Martin George
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,695
- 1,470
Ni vema tu wakati tunatafakari mustakabali wa madini yetu na mikataba yake, basi tujikumbushe pia ni kina nani tuliwahi kuwaamini kama taifa na kuwapa dhamana ya kuisimamia sekta ya Nishati na Madini. Na je, waliisaidiaje sekta hii? Mimi nawakumbuka mzee Daniel Yona ambaye baadae alifungwa jela, pia Msabaha na Karamagi walioondolewa na Richmond scandal, mwingine ni Ngeleja ambaye yupo bungeni akiongoza kamati ya sheria, tunaye pia Simbachawene anayehudumu kama Waziri wa Tamisemi kwa sasa na mwisho ni mwanasayansi mbobezi mzee Muhongo aliyeondoka kwa tuhuma za makanikia ya Acacia. Kama kina niliyemsahau mtanikumbusha ili historian iweze kumtambua na kumkumbuka.