Tukate mizizi ya nidhamu ya woga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tukate mizizi ya nidhamu ya woga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zing, Jul 1, 2009.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kuna hili tatizo ambalo tukiliangalia na kulitatua ndani ya jamii yetu mabadiliko ya ya maendeleo ya kweli yanawezekana. Tatizo hili ni NIDHAMU YA WOGA


  • wengi tumeezaliwa na kulelewa kwenye mazigira ambayo mtoto kwa mzazi hatakiwi kubisha, ni hatukupewa nafasi ya kuchangia

  • Shuleni kuanzia, chekechea primary secondary na hata vyuoni uhusiano kati ya mwalimu/mkufunzi na mwanfunzi ni kama paka na panya.kama mwanafuzi tulijengewa uoga na kuwaogopa walimu

  • matatizo haya yanakuja mapka mtu anapopata kazi ofisini. Nidhamu ya woga imeota mizizi mtu unaogopa kumkosoa bosi ingawa unajua kabisa wazo au ushauri wako ni mzuri. Hivyo hivyo mabosi wengine anajiona kukosolewa au wazo lake kupingw ana mtu wa chini yake ni kujidharirisha.

  • Hata kwenye ndoa kuna mke na mume wanaogopana ogopana kiasi kila mtu anaweza kutoka kuvinjari nje sababu anahisi kuna mambo akimwambia mkewe au mumewe basi atamuona muhuni. matokea yake ndo nyumba ndogo kwa wanaume na vidumu kwa wanawake
  Kuuukata huu mnyororo inabidi inabidi watoto wapaya ( ie wanaozaliwa miaka hii ) wafundishwe kujiamini na kuelezea mawazo na hisia zao wazi wazi na toak wakiwa na umri mdogo.mabadiliko yatakuja kwa wazazi kubadilika, walimu kubadilika na viongozi kubadilika juu ya mtazamo walionao kwa watu wa chini.


  Tujifunze Kukubali kutokubaliana na tujue kila mmoja wetu ana mchango muhimu
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Tatizo hili limetufanya wengi kuishi kwa unafiki nafiki. Nafikiri imefika mahali sasa badala ya kuwa na nidhamu ya woga kila sehemu, tujifunze kukubali au kukataa kwa hoja na heshima bila kuonyesha dharau, ili tujenge jamii yenye kujua nini inataka. Ilivyo sasa hata kupandishwa cheo kazini ni lazima ufanye alignment fulani na wakuu na kukubali hata yale unayoyakataa. Hili halina mustakabali mzuri kwetu as individuals na Taifa letu. Unafiki unatu cost sana maana matatizo mengi ya ukubwa huu tunaouona yametokea kwasababu wengine hawakuyakubali, ila nidhamu ya uoga ndio iliyopelekea kuyapa support bila kujua athari zake nini.
   
 3. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tukiondoa nidhamu ya woga ndio tutaokoa nchi hii na kuwatimua mafisadi Papa.
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 720
  Trophy Points: 280
  nidham ya woga mbaya sana,
  last time ndo nataka kuondoka huko nyumbani kuna jamaa yangu nilimaliza nae chuo. jamaa alikuwa mwoga hata kupeleka application letter mahali.
  na hii nidhamu ya woga inatufanya tuwe na mawazo tegemzi sana maana huwezi kusimama wewe kama wewe,
  akionekana mtu ana mawazo tofauti au hata akihoji jambo flani ikiwa haliendi sawa utaona wenzie wanamshangaa na kumwambia '''wewe unajiamini vipi kusema hivi'''
  safari bado ndefu sana
   
Loading...