Tujuzane namna ya kutinda nyusi na kupaka wanja

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Wakuu habari,

Ukweli ni kwamba kutinda nyusi na kupaka wanja kwenye nyusi imekuwa ni urembo kwa wadada siku hizi, mimi pia napenda kutinda nyusi na kupaka wanja mwemyewe ila siwezi.

Nimekuwa nikienda salon kutindwa ila mara nyingine nakuwa bize na kazi hivyo nahitaji kujifunza.

Mkiweka na picha itakuwa vizuri.

Karibuni mtujuze.
 
Ninanyusi kama kichaka sina mpango wa kutinda nasubiri harusi yangu wafanye yote hayo
 
  • Thanks
Reactions: waj
Zamani nilikua natinda ila sikuhizi sipendi nyusi zimekuwa nyingi ndo nazipenda.
 
Mie natinda saloon kwa uzi i think hiyo afadhali na inakaa muda mrefu..... Kupaka wanja siku hizi si kuna vile vidude vya kulinganisha.. (nimesahau jina) ni mkombozi kiaina.
 
Ar siku hizi ni kwa Zahor kutindwa na kupaka wanja wa piko 3000 tu inakaa wk 1 au mbili ama kutinda kwa uzi ndio napenda
 
Back
Top Bottom