Tujuzane changamoto za Google Map Driving na namna ya kuzitatua

Kremme

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
471
Reaction score
496
Habri za asubuhi Wakuu

Tupeane changamoto za driving maeneo tusiyoyajua kupitia google map driving hasa Dar, baadhi za kwangu ni hizi
  1. Kulazimishwa kupitia barabara wanayoamua wao. Kuna siku nilikuwa naelekea maeneo ya CRDB Mwenge kutokea Shekilango Morogoro road, yule mdada wa Google Map ananilazimisha niende kwanza Mwenge via Sam Nujoma afu ndo nirudi na Shekilango road nifike CRDB Mwenge.
  2. Changamoto za Majina ya barabara( hili ukiwa mgeni utaumia). Kuna siku nilitoka Mliman City nielekee Picolo hotel. Nikapita Coca cola road nikaunga na Mwai Kibaki road from no where Road ile ikaitwa Old Bagamoyo road nafika round about naambiwa niingie Mwai Kibaki road ambayo actual niliijoin toka coca cola road.
  3. Kukiwa na foleni hii Google driving Inachanganyikiwa.
Kiujumla mbali na Changamoto ni msaada sana hasa kwa sisi wa UBER na wageni kwa Dar.

20191201_073413.jpeg
 
Nafikiri wewe ndio hujui. Google map zinawaongoza wageni ambao ndio mara ya kwanza kuingia mji huo na unahitaji kufika mlimani city kwa hiyo google map ipo kwa ajili yao na inawaonyesha barabara salama sasa wewe barabara michepuko unazijua na mji unaujua ya nini gooogle map huo ni ushamba
 
Bonge moja la App. Linanisaidia sana kujua Foreni huu mji. Nikiona njia nyekundu nabadirisha uelekeo au nasikilizia kidogo.
 
Nafikiri wewe ndio hujui. Google map zinawaongoza wageni ambao ndio mara ya kwanza kuingia mji huo na unahitaji kufika mlimani city kwa hiyo google map ipo kwa ajili yao na inawaonyesha barabara salama sasa wewe barabara michepuko unazijua na mji unaujua ya nini gooogle map huo ni ushamba
usiseme ushamba,sema huo ni uzee.
 
Kuna siku hiyo app ilinipitisha barabara ya ajabu wakati ipo nzuri kabisa kwa mbele tu
Google map wanakupitisha njia fupi kuliko zote. Suala la ubora wa barabara hilo sidhani kama linawahusu sana by the way ni gumu barabara inatengenezwa leo then in 3 yrs imechakaa. Kwa ujumla, mimi naitumia sana google map kwenye miji ambayo ni mgeni na mara zote haijaniangusha. I love it. Teknolojia yoyote inazo changamoto but so far inafanya vizuri sana
 
Hili limetukuta wengi, Aisee sitakaa nije kusahau. Nlifika sehem hakuna njia afu yenyewe inaonyesha kuna bonge ya barabara
Watanzania kwa kulalamika hatujambo. Nadhani hata tunapokosa kitu cha kulalamika huwa tunalalamika kwa nini tumekosa kitu cha kulalamika. Jamaa kaniacha hoi aliposema eti ''yule mdada wa Google map akaniambia.....'' Kwa hamjui ile ni software na inafanya kazi kwa kutumia location na siyo kila mara location yako inakuwa accurate? Sasa mtu sehemu unaijua na barabara unazijua Google map ya nini? Ndiyo imeingia Bongo kwa mara ya kwanza au basi tu wengi walikuwa hawajui?
 
Hakuna njia au njia ilikuwa imekatika? Binafsi imenikuta mara moja tu, nilikuta sehemu njia imekatika, nadhani na maji ya mvua. Hii hata bila kutumia google map inaweza kukukuta kama njia hujaipita muda mrefu. Kwa ujumla imenisaidia sana Jijini Nairobi, Arusha Dar na maeneo mengine mengi.
 
