Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Ninatizama dirishani ohoo, naona ni mvua inanyesha oho hakuna kilichobakia oho ila ni huzuni na uchungu ehe, mwingine ni Asha usifate mambo ya dunia asha wewe kumbuka wemaaa Tabora jazz. Tulikuwa tunakacha Math siku nyingine na physics ili kusikia vigongo hivyo. Mhu.
Mi nakumbuka nilikua ndo mtoto so kutumwa mara dukani mara kanunue mkaa mara nenda kwa flan.... Pia wakubwa walikua wananichukua natoka nao ili wapate gia ya kwenda kuonana na wapenzi wao eti mzazi asiwafikirie vibaya mi mdogo Naenda nao hahahaa hahahahahaah
 
Nilipenda External Service sana nikiwa likizo nilikuwa namsikiliza Eda Sanga akituma salam na miziki ya akina Michael Jackson, Cool and the Gang, Bonny M halafu habari toka wapigania uhuru waliokuwa wanatumia External kwenye propaganda zao. Hapo uzalendo ulitujaa tunataja kanuni, imani bila kukosea nukta. We baba wee. Yako wapi sasa. Radio nyingi lakini hakuna chochote watoto watajua.
Elimu ya watu wazima, Kilimo chetu, umoja wa mataifa week hiii.
 
Mi nakumbuka nilikua ndo mtoto so kutumwa mara dukani mara kanunue mkaa mara nenda kwa flan.... Pia wakubwa walikua wananichukua natoka nao ili wapate gia ya kwenda kuonana na wapenzi wao eti mzazi asiwafikirie vibaya mi mdogo Naenda nao hahahaa hahahahahaah
Mdogo wangu wa kiume aliipata, kila nikienda likizo yeye ndo bodyguard wangu ili baba asinikatalie.
 
Back
Top Bottom