Maduka ya fedha Dar hatarini kwa ujambazi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa wanne kwa unyang’anyi wa kutumia silaha na kuwataka mawakala wa huduma za kifedha kuchukua tahadhari za kiusalama dhidi ya uhalifu ulioibuka mwanzoni mwa mwaka huu.

Ushauri huo umetolewa baada ya jeshi hilo kuwakamata watuhumiwa hao ambao wamevamia sehemu za kutoa na kuweka fedha na kupora maeneo ya Madale, Kariakoo, Kunduchi Mtongani, Vikindu, Keko na Goba.

Akizungumza na Mwananchi jana, mtaalamu wa masuala ya usalama, Emmanuel Mkondya alisema kama ilivyo kwa benki, biashara hiyo inapaswa kufanyika kwa kuzingatia misingi ya usalama ili kujiondoa kwenye hatari.

“Wengi hawazingatii suala la ulinzi na usalama, utakuta mtu anafanya mzunguko mkubwa wa miamala lakini hana ulinzi wowote, katika hili nashauri kuepuka kukutana uso kwa uso na wateja na hili linafanyika kwa kuweka madirisha yenye nondo.

“Kuna wale ofisi zao zipo kama maduka kabisa basi ni vyema wakaweka vioo ambavyo haviruhusu risasi, pia ni muhimu kuweka biashara katika eneo ambalo ni rahisi kupata msaada endapo tukio litatokea,” alisema.

Pia, Mkondya alisema ni muhimu kuweka kamera za CCTV na ‘punnic button’ (kitufe kinachounganishwa na kampuni ya ulinzi ambacho ukikibonyeza kinatoa taarifa kwa kampuni husika na eneo la tukio, kisha kinatoa alarm) ambazo gharama yake si kubwa ikilinganishwa na hatari inayoweza kutokea kwa kufanya biashara ya miamala ya fedha bila kuzingatia ulinzi.

Katika mitandao ya kijamii kumesambaa vipande vya video zilizotolewa kwenye CCTV kamera zinazoonyesha wahalifu hao wenye silaha wakiwa wamevamia duka na kuwaamrisha watu kulala chini wakitaka wapewe fedha.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea eneo la Goba Kulangwa, hata hivyo wahalifu hao hawakufanikiwa kutimiza lengo lao kutokana na wahusika kuwa na mafunzo yaliyowawezesha kuomba msaada wa haraka.

Mmiliki wa eneo hilo la biashara ya miamala ya fedha, Fortunatus Luhemeja alikiri tukio la uvamizi kutokea kwenye biashara yake jioni ya Januari 7 mwaka huu baada ya wahalifu hao kuvamia na kutoa maelekezo ya kupatiwa fedha.

“Walipovamia walikuwa wanalazimisha wafunguliwe mlango ili waingie sehemu yenye fedha, kwa bahati nzuri wale wafanyakazi wetu walikuwa na mafunzo, hivyo hawakutekeleza maelekezo waliyopewa na wahalifu hao, badala yake wakabonyeza kitufe cha kutoa taarifa ya hali ya hatari ambacho kilipiga kelele na kuwavuruga wale majambazi.

Baada ya kuona vile, mmoja wao akafyatua risasi na kusababisha purukushani kwa muda lakini walipogundua wameshindwa kutimiza azma yao wakaondoka. Wakati tukio linaendelea wafanyakazi wetu wakatupa taarifa na sisi tukaripoti polisi,” alisema Luhemeja.

“Tunashukuru polisi walitupa msaada wa haraka na tuliwapa kila aina ya ushirikiano ikiwamo picha za video zilizoonyesha tukio zima tangu wanaingia, mmoja wao alitangulia kufanya muamala.” Muathirika mwingine wa uhalifu wa kundi hilo ni Josephat Simamatosombi ambaye ni mfanyabiashara katika eneo la Kunduchi Mtongani ambaye alivamiwa jioni ya Januari 5 mwaka huu.

“Walikuja wakanivamia na kutaka niwaonyeshe fedha zilipo, nilikuwa mbishi wakanipiga na kitako cha bunduki wakachukua Sh3 milioni na kuondoka zao,” alisema Simamatosombi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema Agosti 8 mwaka huu saa 6:30 mchana eneo la Mabibo External, polisi waliwakamata wahalifu hao waliokuwa wamekutana kupanga na kujiandaa kufanya uhalifu.

Kamanda Muliro alisema watuhumiwa hao walipobaini kuzingirwa na askari, mmoja wao alitoa bastola yake na kupiga risasi kuwashambulia askari ambao walijihami na kufanikiwa kuwakamata.

Alisema ukamataji huo ulitokana na taarifa fiche (za siri) ya kuwepo kwa kundi hilo la kihalifu lililoonekana kuanza kufanya matukio mbalimbali ya uhalifu wa kutumia silaha kuanzia Januari 1 hadi 7 mwaka huu.

Alisema katika mahojiano ya awali na watuhumiwa hao ilibainika miongoni mwao waliwahi kukamatwa na kukaa kwenye mahabusu za Keko kwa tuhuma za mauaji na unyang’anyi na walitoka mwaka 2017 na mmoja wao akakimbilia nchi jirani kisha kurejea nchini mwishoni mwa mwaka jana.

MWANANCHI
 
Nchi yenu watu wa mchambawima msiojua hata kung’amua mambo madogo?
Hatuijui si mtuwachie nchi yetu. Wacha karma iwatese kama mlivyotufanyia na nyinyi yamewageukia , hata bado . Lilianza Jiwe subirini kidogo litakuja jabali 😝😝
 
Sikuongezwa mshahara miaka sita, sikupandishwa daraja kwa miaka sita na sikulipwa pesa za likizo kwa wakati.
Magufoool alikuwa mshamba sana.
Mshamba ni ww ambae hukiweza kuzipiga pesa kipindi chake. Hata awamu hii kuna kipi ulipata kama sio unafiki tatizo mnafanya kazi bila connection kipindi cha magu watu walipata stahiki zao tena zile nono kabisa ww mshamba unalalamika hujalipwa 😂😂😂😂😂
 
Hatuijui si mtuwachie nchi yetu. Wacha karma iwatese kama mlivyotufanyia na nyinyi yamewageukia , hata bado . Lilianza Jiwe subirini kidogo litakuja jabali 😝😝
Tuwazimie umeme mkae kizani?
Kwani huyo jiwe hakuwatesa nyie mliufyata kimya hata huyo gavana wenu alikaa kimya
 
Tuwazimie umeme mkae kizani?
Kwani huyo jiwe hakuwatesa nyie mliufyata kimya hata huyo gavana wenu alikaa kimya
Mbona unazimwa mara nyingi tu. Kwani tulipokuwa huru tulitegemea kitu kutoka Tanganyika?
 
Back
Top Bottom