Tujikuumbushe nyimbo ya mwambao za kitambo

Tujikuumbushe nyimbo ya mwambao za kitambo

wadau huu uzi maalumu kwa wapenzi wote wa nyimbo za mwambao za kuanzia mwaka 2000 kurudi nyuma hadi 1918 nimemkumbuka sana asu misambano,bi shakila,bi malika,mushrooms wazee wa embe dodo, , , tukumbushe nyimbo na waimbaje wake wadau wengine wapate kutokwa na machozi wakikumbuka enzi hizo za Y2K manjonjo
 
gere.....cjui unaitwa hivyo,cmjui aloimba
na daktari wa wananjenje

'laambwa lambwa file
maharage yako jikoni nishayapika
nangojea sukari ya bwana haijafika'

pale pa kachiri kachiri kama ulikuwa hutak ata kujitikisa utajitikisa bila kupenda,km huna nyonga utatikisa ata tako,waso na tako tulitikisa mifupa.
MUHOGO

JEE UNAUKUBALI?
 
Mwenye wimbo wa wagosi wa kaya NYETI atume humu jamn maana nauelewa sana hasa maudhui yake...
Ingawa si wimbo wa mwambao kama ilivyoainishwa hapo juu..
 
mwenye nyimbo ya sabal kheri mpenzi iliyorudiwa na marehemu Nasma khamis kidogo akishirikiana na (mwanaume simkumbuki jina)naiomba tafadhari
 
Mwenye wimbo wa wagosi wa kaya NYETI atume humu jamn maana nauelewa sana hasa maudhui yake...
Ingawa si wimbo wa mwambao kama ilivyoainishwa hapo juu..
Aisee niliwahi usikia siku moja kwenye daladala nikaupenda sijawahi usikia tena
 
mwenye nyimbo ya sabal kheri mpenzi iliyorudiwa na marehemu Nasma khamis kidogo akishirikiana na (mwanaume simkumbuki jina)naiomba tafadhari

- Amemshirikisha Seif Kisauji huyu Kisauji ndio alokuwa na ile bendi ya Tanga ta Taarab inaitwa Babloom Modern.
 
Japo thread ni ya kitambo:

1- Bi Malika - Staki Staki
2- Bi Malika - Wape Wape(Huu yeye na mwanahela mmoja aliurudia wa mwenzake)
3- Mwanahela(Golden Stars wa Tanga) - Rabbi Sinipe Mapenzi
4- Golden Stars - Piga Parapanda (ule mimi mwenyewe kwenda, mimi kwenda sokoni, kununua kabichi bidhaa, pelekea bibi jumbani, piga parapanda, sikia nani taumia x2)
5- Siti bint Saad - Subalkheir
6- Sabah Salum - Aso Mtu Ana Mungu
7- Shakila(JKT) - Nahodha
8- JKT - Mapenzi yananitatiza
9- Prof Moh'd Mrisho - Kijungu (kitafinikwa, kitakorogwa, kitapakuliwaaa)
10- Ali Star(TOT) - Zumbukuku
11- Khadija Kopa(TOT) - Gwinji (eti naye ajitambe ajitambe, ajitambe ana nini)
12 - Ikhwan Safaa - Nipepee
13- Issa Matona - Mke Kumpa Talaka
14- Bima Taarab - Ni bure zenu fitina
15- Jasmin Musical(warundi hawa) - Pendo kazi yetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom