Tujuzane njia ya kupokea pesa kwa Paypal Tanzania

Aisee... Kwahiyo mpaka Leo wabongo hatuwezi kupiga kazi online kutoka mataifa mbalimbali duniani.
 
Kama kuna namna yoyote tujuzane wakuu ikipatikana aisee.... pia link za online jobs,per hours jobs ,tupatiane wakuu.
 
Kwasababu inakuwa ngumu kupokea pesa PayPal. Je unaweza kutumia detail za ndugu yako ambaye ni raia wa Kenya na kutumia line ya safaricom yenye usajili wake. Yaani ukasajili kwa data zake mpaka jina unatumia lake. Italeta shida kwa njia hiyo.
Maana ukijisajili ukiwa wako huko mbele hela zinazuiwa na unaambiwa tuma detail zako za vitambulisho wahakiki kama kweli mkenya. Si heri umtumie mzaliwa wa huko huko.
 
Limit ya Kenyan paypal kuhold pesa ni $2000 kwa mwaka...! Bado hata wakihold huwa tuna chomokaga tu... Hakuna mkate mgumu mbele ya chai.. Me nina US paypal account ulisha wahi kuholdiwa na $600 na nikachomoa tu.. Waliomba documents nikawagea (Najua mie nlizipata wapi )

Sent using Jamii Forums mobile app
Pale unapo pokea ujumbe kutoka PayPal kama account yako ipo full verified
Screenshot_2021-03-31-17-33-26-22.jpg
 
Tanzania nchi yetu bado changa sana! itabidi nitafute wajuzi wa mambo tufungue kampuni itakayotuwezesha kutoa pesa kupitia Paypal na mitandao mingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesikia ukiwa na laini ya safaricom ya Kenya uka-link m-pesa ya Kenya kwenye PayPal baadae una-withdraw na kuhamishia kwenye vodacom m-pesa ya tanzania ni masaa mawili tu unashika noti zako mkononi
 
Naandika hii thread nikiwa na masikitiko na machungu juu ya nchi yetu kutoruhusu kupokea pesa kwa platform maarufu duniani ya PAYPAL.

Nimekosa mchongo kibao kwenye mitandao inayolipa kwa mfumo wa PayPal, mitandao kama fiverr na quora partnership ni miongoni ya mitandao ambayo pesa zinatupita hivi hivi watz tunaoziweza kazi zao ila hatuwezi kupokea pesa, INASIKITISHA SANA.

Kuna kipindi nilipiga $400 ndani ya siku 3 tu mitandao flani, ila nilivyofahamishwa wapo strict kutoa pesa kwa PayPal tu, mzuka uliisha hapohapo nikaacha kazi na kuziacha dola nazichungulia tu, ponea yangu hizo dola nilitoa baada ya miezi 8 ya vuta nikuvute kuwabembeleza wenye kampuni wanilipe kwa western union.

Wenzetu Kenya wako mbele sana, PayPal inatumika kwao na vijana wa Kenya kwenye skills zao wapo fiverr, pia online internet marketers wa Kenya wanapata fursa kibao za kujiunga na mitandao kadha na kadha kwa sababu ya urahisi na uhakika wa malipo kupitia PayPal.

Wakuu, katika kizazi hiki ambacho teknolojia inakua kwa kasi basi hata michongo mingi hupatikana online ili kujipatia pesa lakini hiki kitendawili cha PayPal kuruhusiwa tz mpaka Leo hakijateguliwa, kitu kinachotuumiza wengi.

TUJUZANE NJIA ZA KUWEZA KUPOKEA FEDHA PAYPAL UKIWA TZ, IWE DIRECT AMA INDIRECT
Pole mkuu kwa changamoto inayo kumba nchi yetu ya Tanzania...
 
Hilo ni tatizo jamani Mimi Nina $800 huko online za matangazo ya online radio yangu street One radio ila kuzipata shida
 
Naomba kuuliza, hiyo line 6a Safaricom ukishajiunga, ukiwa Tanzania itasoma? Na kama utajiunta na Mpesa ya Kenya, tuseme umejiunga kwa App yao, ukiwa Tanzania inakuwaje kwa line kuwa nje ya simu?
 
Naomba kuuliza, hiyo line 6a Safaricom ukishajiunga, ukiwa Tanzania itasoma? Na kama utajiunta na Mpesa ya Kenya, tuseme umejiunga kwa App yao, ukiwa Tanzania inakuwaje kwa line kuwa nje ya simu?
Nyingi ni za magumash maana zinasajiliwa Kwa detail za watu Wa Kenya!!
Pindi ukitakiwa uthibitishe Kama ni zako ndio utajua hujui .
Labda uende boarder na pass yako usajili kihalali
 
Hilo ni tatizo jamani Mimi Nina $800 huko online za matangazo ya online radio yangu street One radio ila kuzipata shida
Bongo bahati mbaya. Kuishi Tanzania kunahitaji uvumilivu sana wa hali ya juu kwasababu kuna wakati mwingine unapatwa na hasira sana unapoangalia fursa mtandaoni halafu payment method ni paypal
 
Back
Top Bottom