Antar bin Shaddad
JF-Expert Member
- Oct 11, 2010
- 202
- 102
Leo arusha kumetokea tukio la kusikitisha sana:Gari la wagonjwa (ambulance) la hospitali ya Selian inayomilikiwa na kanisa la KKKT lilikuwa linampeleka mgonjwa moja aitwaye Hamad Salim Bawazir (familia maarufu arusha) kwenda hospitali ya KCMC ya mjini Moshi baada ya mgonjwa huyo kuzidiwa sana.Mgonjwza huyo alikuwa anatumia hewa ya oksijen kutokana na matatizo ya kupumua na ndani ya gari hilo kulikuwa na mashine iliyokuwa na hewa hiyo.
Katika hali ya kushangaza gari lilipofika eneo la Kikatiti wakati wanaelekea KCMC nesi aliyeambatana na ndugu wa mgonjwa aliwatangazia kuwa oksijen imeisha hivyo inabidi warudi arusha, na mgonjwa alifariki ndani ya dakika 10.
Hapo ikazuka sokomoko la kufa mtu kati ya ndugu wa mgonjwa na mwuguzi huyo pamoja na dereva ambapo paqmoja na kuchezea kichapo ndugu waliharibu gari hilo kwa kuvunja vioo vyote.
Pia jamaa na marafiki wa familia kutoka mitaa ya katikati ya mji wa Arusha kama Bondeni na pangani waliokuwa na hasira kutokana na kitendo hicho walivamia hospitali ya Selian wakitaka kuichoma moto hadi uongozi ulipolazimika kuwaita askari wa kutuliza ghasia.
Taarifa zinadai kuwa huyo ni mgonjwa pili kuishiwa oksijen njiani na tukio kama hilo lilitokea hivi karibuni ambapo mgonjwa moja alifia eneo la Philips ndani ya gari hilo hilo.
Hospitali ya Selian pamoja na kujengwa kwa gharama kuwa sana zaidi ya shilingi bilioni 10 imeshindwa kutoa huduma yenye viwango kwa wagonjwa na imekuwa kama machinjio ya wagonjwa kutokana na uzembe wa madaktari na wauguzi na pia kukosekana kwa menejimenti ya maana.