Nafikiri wewe ndio hujui. Google map zinawaongoza wageni ambao ndio mara ya kwanza kuingia mji huo na unahitaji kufika mlimani city kwa hiyo google map ipo kwa ajili yao na inawaonyesha barabara salama sasa wewe barabara michepuko unazijua na mji unaujua ya nini gooogle map huo ni ushamba
Google map haiko kwa ajili yetu sisi tusio na mitaa na barabara zenye majina ya kudumu. Kuna nyumba moja ili mwenye nyumba afike kwake imemlazimu ajenge flaiova juu ya jirani yake! Fuatilia kipindi cha uswazi utaona vituko vya jiji la Dar. Ukienda Mbagala wote lazima mpite Mtonimtongani, Misheni na Kokoto kwenda Kongowe, sasa ukitoka barabara kuu hakuna mitaa yenye majina hivyo Google map haifanyikazi.
 
Watanzania kwa kulalamika hatujambo. Nadhani hata tunapokosa kitu cha kulalamika huwa tunalalamika kwa nini tumekosa kitu cha kulalamika. Jamaa kaniacha hoi aliposema eti ''yule mdada wa Google map akaniambia.....'' Kwa hamjui ile ni software na inafanya kazi kwa kutumia location na siyo kila mara location yako inakuwa accurate? Sasa mtu sehemu unaijua na barabara unazijua Google map ya nini? Ndiyo imeingia Bongo kwa mara ya kwanza au basi tu wengi walikuwa hawajui?
Mkuu kuna sehem nimelalamika au nimesema nlikua najua napoelekea.?
..
 
Watanzania kwa kulalamika hatujambo. Nadhani hata tunapokosa kitu cha kulalamika huwa tunalalamika kwa nini tumekosa kitu cha kulalamika. Jamaa kaniacha hoi aliposema eti ''yule mdada wa Google map akaniambia.....'' Kwa hamjui ile ni software na inafanya kazi kwa kutumia location na siyo kila mara location yako inakuwa accurate? Sasa mtu sehemu unaijua na barabara unazijua Google map ya nini? Ndiyo imeingia Bongo kwa mara ya kwanza au basi tu wengi walikuwa hawajui?
Na asiyeijua afanyeje, enzi za kuuliza mitaa zimepitwa na wakati ukiwa na simujanja.
 
Bado sijaona mapungufu ya Google Map kila nilipo itumia other wise labda ujichanganye mwenyewe. Bado kuna asilimia kubwa ya wa Tz hawajui jinsi ya kutumia Google map. So lazima useme inachangamoto.

Sasa wewe unatumia gari then unafuata maelekezo ya kutembea kwa miguu au kinyune chake kwanini usiingie chaka.

Network mwendo wakobe lazima ikupe wrong info au info sahihi zije kwa kuchelewa.

Inakupa option za barabara zaidi ya moja uchaguzi ni wako. Na sio lazima uilazimishe kukuelekeza kuanzia eneo ulipo madhara yake itakupa njia ndefu au yenye mzunguko.
Chagua eneo specific ikuelekeze kuanzia hilo eneo. Nk
 
Kremme,
Change view mkuu weka satellite view, waweza baini hata majengo nk
Kuliko map view.
 
Hakuna njia au njia ilikuwa imekatika? Binafsi imenikuta mara moja tu, nilikuta sehemu njia imekatika, nadhani na maji ya mvua. Hii hata bila kutumia google map inaweza kukukuta kama njia hujaipita muda mrefu. Kwa ujumla imenisaidia sana Jijini Nairobi, Arusha Dar na maeneo mengine mengi.
Itakua reserve ya tanesco high tension lines au pipe za tazama
 
Kremme,

Hapo una uwezo wa kuchagua njia mojawapo kati ya hizo 3 ya kwenda, ni uhamuzi wako kuchagua njia ipi ambayo unataka kuitumia.
 
Bado sijaona mapungufu ya Google Map kila nilipo itumia other wise labda ujichanganye mwenyewe. Bado kuna asilimia kubwa ya wa Tz hawajui jinsi ya kutumia Google map. So lazima useme inachangamoto.

Sasa wewe unatumia gari then unafuata maelekezo ya kutembea kwa miguu au kinyune chake kwanini usiingie chaka.

Network mwendo wakobe lazima ikupe wrong info au info sahihi zije kwa kuchekewa.

Inakupa option za barabara zaidi ya moja uchaguzi ni wako. Na sio lazima uilazimishe kukuelekeza kuanzia eneo ulipo madhara yake itakupa njia ndefu au yenye mzunguko.
Chagua eneo specific ikuelekeze kuanzia hilo eneo. Nk
Fact
 
Back
Top Bottom