara ya 7.7.5 inasema, ‘’Kutakuwa na mfumo wa ulinzi na usalama wa mali, viongozi na maslahi ya chama utakaotambulika kama Brigedi Nyekundu (Red Brigade)’’. Majukumu ya msingi ya Brigedi Nyekundu (Red Brigade) ni kujishughulisha na usalama ndani ya chama kwa maana ya kulinda viongozi wa chama na idara mbalimbali, mali za chama na rasilimali za chama. Pia kulinda maslahi ya chama ili kisije kuhujumiwa.

Tukio la Mbunge Mwita Waitara kujiunga na CCM ambalo limewafanya viongozi wa juu wa CHADEMA na wanazi wao kupigwa butwaa limeendelea kudhihirisha CHADEMA ya sasa imedhoofika sana katika kitengo cha Ulinzi na Usalama. CHADEMA ya sasa haijui hata kinachoendelea ndani na nje ya chama.

Baada ya Mbunge Waitara kujivua uanachama wa CHADEMA niliwaona viongozi wa CHADEMA Dar es Salaam wakiita waandishi wa habari na kusema CHADEMA ilikuwa mbioni kumfukuza uanachama kwa sababu hata barua ya kumuonya walikuwa wamemwandikia na kilichokuwa kimebaki ni kumfukuza wakati wowote. Ukiwangalia kwa makini kwa kutumia body language utagundua kuwa walichokuwa wanakiongea sicho.

Kinachochekesha zaidi, of all people, eti Dk. Milton Makongoro Mahanga ndio alijitokeza kama msemaji wa CHADEMA na kudai kuwa Mwita Waitara alikuwa mzigo ndani ya CHADEMA na kwa sababu walikuwa mbioni kumfukuza. Mahanga ambaye alikuwa mzigo mzito ndani ya CCM kwa sasa anaweza kusimama kwa ruhusa ya CHADEMA na kusema watu kama Waitara eti ni mizigo! Hii ndio CHADEMA MPYA!

Tukio la Mwita Waitara linanifanya nikumbuke maneno ya Mzee Slaa alipowauliza viongozi wa CHADEMA, ‘’Lowassa anakuja kama mtaji au mzigo, yaani kwa lugha ya kiingeza ni asset au liability’’?

Kwa hali jinsi ilivyo ndani ya CHADEMA, Mbunge Waitara hatakuwa wa mwisho kujivua uanachama bila kitengo cha Ulinzi na Usalama kuwa na taarifa mapema.
 
Last edited:
Wenzako wanaamka na sala we asubuhi yote hii wewe unaamka na majungu
Unaonyesha hukupata hata fursa ya kujifunza somo la Jiografia! Kama huwezi kujua kuwa katika dunia hii binadamu wote hawalali kwa wakati mmoja au hujui kuwa kuna sehemu nyingine kwa sasa ni mchana au usiku utaweza vipi kuchambua mada zinazohitaji fikra pana?

Kajifunze kwanza somo la Jiografia!
 
Unaonyesha hukupata hata fursa ya kujifunza somo la Jiografia! Kama huwezi kujua kuwa katika dunia hii binadamu wote hawalali kwa wakati mmoja au hujui kuwa kuna sehemu nyingine kwa sasa ni mchana au usiku utaweza vipi kuchambua mada zinazohitaji fikra pana?

Kajifunze kwanza somo la Jiografia!

Kuna watu wa aina 3 katika utambuzi:-(1) Kuna watu hawajuii kuwa hawajui hao achana nao (wapotezee) maana wanakupoteea muda wako.(2)Kuna watu wanajua hawajui hao wasaidie siku zote(3) Kuna watu wanajua na wanajua kuwa wanajua hao ngozana nao. Huyu achana naye.
 
Kuna watu wa aina 3 katika utambuzi:-(1) Kuna watu hawajuii kuwa hawajui hao achana nao (wapotezee) maana wanakupoteea muda wako.(2)Kuna watu wanajua hawajui hao wasaidie siku zote(3) Kuna watu wanajua na wanajua kuwa wanajua hao ngozana nao. Huyu achana naye.

Mkuu.
Ninashukuru sana kwa ushauri wako mzuri.
 
Lakini bado siamini katika mabadiliko ya CCM, kuhama ama kufa kwa chadema ni maumivu zaidi kwa watanzania,siku hizi serikali ya ccm ikifanya ufisadi,hakuna wa kuikosoa,ukipinga unaonekana juha,mi sipendezwi na kushangilia kifo cha upinzani nchini japo ndo hivyo upinzani nao umechanganyikiwa wala hawajui wafanye nini
MUDA UTATUHUKUMU WENYEWE
 
Unaonyesha hukupata hata fursa ya kujifunza somo la Jiografia! Kama huwezi kujua kuwa katika dunia hii binadamu wote hawalali kwa wakati mmoja au hujui kuwa kuna sehemu nyingine kwa sasa ni mchana au usiku utaweza vipi kuchambua mada zinazohitaji fikra pana?

Kajifunze kwanza somo la Jiografia!
hahahahaa kumbe Lumumba SAA hii ni mchana wacha tukajifunze jiografy
 
Lakini bado siamini katika mabadiliko ya CCM, kuhama ama kufa kwa chadema ni maumivu zaidi kwa watanzania,siku hizi serikali ya ccm ikifanya ufisadi,hakuna wa kuikosoa,ukipinga unaonekana *.**.*,mi sipendezwi na kushangilia kifo cha upinzani nchini japo ndo hivyo upinzani nao umechanganyikiwa wala hawajui wafanye nini
MUDA UTATUHUKUMU WENYEWE
Kichwa kinauma
 
Back
Top Bottom