Wasalaam wana MMU...
Mimi ni MUPYA humu, lakini sio mgeni! Sijui hata kama hiyo ina make sense lakini ndo hivyo. Nasema sio mgeni kwasababu nimekua nikija humu kwa lengo la kujifunza kutoka kwenu toka nilipojiunga September. Katika pitapita zangu nimegundua mengiiii...vile vile baadhi wa members wamekua common machoni mwangu, so nimeshazizoea hizo usernamez zao.
Yeah yeah...najua tayari wapo walioanza kusema hii sio sehemu ya kutuandikia mambo yako binafsi moyoni mwao sahivi...but c'mon, I know! Just bear with me.
I'm on my early 20s kwahiyo wanaonizidi humu ni wengi tu lakini najitahidi hii post isichore mduara kwa watu wa rika fulani tu.
Nataka kuitumia ile 'U' ya kwenye 'MMU' tuongee kama marafiki kwenye hili suala zima la kumuhukumu mtu usiyejuana nae. Naongelea kumuhukumu mtu kwa kumsema kutokana na neno au tendo alilolifanya (i mean giving your opinion the hard way, to be more specific).
Unajua mimi, wewe na yule tumekulia na kulelewa katika mazingira tofauti tofauti. Tumejikuta tukiwa na tabia pamoja na maana za maneno kama 'kitu cha ajabu' na 'kitu cha kawaida' tofauti tofauti. Hivyo basi kutokana na hiyo misingi tumejikuta tukijengeka na kuwa watu wa aina flani kitabia. Sasa akitokea mtu (a stranger) akafanya au kusema kitu cha ajabu kwako mkiwa kwenye mkusanyiko fulani halafu wewe ukaamua kumjia juu hapo hapo bila kujali kuwa yeye kapitia yapi hadi kufika hapo alipo ni sawa??
-Au tuwe tunawafumbia macho tu kwasababu hatujui lolote kuhusu mambo waliopitia??
-Au tuwe tunawajia taratibu kwa kuwa sio kosa lao kukosa malezi uliyopata wewe??
-Je, "Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na Ulimwengu" na uwezo wa kila mwanadamu wa kawaida kutambua jema na baya vinatupa haki ya kuwanyoosha papo hapo wavukao mipaka from our point of view??
*Ningetoa mfano lakini nimehisi ntachukua muda wako mwingi hapa. Nadhani hicho kimetosha kukujengea picha ya ninachokiongelea na naamini mifano tunayo vichwani mwetu as tumeshakutana nayo.
Tujuzane maoni yako juu ya hilo...