Poa mwana ! enzi hizo Mchwampaka ! aliwakamata madogo wamewasha moto kiwanjani saa sita mchana wanaota! kumbe walikuwa wanakamua jani kiulaini walipomuona wakatupa vipisi kwenye moto!
Wewe lazima utakuwa kwenye late 50's!! duh, mazee, wewe ni mkuda na mnoko flani hivi....hooooooovyo sana kujifanya siriasi wakati wote!!
tulia, upo kwenye web hapa! kama hupendi hizi za shule, basi nenda kwenye zile za EPA!! mijitu mingine bwana, buree ghali.🙁😕
1. Mwalimu Ibara (Hatibu) - ticha huyu alikuwa anatumia ibara/vifungu hewa vya Katiba kutoa adhabu za kiutani ila wanafunzi tulikuwa tunazitekeleza kweli mfano aliwakuta wanafunzi wanagombana akawapa adhabu ya kufagia darasa mpaka ligi kuu ya Tanzania na mwaka huo simba na yanga zilikacha kucheza mchezo wa ligi hivyo ligi haikuisha...
2. Mwalimu Miti Mingi - huyu na Mchwa Mpaka walikuwa damu damu katika harakati za kuvunja miiko ya HakiElimu na Kuleana ya 'Chapa Kazi Sio Mtoto', da Miti alikuwa na kasauti kaupole hako ila akikucharaza bakora ilikuwa balaa...
3. Mwalimu Mbaga - mzungu wetu huyu alikuwa mpole sana utadhani hua ila utundu ukizidi darasani alikuwa anaita walimu wakali watuchape ila ikifika fimbo ya pili utasikia mama wa watu anasema 'basi chapa tosha tosha'...
4. Mama Semhando - huyu mama alikuwa anatoa somo la Kiswahili la aina yake, ukiwa njuka lazima akutoe mbele ya darasa na akupe neno ulielezee mbele ya darasa...
5. Mwalimu Matley - da mwalimu wa namba huyu alituchapa sana huyu kidato cha kwanza ila akawa besti sana kidato cha pili, nakumbuka sana maswali yake ya vidoti...
6.Mwalimu Mashanga - kinara wa migomo ya walimu, aliitetemesha sana sirikali...
7. Mama Idi - huyu alikuwa my fevoriti maelezo zaidi baadae...
Eeeeee bwanaeee,Mchwampaka alikuwa noma kichizi;ila kuna mwalimu wangu alikuwa anatufundisha physics Mwl.Mosha alikuwa peace sana;tatizo lake ni kwamba alikuwa napenda sana kuvuta fegi mara anakohoa mara samahani kidogo kumbe anaenda kuongeza nguvu kwa madai yake huku hajui kama anajiua mwenyewe taratibu.
Kiboko ya wote kuna Mwl.Matey alikuwa anatufundisha ugonjwa wa Taifa,acha kabisa ukichemsha katika hilo somo mwenyewe unakosa amani kabla hata hujaonana nae alikuwa anachapa bakora vibaya,utasikia shika meza nyooka ukijitia hujui anakuondoa stand;watu wengi walikuwa wanamnyaa huyu mchizi ile mbayaaaaa.
Chama letu lidumu zaidi na zaidi maana yake tumetokea mbali Azania Boys hadi hivi sasa sijui ni nini vile maana wamechanganyika na mademu duh!
Azania imechanganyika na mademu? Hii kweli balaa! Yani hamna hata fleva tena ya chama letu!! Mimi nakumbuka kiunganishi mashuhuri cha mwalimu Mitimingi hasa, akiongea kiingereza. Badala ya kusema kiufasaha 'another thing' alikuwa akitumia sana neno 'anaza sing' , basi kwetu ikawa kila akija skuli balaza inakuwa tunamwita anaza sing.
Halafu kulikuwa na nunda fulani pale shule linaitwa "batman", sijui bado lipo maana nakumbuka kuna siku lilimzaba Mchwa bonge la kofi kwenye school baraza.I wonder litakuwa lina shughuli gani siku hizi.
Mwalimu Kijazi wa Biolojia sijui bado yuko au vipi. NIlikuwa nammaindi sana, sema basi tu!
Mwalimu Dathi yule mhindi, sijui bado yuko hai, alikuwa mzuri sana wa Chemistry. NIkimuona tena lazima nimpe zawadi.
"Azania, Azania, Azania our school, we look at you with pride, you are known far and wide, you are always our best, we will never forget you",
Wana wa Azania mnakumbuka hii school anthem??
BIla kumsahau Mheshimiwa sana, mwalimu Kente mzee wa Mabuga!!
Yah sio kama ni wabaguzi wa gender ila flava la chama limepungua maana hata huwezi kuita AZABOY tena maana ndio hivyo tena.
Hivi huyu batman unyemsemea ndio huyu aliyemaliza miaka ya 94/95 alikuwa anatembea na paketi ya embassy kwenye mfuko wa shati.
Mama dathi yah alikuwa makini kwenye kemia.
Mimi nimesoma enzi za Kwayu akiwa head master ,mama Massawe akiwa second mis. Mchompaka (MchwaMpaka) huyu alikuwa noma akiwa dicpline master na kanifundisha geography,Mkongo,Mitimingi,Mosha,mama wa kihindi Dath chemistry.........,
Nimekusoma mkuu wakati Kwayu anakuja sisi ndio tulikuwa tunamalizia basi wacha atutandike mijeledi maana sheria yetu ilikuwa hatuchomekei mashati na yeye anasema a smart guy has to tuck in his shirt basi tulikoma mkuu.Mama Massawe alikuwa bado hajawa second ila Mitimingi alikuwa mtaalamu mzur sana wa book keeping vipi na chips dume bado zilikuwepo
jamani na mi nimo,nimepiga O'level na nimemaliza seven years ago,Kwayu akiwa headmaster! Muchwampaka kipindi hicho alishakuwa mpole baada ya kupiga mtoto wa watu na kumalizia nguvu za kiume! Tuliacha simba mmoja anaitwa Mulokozi,huyu tabu tupu..muchwampaka haoni ndani! Kipindi chetu kule 'msituni' waliweka "vimbweta" so tulikuwa tunakula stori na buku huko,alafu kulikuwa na mbu wana hasira..wakikung'ata..!! Kulikuwa na 'POGO' aka mihogo ya jamaa m1 alikuwa anaitwa "husein" na vidagaa vya kukaanga. Aisee,studying Azania was a wonderful experince in real life ya mtoto wa kawaida kabisa wa kibongo!
makitaja Azania sijui najisikiaje, mdogo wangu alimaliza pale 2003 ila hizo bangi anazopuliza ni balaa, na anasema walikuwa wanavuta hadi class