Tukio la majambazi kupora fedha Ubungo Mataa

mboamboa

JF-Expert Member
Jan 30, 2013
237
156
Habari nilizozipata sasa hivi ni kwamba kuna tukio la ujambazi limefanyika Ubungo Mataa muda huu na inasemekana kuwa majambazi hayo yalikuwa na Pikipiki Boxer wakavamia gari aina ya Landcruiser wakalipiga risasi ambayo ilimjeruhi mhusika kisha kufungua mlango wa hiyo gari na wakachukua begi na kutimka nalo kwa kutumia pikipiki kupitia njia ya Ubungo Maziwa,habari hizo zinasema kuwa mpaka muda huu aliyeporwa anasaidiwa na wasamaria wema huku akibubujikwa na damu ili hali traffic Polisi wako kwenye mataa wakiongoza magari
 
Kama la mwake ule, sijui ilikuwa NBC?
Kazi ipo, pole kwa mjeruhiwa
 
Kama la mwake ule, sijui ilikuwa NBC?
Kazi ipo, pole kwa mjeruhiwa

Inaelekea hii ni 'copycat' ya lile tukio la mwaka 2007 (?)
Polisi kazi yao kupandishana vyeo tu na kuwasambaratisha raia wasio na hatia wakifanya mikutano yao halali, suala la ulinzi na usalama wa raia ni sifuri...
Askari polisi wa usalama wa barabarani walikuwepo wanaongoza magari na majambazi wameweza kujeruhi, kupora fedha na kukimbia.
Pole sana kwa mjeruhiwa, Mwenyezi Mungu Ampe nguvu ya uponyaji!!!
 
Lazima utakuwa mchongo huo. Wamejuaje kuna hela

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
pumbavu hao wacha afe wanashindwa kutoa hela kidogo kwaajili ya escort.. trafic endelea kuongoza magari watu wafike salama. tumechoka kusikia hizi habari kila siku kwa style moja.
 
Hili tukio lazima litakuwa lilipangwa...pole kwa majeruhi
 
Du! Majambazi yamepamba moto tuwe makini kubeba pesa nyingi bila ulinzi ni hatari.

Mchongo wa benki huu.
Kwa anaejua muusika ametoka kudraw benki gani na tawi lipi aseme tuifanyie kazi...
 
Mamilion yote hayo eti m2 anashndwa kutoa hata elf 20 ya escort kisa ubahili usokuwa na maana,kwnn asiibiwe!!!
 
Hii kitu naona sasa imeanza kurudi tena kwa kasi ya kutisha. Mwema anakusanya hela ya kustaafia nini? Hivi ni kwanini haya matukio huwa yanaachwa hadi yasbabishe madhara makubwa ndipo mamlaka huska zianze kuchukua hatua?
 
Inaelekea hii ni 'copycat' ya lile tukio la mwaka 2007 (?)
Polisi kazi yao kupandishana vyeo tu na kuwasambaratisha raia wasio na hatia wakifanya mikutano yao halali, suala la ulinzi na usalama wa raia ni sifuri...
Askari polisi wa usalama wa barabarani walikuwepo wanaongoza magari na majambazi wameweza kujeruhi, kupora fedha na kukimbia.
Pole sana kwa mjeruhiwa, Mwenyezi Mungu Ampe nguvu ya uponyaji!!!

tumia akil traffic wangefanyaje wakiwa mikono mitupu? Akil yako imejaa ushabic wakisiasa hata kwenye manbo ya msingi, think BIG kama hauwez jchomoe jf haufai
 
Back
Top Bottom