Tujikumbushie enzi za malani.

anin-gift

Senior Member
Feb 17, 2012
165
0
Wana chit-chat heshima mbele, kwa watoto wa 90 miongoni mwa michezo ilikuwa malani, mitaani kulikuwa na mabingwa ambao waliogopeka kwa malani maana hao unaweza rusha ngumi au kulia. Shuleni vivyo hivyo. Hebu tujikumbushie enzi hizo za malani, tukianzia: kichwa kikubwa kusikitika huwezi, pua ka kona ya sabuni, tumbo kubwa ka unanyea humo humo, nywele ka mkutano wa nzi, tiririka
 

Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,653
2,000
ilikuwa inachagizwa na twende twende twende mdomo mkubwa km bakuli, twende twende unavuta pumzi hapo, umekomaa mpaka ukitema mate yanadunda! Shingo km pila la mavi, puma kubwa kama Kiutuli! Hahaaa ilikuwa raha sana kulikuwa na watemi hao humchokozi
 

anin-gift

Senior Member
Feb 17, 2012
165
0
ilikuwa inachagizwa na twende twende twende mdomo mkubwa km bakuli, twende twende unavuta pumzi hapo, umekomaa mpaka ukitema mate yanadunda! Shingo km pila la mavi, puma kubwa kama Kiutuli! Hahaaa ilikuwa raha sana kulikuwa na watemi hao humchokozi

nilisahau mkuu hii twende twende, nakwambia kulikuwa na machampioni hao utadhani wamesomea, m2 ukichemka unaenda kumwita darasani kwao kwa kumnunulia k2 then raha tupu.
 

anin-gift

Senior Member
Feb 17, 2012
165
0
twende,twende twende, domo kubwa chapati hukunji, sura imekakamaa kama umelamba limao, mimacho imekutoka ka umetajiwa siku yako ya kufa, twende twende mashavu ka unapuliza moto.
 

snochet

JF-Expert Member
Mar 31, 2011
1,341
2,000
twende twende,mashavu kama mimba ya panya,pua kama kona ya sambusa,mwone mrefu hadi unauza karanga kwenye ndege,maskio kama upawa wa uji...twende twende,.....mnakumbuka zile za babaangu anaendesha mkoko 1,baba ako mkoko 2,mpaka mnafika inakuwa mkoko10,mara baba yangu one-moja,ukitegea mwenzako aseme babaake two-mbili(tumbili)
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,084
2,000
Twende Twende Midevu kama Nyenyere wanalamba sukari,twende twende tumbo kama bunju,twende twende mrefu ka ngongoti,twende twende mfupi ka andunje!!
 

kisoda

Senior Member
Dec 4, 2012
168
0
twende twende tumbo ka pakacha la embe,mat@ko juu juu ka breki za honda,kidevu ka kona ya godoro,mdomo ka kijambio cha kuku!twende twende...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom