Tukimaliza kutumbua majipu tunaelekea wapi?

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,491
2,355
Hili ni swali ambalo nimejiuliza sana ila sijawahi kupata majibu "TUKIMALIZA KUTUMBUA MAJIPU TUNAELEKEA WAPI?"

Siku za nyuma kidogo mh. alipoanza kutumbua majipu ilikuwa mchakamchaka kweli maana kila aliyekuwa na kacheo serikalini aliikuwa akiimba hii chorus huku akizunguka huku na kule. Wakati wa kuimba hii chorus kila kiongozi alieelekeza nguvu zote huko kama vile ndio hitaji pekee la nchi na kila mtu alikuwa anachukua kagenge ka waandishi wa habari kwenda kutumbua tena kutumbua wale wa saizi yake. Baada ya hii chorus kuisha utamu sioni tena harakati za namna ile ni kama vile wanasubiri kupewa maagizo mengine wakati huu bwana mkubwa anapomaliziamalizia haka kachorus.

Hali hii naifananisha na parade ya jeshi ni kama vile kiongozi wa parade katoa amri ya mguu pande halafu akaondoka huku akiwaacha wanajeshi hawajui la kufanya wanasubiri arudi aje kusema mguu sawa, wote kulia tawanyika
 
jipu vs jipu ni kazi sana yani jipu lilitumbue jipu.
kwanza hiyo kazi hawawezi kuimaliza leo hii wala kesho kwasababu majipu mengine yamekaa sehemu mbaya sana wala hayana hata dalili ya kuiva.
 
H
jipu vs jipu ni kazi sana yani jipu lilitumbue jipu.
kwanza hiyo kazi hawawezi kuimaliza leo hii wala kesho kwasababu majipu mengine yamekaa sehemu mbaya sana wala hayana hata dalili ya kuiva.
hayo ndio kipimo cha kumaanisha
 
Tutawapa hao wagonjwa wa majipu discharge warudi home kujiunga tena na wenzao
 
Back
Top Bottom